Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Psalms 150 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Msifuni Mwenyezi Mungu kwa ukuu wake

1Msifuni Mwenyezi Mungu.Msifuni Mungu katika patakatifu pake,msifuni katika mbingu zake kuu.

2Msifuni kwa matendo yake makuu,msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

3Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta,msifuni kwa kinubi na zeze,

4msifuni kwa matari na kucheza,msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,

5msifuni kwa matoazi yaliayo,msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

6Kila chenye pumzi na kimsifu Mwenyezi Mungu.Msifuni Mwenyezi Mungu!

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]