Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Job 25 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Bildadi anasema: Mwanadamu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mwenyezi Mungu?

1Ndipo Bildadi Mshuhi akajibu:

2“Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu;yeye huthibitisha amani katika mbingu juu.

3Je, majeshi yake yaweza kuhesabika?Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake?

4Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu?Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi?

5Ikiwa hata mwezi sio mwangavunazo nyota si safi machoni pake,

6sembuse mtu ambaye ni funza:mwanadamu ambaye ni buu tu!”

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]