Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Psalms 23 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Zaburi ya Daudi.

Mwenyezi Mungu mchungaji wetu

1Mwenyezi Mungu ndiye mchungaji wangu,sitapungukiwa na kitu.

2Hunilaza katika malishoya majani mabichi,kando ya maji matulivu huniongoza,

3hunihuisha nafsi yangu.Huniongoza katika njia za hakikwa ajili ya jina lake.

4Hata nikipita katikatiya bonde la uvuli wa mauti,sitaogopa mabaya,kwa maana wewe upo pamoja nami;fimbo yako na mkongojo wakovyanifariji.

5Waandaa meza mbele yangumachoni pa adui zangu.Umenipaka mafuta kichwani pangu,kikombe changu kinafurika.

6Hakika wema na upendo vitanifuatasiku zote za maisha yangu,nami nitakaa nyumbani mwa Mwenyezi Mungumilele.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]