Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Psalms 128 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Wimbo wa kwenda juu.

Thawabu ya kumtii Mwenyezi Mungu

1Heri wale wote wamchao Mwenyezi Mungu,wanaoenda katika njia zake.

2Utakula matunda ya kazi yako;baraka na mafanikio vitakuwa vyako.

3Mke wako atakuwa kama mzabibu uzaaondani ya nyumba yako;wana wako watakuwa kama machipukizi ya mizeitunikuizunguka meza yako.

4Hivyo ndivyo atakavyobarikiwamtu amchaye Mwenyezi Mungu.

5Mwenyezi Mungu na akubariki kutoka Sayunisiku zote za maisha yako,na uone mafanikio ya Yerusalemu,

6nawe ujaliwe kuishi uone watoto wa watoto wako.Amani iwe juu ya Israeli.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]