Side by side with the Father's Heart Bible™ Wimbo wa kwenda juu.
Maombi dhidi ya adui za Israeli
1Wamenitesa sana tangu ujana wangu;Israeli na aseme sasa:
2wamenitesa sana tangu ujana wangu,lakini bado hawajanishinda.
3Wakulima wamelima mgongo wangu,na kufanya mifereji yao mirefu.
4Lakini Mwenyezi Mungu ni mwenye haki;amenifungua toka kamba za waovu.
5Wale wote wanaoichukia Sayunina warudishwe nyuma kwa aibu.
6Wawe kama majani juu ya paa,ambayo hunyauka kabla hayajakua;
7kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake,wala akusanyaye kujaza mikono yake.
8Wale wapitao karibu na wasiseme,“Baraka ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako;tunakubariki katika jina la Mwenyezi Mungu.”