Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Psalms 12 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa sheminithi. Zaburi ya Daudi.

Kuomba msaada

1Mwenyezi Mungu tusaidie, kwa kuwa wacha Mungu wametoweka;waaminifu wametoweka miongoni mwa wanadamu.

2Kila mmoja humwambia jirani yake uongo;midomo yao ya hila huzungumza kwa udanganyifu.

3Mwenyezi Mungu na akatilie mbali midomo yote ya hilana kila ulimi uliojaa majivuno,

4ule unaosema, “Kwa ndimi zetu tutashinda;midomo ni mali yetu, bwana wetu ni nani?”

5“Kwa sababu wanyonge wanaonewa,na wahitaji wanalia kwa uchungu,nitainuka sasa,” asema Mwenyezi Mungu.“Nitawalinda kutokana na walewenye nia mbaya juu yao.”

6Maneno ya Mwenyezi Mungu ni safi,kama fedha iliyosafishwa katika tanuru,iliyosafishwa mara saba.

7Ee Mwenyezi Mungu, utatuweka salamana kutulinda na kizazi hiki milele.

8Watu waovu huenda wakiringa kila mahaliwakati yule aliye mbaya sanandiye anayeheshimiwa miongoni mwa watu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]