Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Psalms 11 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

Kumtumaini Mwenyezi Mungu

1Kwa Mwenyezi Mungu ninakimbilia.Unawezaje basi kuniambia:“Ruka kama ndege utorokee kwenye mlima wako.

2Hebu tazama, waovu wanapinda nyuta zao;wanaweka mishale kwenye nyuzi zakeili wakiwa gizani, wawapigewalio wanyofu wa moyo.

3Wakati misingi imeharibiwa,mwenye haki anaweza kufanya nini?”

4Mwenyezi Mungu yuko ndani ya Hekalu lake takatifu;Mwenyezi Mungu yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni.Huwaangalia wana wa watu,macho yake yanawachunguza.

5Mwenyezi Mungu huwachunguza wenye haki,lakini nafsi yake inachukia waovuna wale wanaopenda mapigano.

6Atawanyeshea waovu makaa ya moto mkalina kiberiti kinachowaka;upepo wenye joto kali ndio fungu lao.

7Kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mwenye haki,yeye hupenda haki.Wanyofu watauona uso wake.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]