Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Psalms 13 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

Sala ya kuomba msaada

1Hadi lini, Ee Mwenyezi Mungu? Je, utanisahau milele?Utanificha uso wako hadi lini?

2Nitapambana na mawazo yangu hadi lini,na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu?Adui zangu watanishinda hadi lini?

3Nitazame, unijibu, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu.Yatie nuru macho yangu,ama sivyo nitalala usingizi wa mauti.

4Adui yangu atasema, “Nimemshinda,”nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka.

5Lakini ninategemea upendo wako usiokoma;moyo wangu unashangilia katika wokovu wako.

6Nitamwimbia Mwenyezi Mungu,kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]