Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Psalms 1 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Furaha ya kweli

1Heri mtu yule ambaye haendikatika shauri la watu waovu,wala hasimami katika njia ya wenye dhambi,au kuketi katika baraza la wenye mizaha.

2Bali huifurahia Torati ya Mwenyezi Mungu,naye huitafakari hiyo Torati usiku na mchana.

3Mtu huyo ni kama mti uliopandwakando ya vijito vya maji,ambao huzaa matunda kwa majira yakena majani yake hayanyauki.Lolote afanyalo hufanikiwa.

Huzuni ya waovu

4Sivyo walivyo waovu!Wao ni kama makapiyanayopeperushwa na upepo.

5Kwa hiyo waovu hawatastahimili hukumu,wala wenye dhambi katika kusanyiko la wenye haki.

6Kwa maana Mwenyezi Mungu huziangalia njia za mwenye haki,bali njia za waovu zitaangamia.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]