Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Psalms 2 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Mfalme aliyechaguliwa na Mwenyezi Mungu

1Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya,na makabila ya watu kula njama bure?

2Wafalme wa dunia wanajipangana watawala wanajikusanyadhidi ya Mwenyezi Munguna dhidi ya Mpakwa Mafuta wake.

3Wanasema, “Tuvunje minyororo yaona kuvitupilia mbali vifungo vyao.”

4Yeye anayetawala mbinguni hucheka,Bwana huwadharau.

5Kisha huwakemea katika hasira yakena kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema,

6“Nimemtawaza Mfalme wangujuu ya Sayuni,mlima wangu mtakatifu.”

Ushindi wa mfalme

7Nitatangaza amri ya Mwenyezi Mungu:Yeye aliniambia, “Wewe ni Mwanangu;leo mimi nimekuwa Baba yako.

8Niombe, nami nitayafanya mataifakuwa urithi wako,na miisho ya dunia kuwa milki yako.

9Utawapondaponda kwa fimbo ya chuma,na kuwavunjavunja kama chombo cha mfinyanzi.”

10Kwa hiyo, ninyi wafalme, kuweni na hekima;mwonyeke, enyi watawala wa dunia.

11Mtumikieni Mwenyezi Mungu kwa hofuna mshangilie kwa kutetemeka.

12Mbusu Mwana, asije akakasirikanawe ukaangamizwa katika njia yako,kwa maana hasira yake inaweza kuwaka ghafula.Heri wote wanaomkimbilia.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]