Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Psalms 15 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Zaburi ya Daudi.

Kitu Mwenyezi Mungu anachotaka

1Mwenyezi Mungu, ni nani awezaye kukaakatika Hekalu lako?Nani awezaye kuishikatika mlima wako mtakatifu?

2Ni yule aendaye pasipo mawaa,atendaye yaliyo haki,asemaye kweli toka moyoni mwake,

3na hana masingizio ulimini mwake,asiyemtenda jirani yake vibaya,na asiyemsingizia mwenzake,

4ambaye humdharau mtu mbaya,lakini huwaheshimu wale wamwogopao Mwenyezi Mungu,yule atunzaye kiapo chakehata kama anaumia.

5Yeye akopeshaye fedha yake bila riba,na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia.Mtu afanyaye hayakamwe hatatikisika.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]