Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Psalms 5 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Kwa mwimbishaji. Kwa filimbi. Zaburi ya Daudi.

Sala kwa ajili ya ulinzi wakati wa hatari

1Ee Mwenyezi Mungu, tegea sikio maneno yangu,uangalie kupiga kite kwangu.

2Sikiliza kilio changu ili unisaidie,Mfalme wangu na Mungu wangu,kwa maana kwako ninaomba.

3Asubuhi, unasikia sauti yangu, Ee Mwenyezi Mungu;asubuhi naleta haja zangu mbele zako,na kusubiri kwa matumaini.

4Wewe si Mungu unayefurahia uovu,kwako mtu mwovu hataishi.

5Wenye kiburi hawawezi kusimama mbele yako,unawachukia wote watendao mabaya.

6Unawaangamiza wasemao uongo.Mwenyezi Mungu huwachukiawanaomwaga damu na wadanganyifu.

7Lakini mimi, kwa rehema zako kuu,nitakuja katika nyumba yako,kwa unyenyekevu, nitasujudukulielekea Hekalu lako takatifu.

8Niongoze katika haki yako, Ee Mwenyezi Mungu,kwa sababu ya adui zangu,nyoosha njia yako mbele yangu.

9Hakuna neno kinywani mwao linaloweza kuaminika,mioyo yao imejaa maangamizi.Koo lao ni kaburi lililo wazi,kwa ndimi zao, wao hunena udanganyifu.

10Uwatangaze kuwa wenye hatia, Ee Mungu!Hila zao ziwe anguko lao wenyewe.Wafukuzie mbali kwa sababu ya dhambi zao nyingi,kwa kuwa wamekuasi wewe.

11Lakini wote wanaokimbilia kwako na wafurahi,waimbe kwa shangwe daima.Ueneze ulinzi wako juu yao,ili wale wanaolipenda jina lakowapate kukushangilia.

12Kwa hakika, Ee Mwenyezi Mungu, unawabariki wenye haki,unawazunguka kwa wema wako kama ngao.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]