Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Psalms 8 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Kwa mwimbishaji. Mtindo wa gitithi. Zaburi ya Daudi.

Utukufu wa Mwenyezi Mungu na heshima ya mwanadamu

1Ee Mwenyezi Mungu, Bwana wetu,tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote!Umeuweka utukufu wakojuu ya mbingu.

2Midomoni mwa watoto wachanga na wanaonyonyaumeamuru sifa,kwa sababu ya watesi wako,kumnyamazisha adui na mlipiza kisasi.

3Nikiziangalia mbingu zako,kazi ya vidole vyako,mwezi na nyota,ulizoziratibisha,

4mwanadamu ni kitu gani hata unamfikiria,binadamu ni nani hata unamjali?

5Umemfanya chini kidogo kuliko viumbe wa mbinguni,ukamvika taji la utukufu na heshima.

6Umemfanya mtawala juu ya kazi za mikono yako;umeweka vitu vyote chini ya miguu yake.

7Mifugo na makundi yote pia,naam, na wanyama wa kondeni,

8ndege wa angani na samaki wa baharini,naam, kila kinachoogelea katika njia za bahari.

9Ee Mwenyezi Mungu, Bwana wetu,tazama jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote!

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]