Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Psalms 20 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

Maombi kwa ajili ya ushindi

1Mwenyezi Mungu na akujibu unapokuwa katika dhiki,jina la Mungu wa Yakobo na liwe kinga yako.

2Na akutumie msaada kutoka patakatifuna akupatie msaada kutoka Sayuni.

3Na azikumbuke dhabihu zako zote,na azikubali sadaka zako za kuteketezwa.

4Na akujalie haja ya moyo wako,na aifanikishe mipango yako yote.

5Tutashangilia kwa furaha utakaposhinda,tutainua bendera zetu kwa jina la Mungu wetu.Mwenyezi Mungu na akupe haja zako zote.

6Sasa nafahamu kuwa Mwenyezi Munguhumwokoa mpakwa mafuta wake,humjibu kutoka mbingu yake takatifukwa nguvu za wokovu wa mkono wake wa kuume.

7Wengine wanatumaini magari ya vita, na wengine farasi,bali sisi tutalitumainia jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wetu.

8Wao wameshushwa chini na kuanguka,bali sisi tunainuka na kusimama imara.

9Ee Mwenyezi Mungu, mwokoe mfalme!Tujibu tunapokuita!

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]