Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Psalms 137 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Maombolezo ya Israeli uhamishoni

1Kando ya mito ya Babeli tuliketi, tukaombolezatulipokumbuka Sayuni.

2Kwenye miti ya hukotulitundika vinubi vyetu,

3kwa maana huko hao waliotutekawalitaka tuwaimbie nyimbo;watesi wetu walidai nyimbo za furaha;walisema, “Tuimbieni wimbo mmojakati ya nyimbo za Sayuni!”

4Tutaimbaje nyimbo za Mwenyezi Mungu,tukiwa nchi ya kigeni?

5Nikikusahau wewe, ee Yerusalemu,basi mkono wangu wa kuume na usahau ujuzi wake.

6Ulimi wangu ushikamane na kaakaa la kinywa changukama sitakukumbuka wewe,kama nisipokufikiri Yerusalemukuwa furaha yangu kubwa.

7Kumbuka, Ee Mwenyezi Mungu, walichokifanya Waedomu,siku ile Yerusalemu ilipoanguka.Walisema, “Bomoa, bomoahata misingi yake!”

8Ee binti Babeli, uliyehukumiwa kuangamizwa,heri yeye atakayekulipiza wewekwa yale uliyotutenda sisi:

9yeye ambaye atawakamata watoto wako wachangana kuwaponda juu ya miamba.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]