Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Psalms 133 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.

Sifa za pendo la undugu

1Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendezandugu wanapoishi pamoja katika umoja!

2Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani,yakitiririka kwenye ndevu,yakitiririka kwenye ndevu za Haruni,hadi kwenye upindo wa mavazi yake.

3Ni kama umande wa Hermoniukianguka juu ya Mlima Sayuni.Kwa maana huko ndiko Mwenyezi Mungu alikoamuru baraka yake,naam, uzima hata milele.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]