Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Psalms 146 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Kumsifu Mwenyezi Mungu mwokozi

1Msifuni Mwenyezi Mungu!Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi Mungu,

2Nitamsifu Mwenyezi Mungu maisha yangu yote;nitamwimbia Mungu wangu sifawakati wote ningali hai.

3Usiweke tumaini lako kwa wakuu,kwa wanadamu ambao hufa,ambao hawawezi kuokoa.

4Roho yao itokapo hurudi mavumbini,siku hiyo hiyo mipango yao yote hukoma.

5Heri yeye ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,ambaye tumaini lake ni katika Mwenyezi Mungu, Mungu wake,

6Muumba wa mbingu na nchi,na bahari na vyote vilivyomo:Mwenyezi Mungu anayedumu kuwa mwaminifumilele na milele.

7Naye huwapatia haki waliodhulumiwa,na kuwapa wenye njaa chakula.Mwenyezi Mungu huwaweka wafungwa huru,

8Mwenyezi Mungu huwafumbua vipofu macho,Mwenyezi Mungu huwainua waliolemewa na mizigo yao,Mwenyezi Mungu huwapenda wenye haki.

9Mwenyezi Mungu huwalinda wagenina kuwategemeza yatima na wajane,lakini hupinga njia za waovu.

10Mwenyezi Mungu atamiliki milele,Mungu wako, ee Sayuni,kwa vizazi vyote.Msifuni Mwenyezi Mungu.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]