Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Psalms 140 ONMM

Side by side with the Father's Heart Bible™

Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.

Kuomba ulinzi wa Mwenyezi Mungu

1Ee Mwenyezi Mungu, niokoe, kutoka kwa watu waovu;nilinde na watu wenye jeuri,

2ambao hupanga mipango mibaya mioyoni mwao,na kuchochea vita siku zote.

3Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka,sumu ya nyoka iko midomoni mwao.

4Ee Mwenyezi Mungu, niepushe na mikono ya waovu;nilinde na watu wenye jeuriwanaopanga kunikwaza miguu yangu.

5Wenye kiburi wameficha mtego wa kuninasa,wametandaza kamba za wavu wao,wametega mitego kwenye njia yangu.

6Ee Mwenyezi Mungu, ninakuambia, “Wewe ni Mungu wangu.”Ee Mwenyezi Mungu, usikie kilio changu na kunihurumia.

7Ee Bwana Mungu Mwenyezi, Mwokozi wangu mwenye nguvu,unikingaye kichwa changu siku ya vita:

8Ee Mwenyezi Mungu, usiwape waovu matakwa yao,usiache mipango yao ikafanikiwa,wasije wakajisifu.

9Vichwa vya wanaonizunguka vifunikwe na shidazilizosababishwa na midomo yao.

10Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie!Na watupwe motoni,katika mashimo ya matope,wasiinuke tena kamwe.

11Wasingiziaji wasifanikiwe katika nchi;maafa na yawawinde watu wenye jeuri.

12Najua kwamba Mwenyezi Mungu huwapatia maskini haki,na kuitegemeza njia ya mhitaji.

13Hakika wenye haki watalisifu jina lako,na waadilifu wataishi mbele zako.

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]