Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Jonah 2 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 Then Jonah prayed to our Father from inside the fish: Akiwa ndani ya tumbo la samaki, Yona alimwomba Mwenyezi Mungu, Mungu wake.
2 In my distress I called to my Father, and he answered me; from the grave's belly I cried for help, and you heard my voice. Akasema: “Katika shida yangu nalimwita Mwenyezi Mungu, naye akanijibu. Kutoka kina cha kaburi niliomba msaada, nawe ukasikiliza kilio changu.
3 You hurled me into the deep, into the heart of the seas, and the currents swirled around me; all your breakers and your waves swept over me. Ulinitupa kwenye kilindi, ndani kabisa ya moyo wa bahari, mikondo ya maji ilinizunguka; mawimbi yako yote na viwimbi vilipita juu yangu.
4 Then I said, 'I have been driven away from your sight; yet I will look again toward your holy temple.' Nikasema, ‘Nimefukuziwa mbali na uso wako, hata hivyo nitatazama tena kuelekea Hekalu lako takatifu.’
5 The waters closed in over me to the point of death; the deep surrounded me; seaweed was wrapped around my head. Maji yaliyonimeza yalinitisha, kilindi kilinizunguka; mwani ulijisokota kichwani pangu.
6 I sank down to the roots of the mountains; the earth shut its gates behind me forever. But you brought my life up from the pit, my Father. Nilizama chini sana hata pande za mwisho za milima, makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele. Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni, Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu.
7 As my life was ebbing away, I remembered my Father, and my prayer rose to you, to your holy temple. “Uhai wangu ulipokuwa unatoka, nilikukumbuka wewe, Mwenyezi Mungu, nayo maombi yangu yalikufikia wewe, katika Hekalu lako takatifu.
8 Those who cling to worthless idols walk away from the love that could be theirs. “Wale watu wanaoshikilia sanamu batili hupoteza neema yao.
9 But I will sacrifice to you with grateful praise; I will keep every vow I have made. Salvation belongs to our Father! Lakini mimi nitakutolea dhabihu, kwa sauti za shukrani na shangwe. Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza. Wokovu watoka kwa Mwenyezi Mungu.”
10 Then our Father spoke to the fish, and it vomited Jonah out onto the dry land. Basi Mwenyezi Mungu akamwamuru yule samaki, naye akamtapika Yona katika nchi kavu.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]