Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Proverbs 9 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 Wisdom has built her house; she has hewn out her seven pillars. Hekima amejenga nyumba yake; amechonga nguzo zake saba.
2 She has slaughtered her animals; she has mixed her wine; she has also set her table. Ameandaa nyama na kuchanganya divai yake; pia ameandaa meza yake.
3 She has sent out her young women to call from the highest places of the town: Amewatuma wajakazi wake, naye huita kutoka mahali pa juu sana pa mji.
4 "Whoever is simple, let him come in here!" To the one who lacks sense she says, Anawaambia wale wasio na akili, “Wote ambao ni wajinga na waje hapa!
5 "Come, eat my bread and drink the wine I have mixed. Njooni, mle chakula changu na mnywe divai niliyoichanganya.
6 Leave your simple ways, and live; walk in the way of insight." Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi; tembeeni katika njia ya ufahamu.
7 Whoever corrects a mocker brings abuse on himself, and whoever rebukes a wicked man gets hurt. “Yeyote anayemkosoa mwenye dhihaka hukaribisha matusi; yeyote anayekemea mtu mwovu hupatwa na matusi.
8 Do not rebuke a mocker, or he will hate you; rebuke a wise man, and he will love you. Usimkemee mwenye dhihaka, la sivyo atakuchukia; mkemee mwenye hekima naye atakupenda.
9 Instruct a wise man and he will grow wiser; teach a righteous man and he will learn even more. Mfundishe mtu mwenye hekima naye atakuwa na hekima zaidi; mfundishe mtu mwadilifu naye atazidi kufundishika.
10 The fear of our Father is the beginning of wisdom, and the knowledge of the Holy One is insight. “Kumcha Mwenyezi Mungu ndicho chanzo cha hekima, na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.
11 For by me your days will be multiplied, and years will be added to your life. Kwa maana kwa msaada wangu siku zako zitakuwa nyingi, na miaka itaongezwa katika maisha yako.
12 If you are wise, you are wise for yourself; if you scoff, you alone will bear it. Kama wewe una hekima, hekima yako itakupa tuzo; kama wewe ni mtu wa mzaha, wewe mwenyewe ndiwe utateseka.”
13 The woman Folly is loud; she is naive and knows nothing. Mwanamke aitwaye Mpumbavu ana kelele; hana adabu na hana maarifa.
14 She sits at the door of her house, on a seat at the highest places of the town, Huketi kwenye mlango wa nyumba yake, kwenye kiti katika mahali pa juu sana pa mji,
15 calling to those who pass by, who are going straight on their way: akiita wale wanaopita karibu, wanaoenda moja kwa moja kwenye njia yao.
16 "Whoever is simple, let him come in here!" And to the one who lacks sense she says, Anawaambia wale wasio na akili, “Wote ambao ni wajinga na waje hapa ndani!
17 "Stolen water is sweet, and bread eaten in secret is pleasant." Maji yaliyoibiwa ni matamu; chakula kinacholiwa sirini ni kitamu!”
18 But he does not know that the dead are there, that her guests are in the depths of the grave. Lakini hawajui hata kidogo kuwa wafu wako humo, kwamba wageni wake huyo mwanamke wako katika vilindi vya Kuzimu.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]