Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Proverbs 8 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 Does not Wisdom call out, and understanding raise her voice? Je, hekima haitani? Je, ufahamu hapazi sauti?
2 Atop the heights along the way, where the paths meet, she takes her stand. Juu ya miinuko karibu na njia, penye njia panda, ndipo asimamapo;
3 Beside the gates, at the entrance to the city, at the doorways she cries aloud: kando ya malango yaelekeayo mjini, kwenye maingilio, hulia kwa sauti kubwa, akisema:
4 "To you, all people, I call out; my voice reaches all humanity. “Ni ninyi watu, ninaowaita; ninapaza sauti yangu kwa wanadamu wote.
5 You who are simple, learn prudence; you who are foolish, gain an understanding heart. Ninyi ambao ni wajinga, pateni akili; ninyi mlio wapumbavu, pateni ufahamu.
6 Listen, for I speak of noble things, and everything I say is right. Sikilizeni, kwa maana nina mambo muhimu ya kusema; ninafungua midomo yangu kusema lililo sawa.
7 My mouth utters truth, for my lips detest wickedness. Kinywa changu husema lililo kweli, kwa maana midomo yangu huchukia uovu.
8 All the words of my mouth are righteous; none of them is twisted or crooked. Maneno yote ya kinywa changu ni ya haki; hakuna mojawapo lililopotoka au la ukaidi.
9 To the one who understands they are all clear, and right to those who find knowledge. Kwa wenye kupambanua, yote ni sahihi; hayana kasoro kwa wale wenye maarifa.
10 Take my instruction instead of silver, and knowledge rather than choice gold, Chagua mafundisho yangu badala ya fedha, maarifa badala ya dhahabu safi,
11 for wisdom is better than jewels, and nothing you desire can compare with her. kwa maana hekima ina thamani kuliko marijani na hakuna chochote unachohitaji kinacholingana naye.
12 I, Wisdom, dwell with prudence, and I find knowledge and discretion. “Mimi hekima, nakaa pamoja na busara; ninamiliki maarifa na busara.
13 The fear of our Father is to hate evil. Pride and arrogance, the evil way, and perverse speech I hate. Kumcha Mwenyezi Mungu ni kuchukia uovu; ninachukia kiburi na majivuno, tabia mbaya na mazungumzo potovu.
14 Counsel is mine, and sound wisdom; I am understanding; strength is mine. Ushauri na hukumu sahihi ni vyangu; nina ufahamu na nina nguvu.
15 By me kings reign, and rulers decree what is just; Kwa msaada wangu wafalme hutawala na watawala hutunga sheria zilizo za haki,
16 by me princes govern, and nobles—all who rule with justice. kwa msaada wangu wakuu hutawala, na wenye vyeo wote watawalao dunia.
17 I love those who love me, and those who search for me find me. Nawapenda wale wanaonipenda, na wale wanaonitafuta kwa bidii wataniona.
18 With me are riches and honor, enduring wealth and righteousness. Utajiri na heshima viko kwangu, utajiri unaodumu na mafanikio.
19 My fruit is better than gold, than the finest gold, and what I yield surpasses choice silver. Tunda langu ni bora kuliko dhahabu safi; kile ninachotoa hupita fedha iliyo bora.
20 I walk in the way of righteousness, along the paths of justice, Natembea katika njia ya unyofu katika mapito ya haki,
21 giving wealth as an inheritance to those who love me, and filling their treasuries. nawapa utajiri wale wanaonipenda na kuzijaza hazina zao.
22 Our Father brought me forth at the beginning of his way, before his works of old. “Mwenyezi Mungu aliniumba mwanzoni mwa kazi yake, kabla ya matendo yake ya zamani;
23 From ages past I was established, from the beginning, before the earth began. niliteuliwa tangu milele, tangu mwanzoni, kabla ya dunia kuumbwa.
24 When there were no deep waters I was brought forth, when there were no springs overflowing with water. Wakati hazijakuwepo bahari, nilikwishazaliwa, wakati hazijakuwepo chemchemi zilizojaa maji;
25 Before the mountains were settled, before the hills, I was brought forth, kabla milima haijawekwa mahali pake, kabla vilima havijakuwepo, nilikwishazaliwa,
26 while he had not yet made the earth and its fields, or the first dust of the world. kabla hajaumba dunia wala mashamba yake au vumbi lolote la dunia.
27 When he set the heavens in place, I was there; when he drew a circle over the face of the deep, Nilikuwepo alipoziweka mbingu mahali pake, wakati alichora mstari wa upeo wa macho kwenye uso wa kilindi,
28 when he set the skies in place above, when he established the springs of the deep, wakati aliweka mawingu juu na kuziweka imara chemchemi za bahari,
29 when he set for the sea its boundary so the waters would not cross their limits, when he marked out the foundations of the earth, wakati aliiwekea bahari mpaka wake ili maji yasivunje agizo lake, na wakati aliweka misingi ya dunia.
30 then I was beside him as a master craftsman, and I was his daily delight, rejoicing before him always, Wakati huo nilikuwa fundi stadi kando yake. Nilijazwa na furaha siku baada ya siku, nikifurahi daima mbele zake,
31 rejoicing in his whole world, and delighting in the human family. nikifurahi katika dunia yake yote nami nikiwafurahia wanadamu.
32 And now, my children, listen to me: blessed are those who keep my ways. “Basi sasa wanangu, nisikilizeni; heri wale wanaozishika njia zangu.
33 Listen to instruction and be wise; do not ignore it. Sikilizeni mafundisho yangu mwe na hekima; msiyapuuze.
34 Blessed is the one who listens to me, watching daily at my gates, waiting beside my doorway. Heri mtu yule anisikilizaye mimi, akisubiri siku zote malangoni mwangu, akingoja kwenye vizingiti vya mlango wangu.
35 For whoever finds me finds life and receives favor from our Father. Kwa maana yeyote anipataye mimi amepata uzima, na kujipatia kibali kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
36 But whoever misses me harms his own soul; all who hate me love death." Lakini yeyote ashindwaye kunipata hujiumiza mwenyewe; na wote wanaonichukia mimi hupenda mauti.”
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]