Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Proverbs 10 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 The proverbs of Solomon: A wise son brings joy to his father, but a foolish son brings grief to his mother. Mithali za Sulemani: Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, lakini mwana mpumbavu huleta huzuni kwa mama yake.
2 Treasures gained by wickedness do not profit, but righteousness rescues from death. Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai, lakini uadilifu huokoa kutoka mautini.
3 Our Father will not let the righteous go hungry, but he thwarts the craving of the wicked. Mwenyezi Mungu hawaachi waadilifu kukaa njaa, lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu.
4 Lazy hands make you poor, but diligent hands bring wealth. Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini lakini mikono yenye bidii huleta utajiri.
5 He who gathers in summer is a prudent son, but he who sleeps during harvest is a son who brings shame. Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi ni mwana mwenye hekima, lakini yeye alalaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.
6 Blessings rest on the head of the righteous, but the mouth of the wicked conceals violence. Baraka huwa taji kichwani mwa mwenye haki, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu.
7 The memory of the righteous is a blessing, but the name of the wicked will rot. Kumbukumbu ya mwenye haki itakuwa baraka, lakini jina la mwovu litaoza.
8 A wise heart accepts commands, but a babbling fool comes to ruin. Mwenye hekima moyoni hupokea maagizo, lakini mpumbavu apayukaye huangamia.
9 Whoever walks in integrity walks securely, but he who makes his ways crooked will be found out. Mtu mwadilifu hutembea salama, lakini mtu aendaye katika njia zilizopotoka atagunduliwa.
10 Whoever winks causes trouble, and a babbling fool comes to ruin. Yeye akonyezaye kwa nia mbaya husababisha huzuni, naye mpumbavu apayukaye huangamia.
11 The mouth of the righteous is a fountain of life, but the mouth of the wicked conceals violence. Kinywa cha mwenye haki ni chemchemi ya uzima, lakini jeuri hufunika kinywa cha mwovu.
12 Hatred stirs up conflict, but love covers all offenses. Chuki huchochea faraka, lakini upendo husitiri mabaya yote.
13 On the lips of the discerning, wisdom is found, but a rod is for the back of one who lacks sense. Hekima hupatikana katika midomo ya wenye kupambanua, lakini fimbo ni kwa ajili ya mgongo wake asiye na ufahamu.
14 The wise store up knowledge, but the mouth of a fool invites ruin. Wenye hekima huhifadhi maarifa, bali kinywa cha mpumbavu hualika maangamizi.
15 The wealth of the rich is their fortified city; the ruin of the poor is their poverty. Mali ya tajiri ni mji wake wenye ngome, bali ufukara ni maangamizi ya maskini.
16 The wage of the righteous leads to life; the gain of the wicked leads to sin. Ujira wa wenye haki huwaletea uzima, lakini mapato ya waovu ni dhambi na mauti.
17 Whoever accepts discipline is on the path to life, but he who ignores correction leads others astray. Anayekubali kuadibishwa yuko katika njia ya uzima, lakini yeyote anayepuuza maonyo hupotosha wengine.
18 Whoever conceals hatred is a liar, and whoever spreads slander is a fool. Yeye afichaye chuki yake ana midomo ya uongo, na yeyote anayeeneza uchonganishi ni mpumbavu.
19 Where words are many, sin is never absent; but whoever holds his tongue is wise. Dhambi haiondolewi kwa maneno mengi, bali wenye busara huzuia ulimi wao.
20 The tongue of the righteous is choice silver; the heart of the wicked is worth little. Ulimi wa mwenye haki ni fedha iliyo bora, bali moyo wa mwovu una thamani ndogo.
21 The lips of the righteous nourish many, but fools die for lack of sense. Midomo ya mwenye haki hulisha wengi, lakini wapumbavu hufa kwa kukosa ufahamu.
22 The blessing of our Father brings wealth, and he adds no sorrow with it. Baraka ya Mwenyezi Mungu hutajirisha, wala haichanganyi na huzuni.
23 Doing wickedness is a game to a fool, but wisdom is the delight of a person of understanding. Mpumbavu hufurahia hila, lakini mtu mwenye ufahamu hupendezwa na hekima.
24 What the wicked dreads will come upon him, but the desire of the righteous will be granted. Kile anachoogopa mwovu ndicho kitakachompata; kile anachoonea shauku mwenye haki atapewa.
25 When the storm has passed, the wicked are gone, but the righteous are established forever. Tufani inapopita, waovu hutoweka, lakini wenye haki husimama imara milele.
26 Like vinegar to the teeth and smoke to the eyes, so is the sluggard to those who send him. Kama siki ilivyo kwa meno na moshi kwa macho, ndivyo alivyo mvivu kwa wale waliomtuma.
27 The fear of our Father lengthens life, but the years of the wicked will be cut short. Kumcha Mwenyezi Mungu huongeza urefu wa maisha, lakini miaka ya mwovu inafupishwa.
28 The hope of the righteous brings joy, but the expectation of the wicked will perish. Tarajio la mwenye haki ni furaha, bali matumaini ya mwovu huwa si kitu.
29 The way of our Father is a refuge for the blameless, but ruin for those who do evil. Njia ya Mwenyezi Mungu ni kimbilio kwa wenye haki, lakini ni maangamizi ya wale watendao mabaya.
30 The righteous will never be shaken, but the wicked will not remain in the land. Kamwe wenye haki hawataondolewa, bali waovu hawatasalia katika nchi.
31 The mouth of the righteous yields wisdom, but the perverse tongue will be cut off. Kinywa cha mwenye haki hutoa hekima, bali ulimi wa upotovu utakatwa.
32 The lips of the righteous know what is acceptable, but the mouth of the wicked, only what is perverse. Midomo ya wenye haki hujua kile chenye kibali, bali kinywa cha mwovu hujua kile kilichopotoka tu.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]