Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Proverbs 21 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 The king's heart is a stream of water in our Father's hand; he turns it wherever he pleases. Moyo wa mfalme uko katika mkono wa Mwenyezi Mungu; huuongoza kama mkondo wa maji, popote apendapo.
2 Every way of a person seems right in their own eyes, but our Father weighs the heart. Njia zote za mwanadamu huonekana sawa kwake, bali Mwenyezi Mungu huupima moyo.
3 To do what is right and just is more pleasing to our Father than sacrifice. Kufanya yaliyo sawa na haki inakubalika zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko dhabihu.
4 Haughty eyes and a proud heart—the lamp of the wicked—are sin. Macho ya kudharau na moyo wa kiburi, ambavyo ni taa ya waovu, vyote ni dhambi!
5 The plans of the diligent lead surely to abundance, but all who are hasty end up in poverty. Mipango ya mwenye bidii huelekeza kwenye faida, kama vile kwa hakika pupa huelekeza kwenye umaskini.
6 Making a fortune by a lying tongue is a fleeting vapor, a deadly trap. Mali iliyopatikana kwa ulimi wa uongo ni mvuke upitao upesi na mtego wa kufisha.
7 The violence of the wicked will drag them away, because they refuse to do what is just. Jeuri ya waovu itawaburuta mbali, kwa kuwa wanakataa kufanya yaliyo sawa.
8 The way of the guilty is crooked, but the conduct of the pure is upright. Njia ya mwenye hatia ni ya upotovu, bali tabia ya mtu asiye na hatia ni nyofu.
9 Better to live in a corner of the roof than in a shared house with a quarrelsome wife. Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba, kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi.
10 The soul of the wicked craves evil; their neighbor finds no mercy in their eyes. Mtu mwovu hutamani sana ubaya, jirani yake hapati huruma kutoka kwake.
11 When a mocker is punished, the simple grow wise; when the wise are instructed, they gain knowledge. Wakati mwenye mzaha ameadhibiwa, mjinga hupata hekima; wakati mtu mwenye hekima anafundishwa, hupata maarifa.
12 Our Father, the Righteous One, observes the house of the wicked and brings the wicked to ruin. Mwenye Haki huyajua yanayotendeka katika nyumba za waovu, naye atawaangamiza waovu.
13 Whoever shuts their ears to the cry of the poor will also cry out and not be answered. Mtu akiziba masikio asisikie kilio cha maskini, yeye pia atalia, wala hatajibiwa.
14 A gift given in secret soothes anger, and a bribe slipped into the cloak calms strong wrath. Zawadi inayotolewa kwa siri hutuliza hasira, na rushwa iliyofichwa kwenye nguo hutuliza ghadhabu kali.
15 When justice is done, it is a joy to the righteous but terror to those who do evil. Wakati haki imetendeka, huleta furaha kwa wenye haki, bali hofu kwa watenda maovu.
16 A person who strays from the way of understanding will rest in the assembly of the dead. Mtu anayepotea kutoka mapito ya ufahamu, hupumzika katika kundi la waliokufa.
17 Whoever loves pleasure will become poor; whoever loves wine and oil will never grow rich. Mtu apendaye anasa atakuwa maskini, yeyote apendaye mvinyo na mafuta kamwe hatakuwa tajiri.
18 The wicked become a ransom for the righteous, and the treacherous for the upright. Waovu huwa fidia kwa ajili ya wenye haki, nao wasio waaminifu kwa ajili ya wanyofu.
19 Better to live in a desert land than with a quarrelsome and complaining wife. Ni afadhali kuishi jangwani kuliko kuishi na mke mgomvi na mkorofi.
20 Precious treasure and oil are in the home of the wise, but a fool devours all he has. Katika nyumba ya mwenye hekima kuna akiba ya vyakula vizuri na mafuta, lakini mtu mpumbavu hutafuna vyote alivyo navyo.
21 Whoever pursues righteousness and faithful love will find life, righteousness, and honor. Yeye afuatiaye haki na upendo hupata uzima, mafanikio na heshima.
22 A wise person scales the city of the mighty and brings down the stronghold they trust in. Mtu mwenye hekima huushambulia mji wa wenye nguvu, na kuangusha ngome wanazozitegemea.
23 Whoever guards their mouth and tongue keeps themselves out of trouble. Yeye alindaye kinywa chake na ulimi wake hujilinda na maafa.
24 "Mocker" is the name of the proud and arrogant who acts with outrageous insolence. Mtu mwenye kiburi na majivuno, “Mdhihaki” ndilo jina lake; hutenda mambo kwa kiburi kilichozidi.
25 The craving of a lazy person kills him, for his hands refuse to work. Kutamani sana kwa mvivu kutakuwa kifo chake, kwa sababu mikono yake haitaki kufanya kazi.
26 All day long the craving grows, but the righteous give and do not hold back. Mchana kutwa hutamani zaidi, lakini mnyofu hutoa pasipo kuzuia.
27 The sacrifice of the wicked is detestable—how much more when brought with evil intent. Dhabihu ya mtu mwovu ni chukizo; si ni chukizo zaidi ikitolewa kwa nia mbaya!
28 A false witness will perish, but whoever listens will testify with lasting effect. Shahidi wa uongo ataangamia, bali maneno ya mwenye kusikia yatadumu.
29 The wicked put on a bold face, but the upright give thought to their ways. Mtu mwovu ana uso wa ushupavu, bali mtu mnyofu huzifikiria njia zake.
30 There is no wisdom, no understanding, no counsel that can stand against our Father. Hakuna hekima, wala akili, wala mpango unaoweza kufaulu dhidi ya Mwenyezi Mungu.
31 The horse is made ready for the day of battle, but victory belongs to our Father. Farasi huandaliwa kwa ajili ya siku ya vita, bali ushindi huwa kwa Mwenyezi Mungu.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]