Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Proverbs 20 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 Wine is a mocker, strong drink a brawler, and whoever staggers under it is not wise. Mvinyo ni mdhihaki na kileo ni mgomvi; yeyote apotoshwaye navyo hana hekima.
2 The terror of a king is like the growl of a lion; whoever provokes him to anger forfeits his own life. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; yeye amkasirishaye hupoteza uhai wake.
3 It is an honor for a person to keep clear of strife, but every fool is quick to quarrel. Ni kwa heshima ya mtu kujitenga ugomvi, bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana.
4 A lazy person will not plow in autumn; so at harvest he looks for a crop and finds nothing. Mvivu halimi kwa majira; kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama lakini hapati chochote.
5 The purposes of a person's heart are deep waters, but one who has understanding draws them out. Makusudi ya moyo wa mwanadamu ni maji yenye kina, lakini mtu mwenye ufahamu huyachota.
6 Many a person proclaims his own loyal love, but a faithful one—who can find? Watu wengi hujidai kuwa na upendo usiokoma, bali mtu mwaminifu ni nani awezaye kumpata?
7 The righteous walk in their integrity; blessed are their children after them! Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama, wamebarikiwa watoto wake baada yake.
8 A king seated on the throne of judgment winnows out all evil with his eyes. Mfalme anapoketi kwenye kiti chake cha ufalme kuhukumu, hupepeta ubaya wote kwa macho yake.
9 Who can say, "I have kept my heart pure; I am cleansed from my sin"? Ni nani awezaye kusema, “Nimeuweka moyo wangu safi; mimi ni safi na sina dhambi?”
10 Unequal weights and unequal measures—our Father detests them both. Mawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti, Mwenyezi Mungu huchukia vyote viwili.
11 Even a child is known by his actions, by whether his conduct is pure and upright. Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake, kama tabia yake ni safi na adili.
12 The hearing ear and the seeing eye—our Father made them both. Masikio yasikiayo na macho yaonayo: Mwenyezi Mungu ndiye alivifanya vyote viwili.
13 Do not love sleep, or you will grow poor; open your eyes, and you will have plenty of bread. Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini, uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba.
14 "Worthless, worthless!" says the buyer—then off he goes and boasts of his bargain. “Haifai, haifai!” asema mnunuzi, kisha huondoka akijisifia ununuzi wake.
15 There is gold and an abundance of jewels, but lips that speak knowledge are a rare treasure. Kuna dhahabu, na marijani kwa wingi, lakini midomo inayonena maarifa ni kito cha thamani.
16 Take the garment of one who puts up security for a stranger; hold it as a pledge when he does so for foreigners. Chukua vazi la yule awekaye dhamana kwa ajili ya mgeni; lishikilie liwe dhamana kwa ajili ya mgeni.
17 Bread gained by deceit tastes sweet, but afterward the mouth is full of gravel. Chakula kilichopatikana kwa hila ni kitamu kwa mwanadamu, bali huishia na kinywa kilichojaa changarawe.
18 Plans are established by counsel; so wage war only with wise guidance. Fanya mipango kwa kutafuta mashauri, ukipigana vita, tafuta maelekezo.
19 A gossip betrays a confidence; so do not keep company with a babbler. Maneno ya kusengenya husababisha kutokuaminika, kwa hiyo mwepuke mtu anayezungumza kupita kiasi.
20 Whoever curses his father or mother—his lamp will be snuffed out in deepest darkness. Ikiwa mtu atamlaani baba yake au mama yake, taa yake itazimwa katika giza nene.
21 An inheritance gained too quickly at the start will not be blessed in the end. Urithi upatikanao haraka mwanzoni, hautabarikiwa mwishoni.
22 Do not say, "I will pay back evil for evil." Wait for our Father, and he will deliver you. Usiseme, “Nitakulipiza kwa ajili ya kosa hili!” Mngojee Mwenyezi Mungu, naye atakuokoa.
23 Our Father detests unequal weights, and dishonest scales are no good. Mwenyezi Mungu anachukia sana mawe ya kupimia ya udanganyifu, nazo mizani zisizo halali hazimpendezi.
24 A person's steps are directed by our Father; how then can anyone understand his own way? Hatua za mtu huongozwa na Mwenyezi Mungu. Anawezaje basi mtu yeyote kuelewa njia yake mwenyewe?
25 It is a trap to rashly dedicate something and only later reconsider the vow. Ni mtego kwa mtu kuweka wakfu kitu kwa haraka na baada ya kitambo kidogo kufikiria tena nadhiri zake.
26 A wise king winnows out the wicked and drives the threshing wheel over them. Mfalme mwenye hekima hupepeta waovu, hulipitisha gurudumu la kupuria juu yao.
27 The human spirit is the lamp of our Father, searching every inmost part. Taa ya Mwenyezi Mungu huchunguza roho ya mwanadamu, huchunguza utu wake wa ndani.
28 Loyal love and faithfulness preserve a king; by loyal love his throne is upheld. Upendo na uaminifu humweka mfalme salama; kiti chake cha ufalme huwa salama kwa upendo.
29 The glory of the young is their strength, but the splendor of the old is gray hair. Utukufu wa vijana ni nguvu zao, mvi ni fahari ya uzee.
30 Wounding blows scrub away evil, and beatings cleanse the inmost parts. Mapigo na majeraha huusafisha ubaya, nayo michapo hutakasa utu wa ndani.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]