Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Proverbs 5 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 My son, pay attention to my wisdom; listen closely to my understanding, Mwanangu, sikiliza kwa makini hekima yangu, sikiliza vizuri maneno yangu ya busara,
2 so that you may guard discretion and your lips may preserve knowledge. ili uweze kutunza busara na midomo yako ihifadhi maarifa.
3 For the lips of the forbidden woman drip honey, and her mouth is smoother than oil, Kwa maana midomo ya mwanamke kahaba hudondoza asali, na maneno ya kinywa chake ni laini kuliko mafuta;
4 but in the end she is bitter as poison, sharp as a double-edged sword. lakini mwisho wake ni mchungu kama nyongo, mkali kama upanga ukatao kuwili.
5 Her feet go down to death; her steps take hold of the grave. Miguu yake hushuka kuelekea kwenye kifo; hatua zake huelekea moja kwa moja kaburini.
6 She gives no thought to the path of life; her ways wander, and she does not know it. Yeye hafikirii kuhusu njia ya uzima; njia zake zimepotoka, lakini yeye hajui.
7 And now, my sons, listen to me, and do not turn away from the words of my mouth. Sasa basi wanangu, nisikilizeni; msiache ninalowaambia.
8 Keep your way far from her, and do not go near the door of her house, Njia zenu ziwe mbali naye, msiende karibu na mlango wa nyumba yake,
9 lest you give your honor to others and your years to one who is cruel, usije ukapoteza heshima yako kwa wengine, na miaka yako kwa aliye mkatili,
10 lest strangers take their fill of your strength, and your hard-earned labors go to the house of a foreigner, wageni wasije wakasherehekea utajiri wako, na jitihada yako ikatajirisha nyumba ya mwanaume mwingine.
11 and at your end you groan, when your flesh and body are consumed, Mwishoni mwa maisha yako utalia kwa uchungu, wakati nyama na mwili wako vimechakaa.
12 and you say, "How I hated discipline, and my heart despised correction! Utasema, “Tazama jinsi gani nilivyochukia adhabu! Tazama jinsi moyo wangu ulivyodharau maonyo!
13 I did not listen to the voice of my teachers or heed my instructors. Sikuwatii walimu wangu, wala kuwasikiliza wakufunzi wangu.
14 I was at the brink of utter ruin in the midst of the assembled congregation." Nimefika ukingoni mwa maangamizi katika kusanyiko la watu wa Mungu.”
15 Drink water from your own cistern, flowing water from your own well. Kunywa maji kwenye kisima chako mwenyewe, maji yanayotiririka kutoka kisima chako mwenyewe.
16 Should your springs overflow in the streets, your streams of water in the public squares? Je, chemchemi zako zifurike katika barabara za mji na vijito vyako vya maji viwanjani?
17 Let them be yours alone, and not shared with strangers. Na viwe vyako mwenyewe, kamwe visishirikishwe wageni.
18 May your fountain be blessed, and rejoice in the wife of your youth, Chemchemi yako na ibarikiwe na umfurahie mke wa ujana wako.
19 a loving doe, a graceful deer. May her love satisfy you always; may you be captivated continually by her love. Kulungu jike apendaye, kulungu mzuri: matiti yake na yakutosheleze siku zote, nawe utekwe daima na upendo wake.
20 Why then, my son, should you be captivated by a forbidden woman and embrace another man's wife? Kwa nini mwanangu, utekwe na mwanamke kahaba? Kwa nini ukumbatie kifua cha mke wa mwanaume mwingine?
21 For a man's ways are before the eyes of our Father, and he examines all the man's paths. Kwa maana njia za mtu ni wazi kabisa mbele za Mwenyezi Mungu, naye huyapima mapito yake yote.
22 The wicked are caught by their own wrongdoing and held fast in the cords of their sin. Matendo mabaya ya mtu mwovu humnasa yeye mwenyewe; kamba za dhambi yake humkamata kwa nguvu.
23 He will die for lack of discipline, and he will go astray because of his great foolishness. Atakufa kwa kukosa nidhamu, akipotoshwa kwa upumbavu wake mwenyewe.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]