Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Proverbs 12 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 Whoever loves discipline loves knowledge, but whoever hates correction is senseless. Yeyote apendaye kuadibishwa hupenda maarifa, bali yeye achukiaye kuonywa ni mpumbavu.
2 A good man obtains favor from our Father, but he condemns the man who schemes evil. Mtu mwema hupata kibali kutoka kwa Mwenyezi Mungu, bali Mwenyezi Mungu humhukumu mwenye hila.
3 No one is established by wickedness, but the root of the righteous will never be moved. Mtu hathibitiki kutokana na uovu, bali mwenye haki hataondolewa.
4 A wife of noble character is her husband's crown, but one who brings shame is like decay in his bones. Mke mwenye tabia nzuri ni taji la mumewe, bali aaibishaye ni kama uozo katika mifupa ya mumewe.
5 The plans of the righteous are just, but the advice of the wicked is deceitful. Mipango ya mtu mwadilifu ni ya haki, bali ushauri wa mwovu ni udanganyifu.
6 The words of the wicked lie in wait for blood, but the speech of the upright rescues the innocent. Maneno ya waovu huotea kumwaga damu, bali maneno ya waadilifu huwaokoa.
7 The wicked are overthrown and are no more, but the house of the righteous will stand. Watu waovu huondolewa na kutoweka, bali nyumba ya mwenye haki husimama imara.
8 A person is praised according to their good sense, but one with a warped mind is despised. Mtu husifiwa kulingana na hekima yake, bali watu wenye akili zilizopotoka hudharauliwa.
9 Better to be lowly and have a servant than to pretend to greatness and go hungry. Heri mtu wa hali ya chini mwenye mtumishi, kuliko kujifanya mtu wa hali ya juu nawe huna chakula.
10 The righteous care for the needs of their animals, but even the mercy of the wicked is cruel. Mtu mwenye haki hujali mahitaji ya mnyama wake, bali matendo ya huruma ya mwovu ni ukatili.
11 Whoever works their land will have plenty of food, but whoever chases worthless pursuits lacks sense. Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele, bali yeye afuataye mambo ya upuzi hana akili.
12 The wicked crave the plunder of evil men, but the root of the righteous yields fruit. Waovu hutamani mateka ya wapotovu, bali shina la mwenye haki hustawi.
13 An evil man is trapped by his sinful talk, but the righteous escapes from trouble. Mtu mwovu hunaswa kwa mazungumzo yake ya dhambi, bali mwenye haki huepuka taabu.
14 From the fruit of their words a person is filled with good things, and the work of their hands comes back to reward them. Kutokana na tunda la midomo yao, watu hujazwa na mambo mema, na kazi ya mikono yao huwaletea thawabu.
15 The way of a fool seems right in his own eyes, but the wise listen to advice. Njia ya mpumbavu huonekana sawa machoni pake mwenyewe, bali mtu mwenye hekima husikiliza ushauri.
16 A fool shows his anger at once, but the prudent overlook an insult. Mpumbavu huonesha kuudhika kwake mara moja, bali mtu wa busara hupuuza matukano.
17 Whoever speaks the truth gives honest testimony, but a false witness tells lies. Shahidi wa kweli hutoa ushuhuda wa kuaminika, bali shahidi wa uongo husema uongo.
18 Reckless words pierce like a sword, but the tongue of the wise brings healing. Maneno ya kipumbavu huchoma kama upanga, bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.
19 Truthful lips endure forever, but a lying tongue lasts only a moment. Midomo isemayo kweli hudumu milele, bali ulimi wa uongo hudumu kwa muda mfupi tu.
20 Deceit fills the hearts of those who plot evil, but joy belongs to those who promote peace. Upo udanganyifu katika mioyo ya wale ambao hupanga mabaya, bali kuna furaha kwa wale wanaoleta amani.
21 No harm overtakes the righteous, but the wicked are full of trouble. Hakuna dhara linalompata mwenye haki, bali waovu wana taabu nyingi.
22 Lying lips are detestable to our Father, but those who act faithfully are his delight. Mwenyezi Mungu anachukia sana midomo idanganyayo, bali hufurahia watu ambao ni wa kweli.
23 The prudent keep their knowledge to themselves, but the heart of fools blurts out foolishness. Mtu mwenye busara hujihifadhia maarifa yeye mwenyewe, bali moyo wa wapumbavu hububujika upumbavu.
24 Diligent hands will rule, but laziness ends in forced labor. Mikono yenye bidii itatawala, bali uvivu huishia katika kazi za utumwa.
25 Anxiety weighs down the heart, but a kind word cheers it up. Moyo wa wasiwasi humlemea mtu, bali neno la fadhili humfurahisha.
26 The righteous guide their neighbor, but the way of the wicked leads them astray. Mtu mwenye haki ni mwangalifu katika urafiki, bali njia ya waovu huwapotosha.
27 The lazy do not roast their game, but the diligent prize their possessions. Mtu mvivu haoki mawindo yake, bali mtu mwenye bidii ana mali ya thamani.
28 In the path of righteousness there is life, and along that way there is no death. Katika njia ya haki kuna uzima; katika mapito hayo kuna maisha ya milele.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]