Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Proverbs 29 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 Whoever is often corrected yet refuses to listen will suddenly be broken beyond healing. Anayekaza shingo baada ya maonyo mengi, ataangamia ghafula, na kamwe hatapona.
2 When the righteous flourish, the people rejoice, but when the wicked rule, the people groan. Wenye haki wanapostawi, watu hufurahi; waovu watawalapo, watu hulia kwa huzuni.
3 A man who loves wisdom brings joy to his father, but a companion of prostitutes squanders his wealth. Mtu apendaye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali aambatanaye na makahaba hutapanya mali yake.
4 By justice a king gives a land stability, but one who is greedy for bribes tears it down. Kwa haki mfalme huipa nchi uthabiti, bali mfalme aliye na tamaa ya rushwa huiangamiza.
5 A man who flatters his neighbor spreads a net for his feet. Yeyote amsifuye jirani yake isivyostahili, anautandaza wavu kuitega miguu yake.
6 An evil man is snared by his own sin, but the righteous sing and rejoice. Mwovu hutegwa na dhambi yake mwenyewe, bali mwenye haki hushangilia na kufurahi.
7 The righteous care about justice for the poor, but the wicked have no such understanding. Mwenye haki hujali haki kwa ajili ya maskini, bali mwovu hajishughulishi na hilo.
8 Mockers set a city ablaze, but the wise calm the anger. Wanaodhihaki huuchochea mji, bali wenye hekima huzuia hasira.
9 When a wise man goes to court with a fool, the fool rages and scoffs, and there is no peace. Mwenye hekima akienda mahakamani na mpumbavu, mpumbavu hukasirika na kudhihaki, wala hakuna amani.
10 The bloodthirsty hate the blameless and seek to kill the upright. Watu wanaomwaga damu humchukia mtu mwadilifu, na hutafuta kumuua mtu mnyofu.
11 A fool vents all his anger, but a wise man holds it back and keeps himself calm. Mpumbavu huonesha hasira yake yote, bali mwenye hekima hujizuia.
12 If a ruler listens to lies, all his officials become wicked. Mtawala akisikiliza uongo, maafisa wake wote huwa waovu.
13 The poor man and the oppressor have this in common: our Father gives sight to the eyes of both. Mtu maskini na mtu mdhalimu wanafanana kwa jambo hili: Mwenyezi Mungu hutia nuru macho yao wote wawili.
14 If a king judges the poor with fairness, his throne will be established forever. Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki, kiti chake kitakuwa thabiti daima.
15 The rod and a word of correction give wisdom, but a child left to himself brings shame to his mother. Fimbo ya maonyo hutia hekima, bali mtoto asiyeonywa humwaibisha mama yake.
16 When the wicked flourish, wrongdoing flourishes, but the righteous will see the wicked's downfall. Waovu wanapostawi, dhambi huongezeka pia; lakini wenye haki wataliona anguko lao.
17 Discipline your son, and he will give you peace; he will bring delight to your heart. Mkanye mwanao, naye atakupa amani; atakuletea furaha unayotamani.
18 Where there is no revelation, the people run wild, but blessed is the one who keeps the law. Mahali pasipo na ufunuo, watu huacha kujizuia, bali ana heri mtu yule anayeitii sheria.
19 A servant cannot be corrected by words alone; though he understands, he will not obey. Mtumishi hawezi kuonywa kwa maneno matupu, hata akielewa, hataitikia.
20 Do you see a man who is hasty with his words? There is more hope for a fool than for him. Je, unamwona mtu azungumzaye kwa haraka? Kuna matumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko yeye.
21 Pamper a servant from childhood, and in the end he will become like an heir. Kama mtu akimdekeza mtumishi wake tangu ujanani, atamletea sikitiko mwishoni.
22 An angry man stirs up strife, and a hot-tempered man commits many sins. Mtu mwenye hasira huchochea ugomvi, naye mtu mwenye hasira ya haraka hutenda dhambi nyingi.
23 A man's pride brings him low, but a humble spirit gains honor. Kiburi cha mtu humshusha, bali mtu mwenye roho ya unyenyekevu hupata heshima.
24 An accomplice of a thief is his own enemy; he hears the curse but says nothing. Anayekubaliana na mwizi ni adui wa nafsi yake mwenyewe; huapishwa lakini hathubutu kushuhudia.
25 Fear of man lays a snare, but whoever trusts in our Father is kept safe. Kuwaogopa watu huwa ni mtego, bali yeyote amtumainiaye Mwenyezi Mungu atakuwa salama.
26 Many seek a ruler's favor, but justice for a person comes from our Father. Wengi hutafuta kusikilizwa na mtawala, bali mtu hupata haki kutoka kwa Mwenyezi Mungu.
27 An unjust man is detestable to the righteous, and an upright person is detestable to the wicked. Mwenye haki huwachukia sana wasio waaminifu; waovu huwachukia sana wenye haki.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]