Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Proverbs 17 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 Better a dry crust eaten in peace than a house full of feasting with strife. Afadhali kula ukoko mkavu ukiwa na amani na utulivu kuliko kukaa kwenye nyumba ya karamu kukiwa na magomvi.
2 A prudent servant will rule over a disgraceful son and will share the inheritance among the brothers. Mtumishi mwenye hekima atamtawala mwana aaibishaye, naye atashirikiana katika urithi kama mmoja wa hao ndugu.
3 The crucible is for silver and the furnace for gold, but our Father tests hearts. Kalibu husafisha fedha na tanuru husafisha dhahabu, bali Mwenyezi Mungu huujaribu moyo.
4 An evildoer listens to wicked lips; a liar listens to a destructive tongue. Mtu mwovu husikiliza midomo mibaya; mwongo husikiliza kwa makini ulimi wa madhara.
5 Whoever mocks the poor insults his Maker; whoever gloats over disaster will not go unpunished. Yeye anaye mdhihaki maskini huonesha dharau kwa Muumba wake; yeyote afurahiaye maafa hataepuka kuadhibiwa.
6 Grandchildren are the crown of the aged, and the glory of children is their parents. Wana wa wana ni taji la wazee, nao wazazi ni fahari ya watoto wao.
7 Fine speech is not fitting for a fool—still less are lying lips for a noble. Midomo yenye uwezo wa ushawishi haimfai mpumbavu: je, ni mibaya kiasi gani zaidi midomo ya uongo kwa mtawala!
8 A bribe seems like a magic charm to the one who gives it; wherever he turns, he thinks he will succeed. Kipawa ni kama kito cha thamani machoni pake yeye aliye nacho; kokote kigeukiapo, hufanikiwa.
9 Whoever covers an offense seeks love, but whoever keeps bringing it up separates close friends. Yeye anayesamehe kosa hudumisha upendo, bali yeyote arudiaye jambo huwatenganisha rafiki wa karibu.
10 A rebuke goes deeper into a person of understanding than one hundred blows into a fool. Karipio humwingia sana mtu mwenye kutambua kuliko mapigo mia kwa mpumbavu.
11 A rebellious man seeks only evil, and a cruel messenger will be sent against him. Mwovu hupenda kuasi tu; mjumbe asiye na huruma atatumwa dhidi yake.
12 Better to meet a bear robbed of her cubs than a fool in his foolishness. Ni afadhali ukutane na dubu aliyenyang’anywa watoto wake, kuliko mpumbavu katika upumbavu wake.
13 If anyone returns evil for good, evil will never leave his house. Ikiwa mtu atalipa baya kwa jema, kamwe ubaya hautaondoka katika nyumba yake.
14 Starting a quarrel is like breaching a dam, so drop the dispute before it bursts out. Kuanzisha ugomvi ni kama kutoboa bwawa la maji; kwa hiyo acha jambo hilo kabla mabishano hayajaanza.
15 Whoever justifies the wicked and whoever condemns the righteous—both alike are detestable to our Father. Yeye asemaye kuwa asiye na haki ana haki, naye asemaye kuwa mwenye haki hana haki: Mwenyezi Mungu huwachukia sana wote wawili.
16 Why should a fool have money in hand to buy wisdom, when he has no heart to learn? Fedha ina faida gani mikononi mwa mpumbavu, wakati yeye hana haja ya kupata hekima?
17 A friend loves at all times, and a brother is born for a time of trouble. Rafiki hupenda wakati wote naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida.
18 One who lacks sense shakes hands on a pledge and puts up security for his neighbor. Mtu mjinga huutoa mkono ili kuweka rehani, naye huweka dhamana kwa jirani yake.
19 Whoever loves wrongdoing loves strife; whoever builds his gate high invites destruction. Yeye apendaye ugomvi apenda dhambi; naye ainuaye sana lango lake hutafuta uharibifu.
20 A crooked heart finds no good, and a twisted tongue falls into trouble. Mtu mwenye moyo mpotovu hawezi kufanikiwa; naye ambaye ulimi wake ni mdanganyifu huanguka kwenye taabu.
21 Whoever fathers a fool brings grief on himself; the father of a godless fool has no joy. Kuwa na mwana mpumbavu huleta huzuni; hakuna furaha kwa baba wa mpumbavu.
22 A joyful heart is good medicine, but a crushed spirit dries up the bones. Moyo wenye furaha ni dawa nzuri, bali roho iliyopondeka hukausha mifupa.
23 A wicked man takes a bribe in secret to pervert the ways of justice. Mtu mwovu hukubali rushwa kwa siri ili kupotosha njia ya haki.
24 A discerning person keeps wisdom in view, but the eyes of a fool wander to the ends of the earth. Mtu wa ufahamu huitazama hekima, lakini macho ya mpumbavu huhangaika hadi kwenye miisho ya dunia.
25 A foolish son is a grief to his father and bitterness to the mother who bore him. Mwana mpumbavu huleta huzuni kwa baba yake na uchungu kwa yeye aliyemzaa.
26 To punish the righteous is not good, nor to flog the noble for their integrity. Si vizuri kumwadhibu mtu asiye na hatia, au kuwapiga sana maafisa kwa ajili ya uadilifu wao.
27 Whoever holds back his words has knowledge, and one with a calm spirit is a person of understanding. Mtu mwenye maarifa hutumia maneno kwa kujizuia, naye mtu mwenye ufahamu ana moyo wa utulivu.
28 Even a fool who keeps silent is thought wise; when he closes his lips, he seems discerning. Hata mtu mpumbavu hudhaniwa kuwa na hekima akinyamaza, na mwenye ufahamu akiuzuia ulimi wake.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]