Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Proverbs 26 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 Like snow in summer and like rain at harvest, honor is not fitting for a fool. Kama theluji wakati wa kiangazi au mvua wakati wa mavuno, ndivyo asivyostahili heshima mpumbavu.
2 Like a fluttering sparrow or a darting swallow, an undeserved curse does not come to rest. Kama shomoro apigapigavyo mabawa yake au mbayuwayu katika kuruka kwake kasi, ndivyo ilivyo laana isiyo na sababu haimpati mtu.
3 A whip for the horse, a bridle for the donkey, and a rod for the backs of fools. Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, nayo fimbo kwa migongo ya wapumbavu!
4 Do not answer a fool according to his foolishness, or you yourself will be like him. Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama wewe mwenyewe utakuwa kama yeye.
5 Answer a fool according to his foolishness, or he will be wise in his own eyes. Mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama atakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe.
6 Whoever sends a message through a fool cuts off his own feet and drinks down violence. Kama vile ilivyo kujikata miguu au kunywa sumu, ndivyo ilivyo kutuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu.
7 Like the legs of a lame man hanging useless is a proverb in the mouth of fools. Kama miguu ya kiwete inavyoning’inia ndivyo ilivyo mithali katika kinywa cha mpumbavu.
8 Like binding a stone in a sling is giving honor to a fool. Kama kufunga jiwe kwenye kombeo, ndivyo ilivyo kumpa mpumbavu heshima.
9 Like a thornbush in the hand of a drunkard is a proverb in the mouth of fools. Kama mwiba kwenye mkono wa mlevi ndivyo ilivyo mithali kinywani mwa mpumbavu.
10 Like an archer who wounds everyone is one who hires a fool or hires any passerby. Kama mpiga upinde ambaye hujeruhi ovyo, ndivyo alivyo yeye aajiriye mpumbavu au yeyote apitaye njiani.
11 As a dog returns to its vomit, so a fool repeats his foolishness. Kama mbwa ayarudiavyo matapiko yake, ndivyo mpumbavu arudiavyo upumbavu wake.
12 Do you see someone wise in his own eyes? There is more hope for a fool than for him. Je, unamwona mtu ajionaye mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Liko tumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake.
13 The lazy person says, "There is a lion in the road! A lion in the streets!" Mvivu husema, “Yuko simba barabarani, simba mkali anazunguka mitaa!”
14 As a door turns on its hinges, so the lazy person turns on his bed. Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake, ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake.
15 The lazy person buries his hand in the dish; it wearies him to bring it back to his mouth. Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, naye huchoka kuupeleka kwenye kinywa chake.
16 The lazy person is wiser in his own eyes than seven who answer wisely. Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe, kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara.
17 Like grabbing a dog by the ears is a passerby who meddles in a quarrel not his own. Kama yeye amkamataye mbwa kwa masikio, ndivyo alivyo mtu apitaye njiani na kujiingiza kwenye ugomvi usiomhusu.
18 Like a madman shooting firebrands, arrows, and death, Kama mwendawazimu atupaye mishale ya moto ya kufisha,
19 so is the one who deceives his neighbor and says, "I was only joking!" ndivyo alivyo mtu amdanganyaye jirani yake na kusema, “Nilikuwa nikifanya mzaha tu!”
20 Without wood a fire goes out, and without a gossip a quarrel dies down. Bila kuni moto huzimika; pasipo uchongezi ugomvi humalizika.
21 As charcoal to embers and wood to fire, so a quarrelsome person kindles strife. Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, na kama kuni kwenye moto, ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuchochea ugomvi.
22 The words of a gossip are like choice morsels; they sink down into the inmost parts. Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu; huingia sehemu za ndani sana za mtu.
23 Like a glaze covering an earthen pot are smooth lips with an evil heart. Kama rangi ing’aayo iliyopakwa kwenye vyombo vya udongo ndivyo ilivyo midomo laini pamoja na moyo mbaya.
24 An enemy disguises himself with his lips, but in his heart he harbors deceit. Mtu mwenye nia ya kudhuru wengine hujificha kwa maneno ya midomo yake, lakini moyoni mwake huficha udanganyifu.
25 When he speaks graciously, do not believe him, for seven abominations fill his heart. Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini, kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake.
26 Though his hatred is hidden by deceit, his wickedness will be exposed in the assembly. Nia yake ya kudhuru wengine inaweza kufichwa na udanganyifu, lakini uovu wake utafichuliwa kwenye kusanyiko.
27 Whoever digs a pit will fall into it, and a stone rolls back on the one who rolls it. Mtu akichimba shimo, atatumbukia ndani yake; mtu akivingirisha jiwe, litamrudia.
28 A lying tongue hates those it crushes, and a flattering mouth works ruin. Ulimi wa uongo huwachukia wale unaowaumiza, nacho kinywa cha kujipendekeza husababisha uharibifu.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]