Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Proverbs 27 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 Do not boast about tomorrow, for you do not know what a day may bring. Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa kuwa hujui ni nini kitakachozaliwa kwa siku moja.
2 Let someone else praise you, and not your own mouth; a stranger, and not your own lips. Mwache mwingine akusifu, wala si kinywa chako mwenyewe; mtu mwingine afanye hivyo na si midomo yako mwenyewe.
3 A stone is heavy and the sand a burden, but a fool's provocation is heavier than both. Jiwe ni zito na mchanga ni mzigo, lakini kukasirishwa na mpumbavu ni kuzito kuliko vyote viwili.
4 Wrath is cruel and anger is overwhelming, but who can stand before jealousy? Hasira ni ukatili na ghadhabu kali ni gharika, lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu?
5 Open rebuke is better than love that stays hidden. Afadhali karipio la wazi kuliko upendo uliofichika.
6 A friend's wounds are faithful, but an enemy's kisses are deceitful. Majeraha kutoka kwa rafiki yaonesha uaminifu, lakini adui huzidisha busu.
7 A well-fed person tramples honeycomb, but to the hungry even what is bitter tastes sweet. Yeye aliyeshiba huchukia kabisa asali, bali kwa mwenye njaa hata kile kilicho kichungu kwake ni kitamu.
8 A man who strays from his home is like a bird that strays from its nest. Kama ndege atangatangavyo mbali na kiota chake, ndivyo alivyo mtu atangatangaye mbali na nyumbani mwake.
9 Oil and incense gladden the heart, and the sweetness of a friend comes from heartfelt counsel. Manukato na uvumba huleta furaha moyoni, nao uzuri wa rafiki huchipuka katika ushauri wake wa uaminifu.
10 Do not forsake your friend or your father's friend, and do not go to your brother's house when disaster strikes; better a neighbor nearby than a brother far off. Usimwache rafiki yako wala rafiki wa baba yako, tena usiende nyumbani mwa ndugu yako wakati umepatwa na maafa. Bora jirani wa karibu kuliko ndugu aliye mbali.
11 Be wise, my son, and make my heart glad, so that I can answer anyone who taunts me. Mwanangu, uwe na hekima, nawe ulete furaha moyoni mwangu, ndipo nitakapoweza kumjibu yeyote anitendaye kwa dharau.
12 The prudent sees danger and takes cover, but the simple keep going and pay the price. Mtu mwenye busara huona hatari na kujificha, bali mjinga huendelea mbele, naye hupata madhara.
13 Take the garment of one who puts up security for a stranger; hold it as collateral when he does so for a foreign woman. Chukua vazi la yule awekaye dhamana kwa ajili ya mgeni; lishikilie liwe dhamana kwa ajili ya mgeni.
14 Whoever blesses his neighbor with a loud voice early in the morning, it will be taken as a curse. Mtu akimbariki jirani yake kwa sauti kuu asubuhi na mapema, itahesabiwa kuwa ni laana.
15 A quarrelsome wife is like a constant dripping on a rainy day. Mke mgomvi ni kama matone yasiyokoma siku ya mvua.
16 Restraining her is like restraining the wind, or grasping oil with the right hand. Kumzuia ni kama kuuzuia upepo, au kukamata mafuta kwa kiganja cha mkono.
17 Iron sharpens iron, and one person sharpens another. Kama vile chuma kinoavyo chuma, ndivyo mtu amnoavyo mwenzake.
18 Whoever tends a fig tree will eat its fruit, and whoever guards his master will be honored. Yeye autunzaye mtini atakula tunda lake, naye amtunzaye bwana wake ataheshimiwa.
19 As water reflects the face, so the heart reflects the person. Kama uso uonekanavyo kwenye maji, ndivyo hivyo moyo wa mtu humwonesha alivyo.
20 The grave and Destruction are never satisfied, and a person's eyes are never satisfied. Kuzimu na Uharibifu havishibi, wala macho ya mwanadamu hayashibi.
21 The crucible is for silver and the furnace for gold, and a person is tested by the praise he receives. Kalibu husafisha fedha na tanuru husafisha dhahabu, bali mtu hupimwa kwa sifa anazopewa na watu.
22 Though you grind a fool in a mortar with a pestle, along with the grain, his foolishness will not leave him. Hata ukimtwanga mpumbavu kwenye kinu, ukimtwanga kama nafaka kwa mchi, hutauondoa upumbavu wake.
23 Know well the condition of your flocks, and give careful attention to your herds. Hakikisha kuwa unajua hali ya makundi yako ya kondoo na mbuzi; angalia ng’ombe wako kwa makini.
24 For riches do not last forever, nor does a crown endure to every generation. Kwa kuwa utajiri haudumu milele, nalo taji halidumu vizazi vyote.
25 When the grass is gone and the new growth appears and the mountain herbs are gathered, Wakati majani makavu yameondolewa na mapya yamechipua, nayo majani toka milimani yamekusanywa,
26 the lambs will provide your clothing, and the goats will provide the price of a field; wana-kondoo watakupatia mavazi na mbuzi thamani ya shamba.
27 and there will be enough goats' milk for your food, for the food of your household and to sustain your servant girls. Utakuwa na maziwa mengi ya mbuzi kukulisha wewe na jamaa yako, na kuwalisha wajakazi wako.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]