Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Proverbs 24 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 Do not envy evil men, and do not desire to be with them, Usiwaonee wivu watu waovu, usitamani ushirika nao;
2 for their hearts plot violence, and their lips speak of trouble. kwa maana mioyo yao hupanga mambo ya jeuri, nayo midomo yao husema kuhusu kuleta madhara.
3 By wisdom a house is built, and by understanding it is established; Kwa hekima nyumba hujengwa, nayo kupitia ufahamu huimarishwa;
4 and by knowledge its rooms are filled with all precious and pleasant riches. kwa maarifa vyumba vyake hujazwa vitu vya thamani na vya kupendeza.
5 A wise man is full of strength, and a man of knowledge increases his power, Mtu mwenye hekima ana uwezo mkubwa, naye mtu mwenye maarifa huongeza nguvu,
6 for by wise guidance you can wage your war, and victory comes through many counselors. kwa kufanya vita unahitaji uongozi na kwa ushindi washauri wengi.
7 Wisdom is too high for a fool; at the gate, he has nothing to say. Hekima i juu mno kwa mpumbavu, katika kusanyiko langoni hana lolote la kusema.
8 Whoever plans to do evil will be called a schemer. Yeye apangaye mabaya atajulikana kama mtu wa hila.
9 A fool's scheming is sin, and the scoffer is detestable to people. Mipango ya upumbavu ni dhambi, watu huchukizwa na mwenye dhihaka.
10 If you falter in a time of trouble, your strength is small. Ukikata tamaa wakati wa taabu, jinsi gani nguvu zako ni kidogo!
11 Rescue those being taken away to death, and hold back those stumbling toward the slaughter. Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo; wazuie wote wanaojikokota kuelekea machinjoni.
12 If you say, "Look, we did not know this," does not he who weighs the heart perceive it? Does not he who watches over your soul know it? And will he not repay each person according to his deeds? Mkisema, “Lakini hatukujua lolote kuhusu hili,” je, yule apimaye mioyo halitambui hili? Je, yule awalindaye maisha yenu halijui hili? Je, hatamlipa kila mtu kulingana na aliyotenda?
13 My son, eat honey, for it is good, and the honeycomb's drippings are sweet to your taste. Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri; asali kutoka sega ni tamu kwa kuonja.
14 Know that wisdom is just like this to your soul; if you find it, there is a future, and your hope will not be cut off. Ujue pia kwamba hekima ni tamu kwa nafsi yako: Ukiipata, kuna matumaini kwako ya siku zijazo, nalo tumaini lako halitakatiliwa mbali.
15 Do not lie in wait, you wicked man, against the home of the righteous; do not destroy his resting place, Usivizie kama haramia afanyavyo ili kuyashambulia makao ya mwenye haki, wala usiyavamie makazi yake,
16 for though the righteous falls seven times, he rises again, but the wicked stumble in disaster. kwa maana ingawa mtu mwenye haki huanguka mara saba, huinuka tena; lakini waovu huangushwa chini na maafa.
17 Do not rejoice when your enemy falls, and do not let your heart be glad when he stumbles, Usitazame kwa kufurahia adui yako aangukapo; wakati anapojikwaa, usiruhusu moyo wako ushangilie.
18 lest our Father see it and be displeased, and turn his anger away from him. Mwenyezi Mungu asije akaona na kuchukia akaiondoa ghadhabu yake mbali naye.
19 Do not fret because of evildoers, and do not envy the wicked, Usikasirike kwa sababu ya wapotovu, wala usiwaonee wivu waovu,
20 for the evil man has no future; the lamp of the wicked will be snuffed out. kwa maana mpotovu hana tumaini la siku zijazo, nayo taa ya waovu itazimwa.
21 My son, fear our Father and the king, and do not join with those who rebel against them, Mwanangu, mche Mwenyezi Mungu na mfalme, wala usijiunge na waasi,
22 for their disaster will rise suddenly, and who knows the ruin that both of them can bring? kwa maana hao wawili watatuma maangamizi ya ghafula juu yao, naye ni nani ajuaye maafa wawezayo kuleta?
23 These also are sayings of the wise: Showing partiality in judgment is not good. Hii pia ni misemo ya wenye hekima: Kuonesha upendeleo katika hukumu si vyema:
24 Whoever says to the guilty, "You are innocent," peoples will curse him and nations will denounce him, Yeyote amwambiaye mwenye hatia, “Wewe huna hatia,” makabila ya watu watamlaani, na mataifa watamkana.
25 but it will go well for those who convict the guilty, and a rich blessing will come upon them. Bali itakuwa vyema kwa wale watakaowatia hatiani wenye hatia, nazo baraka tele zitawajilia juu yao.
26 An honest answer is like a kiss on the lips. Jawabu la uaminifu ni kama busu la mdomoni.
27 Prepare your work outside, get your fields ready, and after that build your house. Maliza kazi zako za nje, nawe uweke mashamba yako tayari, baada ya hayo, jenga nyumba yako.
28 Do not be a witness against your neighbor without cause; would you deceive with your lips? Usishuhudie dhidi ya jirani yako bila sababu, au kutumia midomo yako kudanganya.
29 Do not say, "I will do to him as he did to me; I will pay the man back for what he has done." Usiseme, “Nitamtenda kama alivyonitenda mimi; nitamlipiza mtu yule kwa kile alichonitendea.”
30 I passed by the field of a lazy man, by the vineyard of someone lacking sense, Nilipita karibu na shamba la mvivu, karibu na shamba la mizabibu la mtu asiye na akili,
31 and there it was, all overgrown with thorns; the ground was covered with weeds, and its stone wall was broken down. miiba ilikuwa imeota kila mahali, ardhi ilikuwa imefunikwa na magugu, na ukuta wa mawe ulikuwa umebomoka.
32 Then I looked and took it to heart; I saw and received instruction. Nikatafakari moyoni mwangu lile nililoliona, nami nikajifunza somo kutokana na niliyoyaona:
33 A little sleep, a little slumber, a little folding of the hands to rest, Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo, bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:
34 and poverty will come upon you like a robber, and scarcity like an armed man. na umaskini utakuja juu yako kama mnyang’anyi, na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]