Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Mark 4 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 Jesus again taught by the sea. So large a crowd gathered around him that he got into a boat on the water and sat, while the whole crowd was on land by the sea. Isa akaanza kufundisha tena kando ya bahari. Palikuwa na umati mkubwa wa watu waliokuwa wamekusanyika kumzunguka, hata ikambidi Isa aingie kwenye mashua iliyokuwa baharini na kuketi humo, nao watu wote walikuwa ufuoni mwa bahari.
2 He taught them many things in parables, and in his teaching he said to them: Akawafundisha mambo mengi kwa mifano, naye katika mafundisho yake akasema:
3 "Listen! A sower went out to sow. “Sikilizeni! Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu
4 And as he sowed, some seed fell along the path, and the birds came and devoured it. Alipokuwa akitawanya mbegu, nyingine zilianguka kando ya njia, nao ndege wakaja na kuzila.
5 Other seed fell on rocky ground, lacking much soil, and sprang up at once since the soil had no depth. Nyingine zilianguka kwenye mwamba usio na udongo mwingi. Ziliota haraka kwa kuwa udongo ulikuwa kidogo.
6 When the sun rose, the plants were scorched, and since they had no root, they withered. Lakini jua lilipozidi, mimea ikanyauka na kukauka kwa kuwa mizizi yake haikuwa na kina.
7 Other seed fell among thorns, and the thorns grew up and choked it, yielding no grain. Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba, nayo miiba ikakua, ikaisonga hiyo mimea, hivyo haikutoa mazao.
8 Other seed fell into good soil, producing grain that sprouted, grew, and yielded thirty, sixty, one hundred times what was sown." Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri, zikaota vizuri na kukua, zikatoa mazao, moja mara thelathini, nyingine mara sitini, na nyingine mara mia moja.”
9 And he said, "Whoever has ears to hear, let him hear." Kisha Isa akasema, “Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.”
10 When he was alone, those around him, together with the Twelve, asked him about the parables. Alipokuwa peke yake, watu waliokuwa naye pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili wakamuuliza kuhusu mifano yake.
11 He said to them, "To you is given the secret of the kingdom of our Father, but to those outside, everything comes in parables, Naye akawaambia, “Ninyi mmepewa siri ya ufalme wa Mungu. Lakini kwa wale walio nje, kila kitu husemwa kwa mifano,
12 so that 'they may look but not perceive, and hear but not understand, and not turn and be forgiven.'" ili, “ ‘kuona waone lakini wasitambue, na kusikia wasikie lakini wasielewe; wasije wakageuka na kusamehewa!’ ”
13 He said to them, "You don't understand this parable? Then how will you understand all the parables? Kisha Isa akawauliza, “Hamwelewi maana ya mfano huu? Basi mtaelewaje mifano mingine?
14 The sower sows the word. Yule mpanzi hupanda neno.
15 These are the ones on the path where the word is sown: once they hear, Satan comes immediately and takes away the word sown in them. Hawa ndio wale walio kando ya njia ambako neno lilipandwa. Walisikiapo neno, mara Shetani huja na kulinyakua lile neno lililopandwa ndani yao.
16 These are the ones sown on rocky ground, who hear the word and immediately receive it with joy. Nazo zile mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye miamba, ni wale wanaolisikia neno, na mara hulipokea kwa furaha.
17 But they have no root in themselves, lasting only briefly; when trouble or persecution comes because of the word, they fall away at once. Lakini kwa kuwa hawana mizizi, wao hudumu kwa muda mfupi tu. Kisha dhiki au mateso yanapoinuka kwa ajili ya lile neno, mara wao huiacha imani.
18 And others are the ones sown among thorns. These are those who hear the word, Lakini wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye miiba, hulisikia lile neno;
19 but worries of this age, the deceit of wealth, and desires for other things enter and choke the word, and it produces no fruit. lakini masumbufu ya maisha haya, na udanganyifu wa mali na tamaa ya mambo mengine huja na kulisonga lile neno na kulifanya lisizae.
20 And these are the ones sown on good soil: they hear the word, accept it, and produce fruit—thirty, sixty, one hundred times over." Wengine, kama mbegu iliyopandwa kwenye udongo mzuri, hulisikia lile neno, wakalipokea na kuzaa mazao. Wao huzaa mara thelathini, au mara sitini, au mara mia ya mbegu iliyopandwa.”
21 He told them, "Does anyone bring in a lamp to put it under a basket or bed—not on a stand? Akawaambia, “Je, taa huwashwa na kufunikwa chini ya kikapu au mvunguni mwa kitanda? Je, haiwashwi na kuwekwa juu ya kinara chake?
22 Nothing is hidden except to be revealed; nothing is secret except to surface. Kwa kuwa hakuna kilichofichika ambacho hakitafunuliwa, wala hakuna jambo lolote la siri ambalo halitaletwa nuruni.
23 If anyone has ears to hear, let him hear." Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.”
24 He told them, "Watch what you hear. The measure you use will be measured to you—and more added. Naye akawaambia, “Kuweni waangalifu na yale mnayosikia. Kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa ninyi, hata na zaidi.
25 For whoever has will be given more; whoever doesn't, even what he has will be taken from him." Kwa maana kila mtu aliye na kitu atapewa zaidi, naye atakuwa navyo tele. Lakini yule asiye na kitu, hata kile alicho nacho atanyang’anywa.”
26 He said, "This is what the kingdom of our Father is like: a man scatters seed on the ground. Pia akawaambia, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani.
27 Night and day, asleep or awake, the seed sprouts and grows, though he doesn't know how. Baada yake kuzipanda, usiku na mchana, akiwa amelala au ameamka, mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua ikuavyo.
28 The soil yields grain on its own—first blade, then head, then full kernel in the head. Udongo huifanya iote kuwa mche, halafu suke, kisha nafaka kamili kwenye suke.
29 But when the grain ripens, he immediately sends the sickle, since harvest has come." Mara nafaka inapokuwa imekomaa, mkulima huenda shambani na mundu kuvuna, maana mavuno yamekuwa tayari.”
30 He said, "What can we compare the kingdom of our Father to, or what parable can we use for it? Akawaambia tena, “Tuufananishe ufalme wa Mungu na nini? Au tutumie mfano gani ili kuueleza?
31 It's like a mustard seed, the smallest of all seeds when sown on the ground. Ni kama punje ya haradali, ambayo ni mbegu ndogo sana kuliko mbegu zote zinazopandwa ardhini.
32 Yet once sown, it grows up and becomes the largest of all garden plants, producing branches so big that birds of the air can nest in its shade." Lakini ikipandwa, hukua ikawa mmea mkubwa kuliko yote katika bustani, ikawa na matawi makubwa hata ndege wa angani wanaweza kujenga viota kwenye kivuli chake.”
33 With many such parables he spoke the word to them, as they were able to hear. Kwa mifano mingine mingi kama hii Isa alinena nao neno lake, kwa kadiri walivyoweza kulielewa.
34 He spoke to them only in parables, but privately explained everything to his own disciples. Hakusema nao neno lolote pasipo mfano. Lakini alipokuwa na wanafunzi wake, aliwafafanulia kila kitu.
35 That day, when evening came, he said to them, "Let us cross over to the other side." Ilipokaribia jioni ya siku hiyo, Isa akawaambia wanafunzi wake, “Tuvukeni hadi ng’ambo ya ziwa.”
36 They left the crowd and took him along, just as he was, in the boat, other boats accompanying him. Wakaacha umati wa watu, na wakamchukua vile alivyokuwa kwenye mashua. Palikuwa pia na mashua zingine nyingi pamoja naye.
37 A fierce windstorm came up. Waves broke over the boat, so that it was already being swamped. Kukawa na dhoruba kali, nayo mawimbi yakaipiga ile mashua hata ikawa karibu kujaa maji.
38 But Jesus was asleep in the stern on the cushion. They woke him and said, "Teacher, don't you care that we're dying?" Isa alikuwa katika shetri, akiwa analala juu ya mto. Wanafunzi wake wakamwamsha, wakamwambia, “Mwalimu, hujali kama tunazama?”
39 He got up, rebuked the wind, and told the sea, "Peace! Be still!" The wind stopped, and it grew totally calm. Akaamka, akaukemea ule upepo, akayaambia yale mawimbi, “Uwe kimya! Tulia!” Ule upepo ukatulia, kukawa shwari kabisa.
40 He said to them, "Why are you so afraid? Do you still have no faith?" Isa akawaambia wanafunzi wake, “Kwa nini mnaogopa hivyo? Je, bado hamna imani?”
41 They were terrified and asked one another, "Who then is this, that even the wind and the sea obey him?" Nao wakawa wameogopa sana, wakaulizana, “Ni nani huyu? Hata upepo na mawimbi vinamtii!”
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]