Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Mark 3 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 Once again Jesus entered the synagogue, and a man with a withered hand was there. Isa akaingia tena ndani ya sinagogi, na kulikuwa na mtu aliyepooza mkono.
2 They watched closely to see if he'd heal the man on the Sabbath, to accuse Jesus. Wakawa wanamwangalia waone kama atamponya huyo mtu siku ya Sabato, ili wapate sababu ya kumshtaki.
3 Jesus said to the man with the withered hand, "Stand up and come forward." Isa akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Njoo hapa mbele ya watu wote.”
4 Then he asked them, "Is it lawful on the Sabbath to do good or to do harm, to save life or to kill?" But they stayed silent. Kisha Isa akawauliza, “Je, ni lipi lililo halali siku ya Sabato: Ni kutenda mema au kutenda mabaya? Ni kuokoa maisha au kuua?” Lakini wao wakanyamaza.
5 He looked around at them in anger, grieved by their hardness of heart, and told the man, "Stretch out your hand." He stretched it out, and his hand was restored. Isa akawatazama kwa hasira watu waliomzunguka pande zote, akahuzunika sana kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao. Akamwambia yule mtu mwenye mkono uliopooza, “Nyoosha mkono wako.” Akaunyoosha, nao ukawa umeponywa kabisa!
6 Then the Pharisees went out and immediately began plotting with the Herodians how they might destroy him. Kisha Mafarisayo wakatoka nje, nao wakaanza kufanya njama ya kumuua Isa wakishirikiana na Maherode.
7 Jesus withdrew with his disciples to the sea; a large crowd from Galilee followed, and from Judea, Isa na wanafunzi wake wakaondoka huko, wakaenda baharini, nao umati mkubwa wa watu kutoka Galilaya wakamfuata.
8 from Jerusalem, Idumea, beyond the Jordan, and the region around Tyre and Sidon—hearing all he was doing, a great crowd came to him. Waliposikia mambo yote aliyokuwa akiyafanya, makundi ya watu wakamjia kutoka Yudea, Yerusalemu, Idumaya, na ng’ambo ya Yordani, pamoja na wale wa maeneo ya Tiro na Sidoni.
9 He told his disciples to keep a small boat ready, because of the crowd, so they wouldn't crush him. Kwa sababu ya umati mkubwa wa watu, aliwaambia wanafunzi wake watayarishe mashua ndogo kwa ajili yake, ili kuwazuia watu kumsonga.
10 For he had healed so many that all who had diseases were pressing forward to touch him. Kwa kuwa alikuwa amewaponya wagonjwa wengi, wale wenye magonjwa walikuwa wanasukumana ili wapate kumgusa.
11 Whenever the unclean spirits saw him, they fell before him, shouting, "You are the Son of God!" Kila mara pepo wachafu walipomwona, walianguka chini mbele yake na kupiga kelele wakisema, “Wewe ndiwe Mwana wa Mungu.”
12 But he firmly warned them not to reveal him. Lakini aliwaonya wasiwaambie wengine kumhusu.
13 Jesus went up the mountain and called those he wanted; they came to him. Isa akapanda mlimani na kuwaita wale aliowataka, nao wakamjia.
14 He appointed twelve, named apostles, so they could be with him and he could send them out to preach, Akawachagua watu kumi na wawili ambao aliwaita mitume, ili wapate kuwa naye, na awatume kwenda kuhubiri
15 and to have authority to drive out demons. na kuwa na mamlaka ya kutoa pepo wachafu.
16 These are the twelve he appointed: Simon, to whom he gave the name Peter; Hawa ndio wale kumi na wawili aliowachagua: Simoni (ambaye alimwita Petro);
17 James son of Zebedee, and John his brother, whom he named Boanerges, meaning Sons of Thunder; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye (ambao aliwaita Boanerge, maana yake Wana wa Ngurumo);
18 Andrew, Philip, Bartholomew, Matthew, Thomas, James son of Alphaeus, Thaddaeus, Simon the Zealot, Andrea, Filipo, Bartholomayo, Mathayo, Tomaso, Yakobo mwana wa Alfayo, Thadayo, Simoni Mkananayo,
19 and Judas Iscariot, who betrayed him. na Yuda Iskariote aliyemsaliti Isa.
20 He went home; the crowd gathered again, so he and his disciples couldn't even eat. Kisha Isa alipoingia ndani ya nyumba, umati wa watu wakakusanyika tena, kiasi kwamba yeye na wanafunzi wake hawakuweza kula chakula.
21 When his family heard, they went out to restrain him, for they said, "He's out of his mind." Ndugu zake walipopata habari wakaja ili kumchukua kwa maana watu walikuwa wakisema, “Amerukwa na akili.”
22 The scribes who came down from Jerusalem said, "He has Beelzebul," and, "By the prince of demons he drives out demons." Walimu wa Torati walioteremka kutoka Yerusalemu walisema, “Amepagawa na Beelzebuli! Anatoa pepo wachafu kwa nguvu ya mkuu wa pepo wachafu!”
23 So Jesus called them to him and spoke in parables: "How can Satan drive out Satan? Basi Isa akawaita na kuzungumza nao kwa mifano akasema: “Shetani awezaje kumtoa Shetani?
24 If a kingdom is divided against itself, that kingdom cannot stand. Kama ufalme ukigawanyika dhidi yake wenyewe, ufalme huo hauwezi kusimama.
25 And if a house is divided against itself, that house will not be able to stand. Nayo nyumba ikigawanyika dhidi yake yenyewe, nyumba hiyo haiwezi kusimama.
26 And if Satan opposes himself and is divided, he cannot stand; his end has come. Na kama Shetani akijipinga mwenyewe na awe amegawanyika, hawezi kusimama, bali mwisho wake umetimia.
27 No one can enter a strong man's house and take his goods without first tying up the strong man—then he can plunder the house. Hakuna mtu yeyote awezaye kuingia kwenye nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali yake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu. Ndipo ataweza kuteka nyara mali yake.
28 Truly I tell you, all sins and insults against God will be forgiven children of mankind, whatever they say, Amin, nawaambia, watu wataweza kusamehewa dhambi na kufuru zao zote;
29 but whoever blasphemes against the Holy Spirit never has forgiveness; they are guilty of an eternal sin," lakini yeyote anayemkufuru Roho Mtakatifu wa Mungu hatasamehewa kamwe, atakuwa na hatia ya dhambi ya milele.”
30 for they were saying, "He has an unclean spirit." Isa alisema hivi kwa sababu walikuwa wanasema, “Ana pepo mchafu.”
31 His mother and brothers arrived and, standing outside, sent to him, calling him. Kisha wakaja ndugu zake Isa pamoja na mama yake. Wakiwa wamesimama nje, wakamtuma mtu kumwita.
32 A crowd sat around him and said to him, "Look, your mother and your brothers are outside, asking for you." Umati wa watu walikuwa wameketi kumzunguka, nao wakamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje, wanakutafuta.”
33 He answered them, "Who are my mother and my brothers?" Akawauliza, “Mama yangu na ndugu zangu ni nani?”
34 Looking around at those sitting in a circle around him, he said, "Here are my mother and my brothers! Kisha akawatazama wale watu waliokuwa wameketi kumzunguka pande zote, akasema, “Hawa ndio mama yangu na ndugu zangu.
35 Whoever does the will of our Father is my brother and sister and mother." Mtu yeyote anayetenda mapenzi ya Mungu, huyo ndiye kaka yangu, na dada yangu, na mama yangu.”
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]