Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Mark 5 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 They came to the other side of the sea, to the region of the Gerasenes. Isa na wanafunzi wake wakafika upande wa pili wa ziwa, wakaingia katika nchi ya Wagerasi.
2 As Jesus left the boat, a man with an unclean spirit met him at once, from the tombs. Isa alipotoka kwenye mashua, mara mtu mmoja mwenye pepo mchafu akatoka makaburini, akakutana naye.
3 He lived among the tombs, and no one could bind him anymore, not even with a chain. Mtu huyu aliishi makaburini, wala hakuna aliyeweza kumzuia hata kwa kumfunga minyororo.
4 For he'd often been bound with shackles and chains, but tore the chains apart and shattered the shackles—no one had strength to subdue him. Kwa kuwa mara kwa mara alikuwa amefungwa minyororo mikononi na miguuni, lakini akaikata hiyo minyororo na kuzivunja zile pingu miguuni mwake. Hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa na nguvu za kumzuia.
5 Night and day, among the tombs and on the mountains, he cried out constantly, cutting himself with stones. Usiku na mchana alikuwa makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikatakata kwa mawe.
6 And when he saw Jesus from a distance, he ran and fell down before him. Alipomwona Isa kwa mbali, alimkimbilia, akapiga magoti mbele yake.
7 Shouting loudly, he said, "What do you want with me, Jesus, Son of the Most High God? I beg you by God, don't torment me!" Akapaza sauti kwa nguvu akisema, “Una nini nami, Isa, Mwana wa Mungu Aliye Juu Sana? Ninakusihi kwa jina la Mungu, usinitese!”
8 For Jesus had been saying to him, "Come out of the man, you unclean spirit!" Kwa kuwa Isa alikuwa amemwambia, “Mtoke mtu huyu, wewe pepo mchafu!”
9 Jesus asked, "What is your name?" "Legion," he said, "we are many." Isa akamuuliza, “Jina lako ni nani?” Akamjibu, “Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tuko wengi.”
10 He kept begging him not to send them out of the region. Akamsihi Isa sana asiwapeleke nje ya nchi ile.
11 Now a great herd of pigs was feeding there on the hillside. Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe lililokuwa likilisha karibu kando ya kilima.
12 And they begged him, "Send us to the pigs; let us enter them." Wale pepo wachafu wakamsihi Isa wakisema, “Tuamuru twende kwenye wale nguruwe. Turuhusu tuwaingie.”
13 He gave permission. The unclean spirits came out and entered the pigs; the herd—about 2,000—rushed down the cliff into the sea and drowned in the sea. Basi Isa akawaruhusu, nao wale pepo wachafu wakatoka, wakawaingia hao nguruwe. Lile kundi lilikuwa na nguruwe wapatao elfu mbili, nao wote wakateremkia gengeni kwa kasi, nao wakatumbukia ziwani na kuzama.
14 The herders fled and told it in town and country; people came to see what happened. Wale watu waliokuwa wakichunga hao nguruwe wakakimbilia mjini na vijijini kueleza yaliyotukia. Watu wakaenda kuona hayo yaliyokuwa yametukia.
15 They came to Jesus and saw the man who had been possessed by the demons, the one who'd had the legion, sitting there, dressed and thinking clearly—and they were afraid. Walipofika kwa Isa, wakamwona yule mtu aliyekuwa amepagawa na legioni ya pepo wachafu akiwa ameketi hapo, amevaa nguo na mwenye akili timamu. Wakaogopa.
16 Eyewitnesses told them what had happened to the demon-possessed man, and about the pigs. Wale walioyaona mambo hayo wakawaeleza watu wengine yaliyomtokea yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo wachafu, na habari za lile kundi la nguruwe pia.
17 And they began to beg Jesus to leave their region. Basi watu wakaanza kumwomba Isa aondoke katika nchi yao.
18 As he was getting into the boat, the once-possessed man begged to be with him. Isa alipokuwa anaingia kwenye mashua, yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo wachafu akamsihi Isa waende pamoja.
19 But Jesus refused, telling him instead, "Go home to your own people and tell them how much our Father has done for you, and how he has had mercy on you." Isa hakumruhusu, bali alimwambia, “Nenda nyumbani kwa jamaa yako ukawaeleze mambo makuu aliyokutendea Mwenyezi Mungu, na jinsi alivyokuhurumia.”
20 He went and began proclaiming in the Decapolis all Jesus had done for him, and everyone was amazed. Yule mtu akaenda zake, akaanza kutangaza katika Dekapoli mambo makuu Isa aliyomtendea. Nao watu wote wakastaajabu.
21 When Jesus crossed again by boat to the other side, a large crowd gathered around him by the sea. Isa alipokwisha kuvuka tena na kufika ng’ambo, umati mkubwa wa watu wakamzunguka hapo kando ya bahari.
22 One of the synagogue leaders, named Jairus, came, saw Jesus, and fell at his feet, Kisha mmoja wa viongozi wa sinagogi aliyeitwa Yairo akafika pale. Naye alipomwona Isa, akapiga magoti miguuni pake,
23 and begged him urgently, "My little daughter is dying. Come, lay your hands on her, so she may be healed and live." akamsihi akisema, “Binti yangu mdogo ni mgonjwa mahututi. Tafadhali nakusihi, njoo uweke mikono yako juu yake ili apate kupona, naye ataishi.”
24 So Jesus went with him. And a great crowd followed him and pressed around him. Hivyo Isa akaenda pamoja naye. Umati mkubwa wa watu wakamfuata, nao watu wakawa wanamsonga.
25 And there was a woman with a discharge of blood that had gone on for twelve years. Hapo palikuwa na mwanamke aliyekuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa miaka kumi na mbili.
26 She had suffered much under many doctors, spent all she owned, gained nothing, and only grew worse. Mwanamke huyu alikuwa ameteseka sana kwa mikono ya matabibu wengi, na kutumia kila kitu alichokuwa nacho. Lakini badala ya kupona, hali yake ilizidi kuwa mbaya.
27 Hearing about Jesus, she came up behind him in the crowd and touched his cloak. Alikuwa amesikia habari za Isa, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake,
28 For she kept saying, "If I just touch his garments, I will be made well." kwa maana alisema moyoni mwake, “Nikiligusa vazi lake tu, nitaponywa.”
29 Her flow of blood dried up instantly, and she felt in her body that she was healed of her suffering. Mara kutoka damu kwake kukakoma, naye akajisikia mwilini mwake amepona kabisa.
30 At once Jesus, aware that power had left him, turned around in the crowd and asked, "Who touched my clothes?" Ghafula Isa akatambua kuwa nguvu zimemtoka. Akageukia umati wa watu na kuuliza, “Ni nani aliyegusa mavazi yangu?”
31 His disciples said to him, "You see the crowd crushing you, yet you ask, 'Who touched me?'" Wanafunzi wake wakamjibu, “Unaona jinsi watu wanavyokusonga. Wawezaje kuuliza, ‘Ni nani aliyenigusa?’ ”
32 And he looked around to see who had done it. Lakini Isa akaangalia pande zote ili aone ni nani aliyemgusa.
33 But the woman, afraid and trembling, knowing what had happened to her, came, fell before him, and told him the whole truth. Yule mwanamke, akijua kilichomtokea, akaja, akaanguka miguuni pake akitetemeka kwa hofu, akamweleza ukweli wote.
34 He told her, "Daughter, your faith made you well. Go in peace, healed of your suffering." Isa akamwambia, “Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani, upone kabisa ugonjwa wako.”
35 While he was still speaking, people came from the synagogue leader's house, saying, "Your daughter has died. Why bother the Teacher any longer?" Alipokuwa bado anaongea, watu wakafika kutoka nyumbani mwa Yairo. Wakamwambia, “Binti yako amekufa. Kwa nini kuendelea kumsumbua Mwalimu?”
36 But Jesus overheard what they said and told the synagogue leader, "Don't fear, only believe." Aliposikia hayo waliyosema, Isa akamwambia huyo kiongozi wa sinagogi, “Usiogope. Amini tu.”
37 And he allowed no one to follow him except Peter, James, and John the brother of James. Hakumruhusu mtu yeyote amfuate isipokuwa Petro, Yakobo na Yohana, nduguye Yakobo.
38 They came to the synagogue leader's house and Jesus saw chaos—people weeping, wailing loudly. Walipofika nyumbani mwa yule kiongozi wa sinagogi, Isa akaona ghasia, watu wakilia na kuomboleza kwa sauti kubwa.
39 Entering, he said to them, "Why this commotion and crying? The child isn't dead, just asleep." Alipokwisha kuingia ndani, akawaambia, “Kwa nini mnafanya ghasia na kulia? Mtoto hajafa, bali amelala tu.”
40 They laughed at him. But he sent them all out, took the child's father and mother and his companions, and entered where the child was. Wale watu wakamcheka. Baada ya kuwafukuza wote nje, Isa akaenda na baba na mama wa yule mtoto, pamoja na wale wanafunzi aliokuwa nao, wakaingia ndani hadi pale alipokuwa mtoto yule.
41 He took her hand and said to her, "Talitha koum," which means, "Little girl, I say to you, get up!" Akamshika mtoto mkono, akamwambia, “Talitha koum!” (maana yake, “Msichana, nakuambia: amka!”)
42 At once the girl got up and walked—for she was twelve—and they were instantly overwhelmed with great amazement. Mara yule msichana akasimama, akaanza kutembea (alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili). Walipoona haya, wakastaajabu sana.
43 He strictly ordered them to tell no one of this, and said to give her something to eat. Isa akawaagiza kwa ukali wasimweleze mtu yeyote jambo hilo, naye akawaambia wampe yule msichana chakula.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]