Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

John 9 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 As Jesus passed by, he saw a man who had been blind from birth. Isa alipokuwa akipita, akamwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa.
2 His disciples asked him, "Rabbi, who sinned, this man or his parents, that he was born blind?" Wanafunzi wake wakamuuliza, “Mwalimu, ni nani aliyetenda dhambi; ni huyu mtu au wazazi wake hata azaliwe kipofu?”
3 "Neither this man nor his parents sinned,' Jesus answered, 'but this happened so the works of our Father might be revealed in him. Isa akawajibu, “Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake.
4 We must do the works of the one who sent me while it is day; night comes, when no one can work. Yanipasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi.
5 As long as I am in the world, I am the light of the world.'" Wakati niko ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu.”
6 Saying this, he spat on the ground, made mud from the saliva, and smeared it on the man's eyes. Baada ya kusema haya, akatema mate ardhini, akatengeneza tope kwa mate na kumpaka yule kipofu machoni.
7 He told him, "Go, wash in the pool of Siloam" (meaning Sent). So the man went, washed, and returned able to see. Kisha akamwambia, “Nenda ukanawe katika Bwawa la Siloamu” (Siloamu maana yake ni Kutumwa). Ndipo yule kipofu akaenda, akanawa, naye akarudi akiwa anaona.
8 Neighbors and those who'd seen him begging before said, "Isn't this the one who used to sit and beg?" Majirani zake na wale wote waliokuwa wamemwona hapo awali akiombaomba wakaanza kuuliza, “Je, huyu si yule aliyekuwa akiketi akiombaomba?”
9 Some said, "That's him." Others said, "No, he just looks like him." He kept saying, "I'm the one." Wengine wakasema, “Ndiye.” Wengine wakasema, “Siye, bali anafanana naye.” Lakini yeye akawaambia, “Mimi ndiye.”
10 So they asked him, "Then how were your eyes opened?" Wakamuuliza, “Basi macho yako yalifumbuliwaje?”
11 He replied, "The man called Jesus made mud, smeared it on my eyes, and told me, 'Go to Siloam and wash.' So I went, washed, and could see." Yeye akawajibu, “Yule mtu aitwaye Isa alitengeneza tope, akanipaka machoni mwangu, naye akaniambia, ‘Nenda ukanawe katika Bwawa la Siloamu,’ ndipo nikanawa nami nikapata kuona!”
12 They said to him, "Where is he?" He said, "I do not know." Wale wakamuuliza, “Yeye huyo mtu yuko wapi?” Akawajibu, “Sijui.”
13 They brought the man who had been blind to the Pharisees. Wakamleta yule mtu aliyekuwa kipofu hapo awali kwa Mafarisayo.
14 Now it was a Sabbath day when Jesus made the mud and opened his eyes. Basi siku hiyo Isa alitengeneza tope na kuyafungua macho ya huyo mtu ilikuwa Sabato.
15 So the Pharisees also asked him again how he had gained sight. He told them, "He put mud on my eyes, and I washed, and I see." Mafarisayo nao wakaanza kumuuliza yule mtu alivyopata kuona. Naye akawaambia, “Alinipaka tope kwenye macho yangu, nikanawa na sasa ninaona.”
16 Some Pharisees said, "This man isn't from God—he doesn't keep the Sabbath." Others said, "How can a sinful man do such signs?" So they were divided among them. Baadhi ya Mafarisayo wakasema, “Huyu mtu hatoki kwa Mungu, kwa sababu hashiki Sabato.” Lakini wengine wakasema, “Awezaje mtu mwenye dhambi kufanya miujiza kama hii?” Wakagawanyika.
17 Again they asked the blind man, "What do you say about him, since he opened your eyes?" He said, "He is a prophet." Hivyo wakamwambia tena yule mtu aliyekuwa kipofu, “Wewe ndiwe uliyefumbuliwa macho. Wasemaje kuhusu mtu huyo?” Yeye akawajibu, “Yeye ni nabii.”
18 The Jews did not believe he had been blind and gained sight, until they summoned the parents of the man who had gained sight. Wale Wayahudi hawakuamini ya kuwa mtu huyo alikuwa kipofu akapata kuona, hadi walipowaita wazazi wake.
19 They asked them, "Is this your son you say was born blind? How then does he now see?" Wakawauliza, “Je, huyu ni mtoto wenu, ambaye mnasema alizaliwa kipofu? Imekuwaje basi sasa anaona?”
20 His parents answered, "We know that this is our son and that he was born blind. Wazazi wake wakajibu, “Tunajua ya kuwa huyu ni mtoto wetu na ya kuwa alizaliwa kipofu.
21 But how he now sees, we don't know; or who opened his eyes, we don't know. Ask him—he's an adult; he'll speak for himself." Lakini hatujui jinsi anavyoweza kuona sasa, wala hatujui ni nani aliyemfungua macho yake. Muulizeni; yeye ni mtu mzima na anaweza kujieleza mwenyewe.”
22 His parents said this, fearing the Jews, since the Jews had already agreed that if anyone confessed Jesus as the Christ, he would be expelled from the synagogue. Wazazi wake walisema hivi kwa sababu waliwaogopa viongozi wa Wayahudi, kwani walikuwa wamekubaliana kuwa mtu yeyote atakayemkiri Isa kuwa ndiye Al-Masihi atafukuzwa kutoka sinagogi.
23 That was why his parents said, "He is of age; ask him." Kwa hiyo wazazi wake wakasema, “Yeye ni mtu mzima. Muulizeni.”
24 So they called the once-blind man again and said, "Give God the glory. We know this man is a sinner." Hivyo kwa mara ya pili wakamwita yule aliyekuwa kipofu, nao wakamwambia, “Mpe Mungu utukufu! Sisi tunafahamu kuwa mtu huyu aliyekuponya ni mwenye dhambi.”
25 He replied, "Whether he's a sinner, I don't know. I know one thing: I was blind, now I see." Akawajibu, “Mimi sijui kama yeye ni mwenye dhambi. Lakini jambo moja ninalojua, nilikuwa kipofu na sasa ninaona.”
26 They said to him, "What did he do to you? How did he open your eyes?" Wakamuuliza, “Alikufanyia nini? Aliyafumbuaje macho yako?”
27 He answered them, "I already told you, and you didn't listen. Why do you want to hear it again? Do you also want to become his disciples?" Akawajibu, “Tayari nimekwisha kuwaambia, nanyi hamtaki kunisikiliza. Mbona mnataka kusikia tena? Je, ninyi nanyi mnataka kuwa wanafunzi wake?”
28 And they reviled him, saying, "You are his disciple, but we are disciples of Moses. Ndipo wakamtukana na kusema, “Wewe ndiwe mwanafunzi wake! Sisi ni wanafunzi wa Musa.
29 We know God spoke to Moses, but we don't know where this man is from." Tunajua kwamba Mungu alisema na Musa, lakini mtu huyu hatujui anakotoka.”
30 The man answered them, "Here's the amazing thing: you don't know where he's from, yet he opened my eyes. Yule mtu akawajibu, “Hili ni jambo la ajabu! Hamjui anakotoka, naye amenifungua macho yangu!
31 We know God doesn't listen to sinners, but if anyone reveres God and does his will, God listens to him. Tunajua ya kuwa Mungu hawasikilizi wenye dhambi, lakini huwasikiliza wote wanaomcha na kumtii.
32 Never since the world began has anyone heard of someone opening the eyes of a person born blind. Tangu zamani hatujasikia kwamba mtu amemponya yeyote aliyezaliwa kipofu.
33 If this man were not from God, he could do nothing." Kama huyu mtu hakutoka kwa Mungu, asingeweza kufanya lolote.”
34 They answered him, "You were born entirely in sin, yet you teach us?" and threw him out. Wakamjibu, “Wewe ulizaliwa katika dhambi kabisa, nawe unajaribu kutufundisha?” Wakamfukuza atoke nje.
35 Jesus heard they had thrown him out, and finding him, said, "Do you believe in the Son of Man?" Isa aliposikia kuwa wamemfukuza atoke nje yule mtu aliyemfumbua macho, alimkuta, akamuuliza, “Je, unamwamini Mwana wa Adamu?”
36 He answered, "And who is he, sir, so I can believe in him?" Yule mtu akamjibu, “Yeye ni nani, Bwana? Niambie ili nipate kumwamini.”
37 Jesus said to him, "You have seen him, and it is he who is speaking with you." Isa akamjibu, “Umekwisha kumwona; naye anayezungumza nawe, ndiye.”
38 He said, "Lord, I believe," and he worshiped him. Yule mtu akasema, “Bwana, naamini.” Naye akamwabudu.
39 Jesus said, "I came into this world for judgment, so those who don't see may see, and those who see may become blind." Isa akasema, “Nimekuja ulimwenguni humu kwa ajili ya kuhukumu, ili wale walio vipofu wapate kuona, nao wale wanaoona wawe vipofu.”
40 Some Pharisees with him heard this and said, "Are we blind too?" Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa karibu naye wakamsikia na kumwambia, “Je, kweli sisi ni vipofu?”
41 Jesus told them, "If you were blind, you would have no sin; but since you say, 'We see,' your sin remains." Isa akawajibu, “Kama mngekuwa vipofu kweli, msingekuwa na hatia ya dhambi, lakini kwa kuwa mnasema, ‘Tunaona,’ basi mna hatia.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]