Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

John 8 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 But Jesus went to the Mount of Olives. Lakini Isa akaenda katika Mlima wa Mizeituni.
2 At dawn he came again to the temple; all the people came to him, and he sat down and taught them. Alfajiri na mapema Isa akaja tena Hekaluni; watu wote wakakusanyika, naye akaketi, akaanza kuwafundisha.
3 The scribes and Pharisees brought a woman caught in adultery and stood her in the middle. Walimu wa Torati na Mafarisayo wakamleta mwanamke mmoja aliyefumaniwa akizini. Wakamsimamisha katikati ya umati wa watu wote.
4 They said to him, "Teacher, this woman was caught in the act of adultery. Wakamwambia Isa, “Mwalimu, huyu mwanamke amekutwa akizini.
5 Now in the Law, Moses commanded us to stone such women. So what do you say? Katika sheria, Musa alituamuru kuwapiga kwa mawe wanawake wa namna hii, hadi wafe. Sasa wewe wasemaje?”
6 They said this to test him, seeking grounds to accuse him. But Jesus bent down and wrote on the ground with his finger." Walimuuliza swali hili kama mtego ili wapate sababu ya kumshtaki. Lakini Isa akainama akaanza kuandika ardhini kwa kidole chake.
7 When they kept questioning him, he stood up and said to them, "Whichever of you has no sin, cast the first stone at her." Walipoendelea kumuulizauliza akainuka, akawaambia, “Kama kuna mtu yeyote miongoni mwenu ambaye hana dhambi na awe wa kwanza kumtupia jiwe.”
8 And once more he bent down and wrote on the ground. Akainama tena na kuandika ardhini.
9 Hearing this, they left one by one, starting with the oldest, until Jesus was left alone with the woman standing there. Waliposikia haya, wakaanza kuondoka mmoja mmoja, wakianzia wazee, hadi Isa akabaki peke yake na yule mwanamke akiwa amesimama mbele yake.
10 Jesus stood up and said to her, "Woman, where are they? Has no one condemned you?" Isa akainuka na kumwambia, “Mwanamke, wako wapi wale waliokuwa wanakuhukumu kuwa mwenye hatia?”
11 She said, "No one, Lord." Jesus said, "I don't condemn you either. Go, and from now on, don't sin anymore." Yule mwanamke akajibu, “Hakuna hata mmoja, Bwana.” Isa akamwambia, “Hata mimi sikuhukumu. Nenda zako. Kuanzia sasa usitende dhambi tena.”]
12 Jesus spoke to them again: "I am the world's light. Whoever follows me will never walk in darkness but will have the light of life." Kisha Isa akasema nao tena, akawaambia, “Mimi ni nuru ya ulimwengu. Mtu yeyote akinifuata, hatatembea gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.”
13 So the Pharisees said to him, "You are bearing witness about yourself; your testimony is not true." Mafarisayo wakamwambia, “Ushuhuda wako haukubaliki, kwa kuwa unajishuhudia mwenyewe.”
14 Jesus replied, "Even if I testify about myself, my testimony is true, because I know where I came from and where I'm going; but you don't know where I come from or where I'm going. Isa akawajibu, “Hata kama najishuhudia mwenyewe, ushuhuda wangu ni kweli, kwa sababu najua nilikotoka na ninakoenda. Lakini ninyi hamjui nilikotoka wala ninakoenda.
15 You judge according to the flesh; I judge no one. Ninyi mnahukumu kwa kufuata vipimo vya kibinadamu; mimi simhukumu mtu yeyote.
16 Even if I judge, my judgment is true, since I do not judge alone, but I and the Father who sent me. Lakini hata nikihukumu, uamuzi wangu ni sahihi kwa sababu sitoi hukumu yangu peke yangu, bali niko pamoja na Baba, aliyenituma.
17 In your Law it is written that the testimony of two people is true. Imeandikwa katika Torati yenu kwamba ushahidi wa watu wawili ni thabiti.
18 I testify about myself, and the Father who sent me testifies about me." Mimi najishuhudia mwenyewe, naye Baba aliyenituma hunishuhudia.”
19 They asked, "Where is your Father?" Jesus answered, "You know neither me nor my Father. If you knew me, you would know my Father also." Ndipo wakamuuliza, “Huyo Baba yako yuko wapi?” Isa akawajibu, “Ninyi hamnifahamu mimi ni nani, wala hammfahamu Baba yangu. Kama mngenifahamu mimi, mngemfahamu na Baba yangu.”
20 He said this while teaching in the temple, in the treasury; no one seized him—his hour had not yet come. Isa alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika chumba cha hazina Hekaluni. Lakini hakuna mtu aliyemkamata kwa kuwa saa yake ilikuwa haijawadia.
21 So he told them again, "I am going away. You will look for me and die in your sin. Where I am going, you cannot come." Isa akawaambia tena, “Ninaenda zangu, nanyi mtanitafuta, lakini mtakufa katika dhambi zenu. Niendako mimi, ninyi hamwezi kuja.”
22 So the Jews said, "Will he kill himself, since he says, "You can't come where I'm going"?" Ndipo wale Wayahudi wakasema, “Je, atajiua? Je, hii ndiyo sababu amesema, ‘Niendako mimi ninyi hamwezi kuja’?”
23 He said to them, "You're from below; I'm from above. You're of this world; I'm not of this world. Akawaambia, “Ninyi mmetoka chini; mimi nimetoka juu. Ninyi ni wa ulimwengu huu; mimi si wa ulimwengu huu.
24 I told you that you'll die in your sins; if you don't believe I AM, you'll die in your sins." Niliwaambia kuwa mtakufa katika dhambi zenu; kwa maana msipoamini kwamba ‘Mimi Ndiye,’ mtakufa katika dhambi zenu.”
25 So they said to him, "Just who are you?" Jesus said to them, "Exactly what I've said from the start. Wakamuuliza, “Wewe ni nani?” Naye Isa akawajibu, “Mimi ndiye yule ambaye nimekuwa nikiwaambia tangu mwanzo.
26 I have much to say and judge about you, but the One who sent me is true; what I heard from him, I tell the world." Nina mambo mengi ya kusema kuwahusu ya kuwahukumu. Lakini yeye aliyenituma ni wa kuaminika, nami nanena na ulimwengu niliyoyasikia kutoka kwake.”
27 They did not understand that he had been speaking to them about the Father. Hawakuelewa kuwa alikuwa akiwaambia kuhusu Baba yake wa Mbinguni.
28 So Jesus told them, "When you lift up the Son of Man, then you'll know that I AM, and that I do nothing on my own, but say these things as the Father taught me. Kisha Isa akawaambia, “Mtakapokwisha kumwinua Mwana wa Adamu juu, ndipo mtajua kuwa mimi ndiye yule niliyesema, na kwamba mimi sitendi jambo lolote peke yangu, bali ninasema yale tu Baba yangu amenifundisha.
29 The one who sent me is with me; he hasn't left me alone, because I always do what pleases him." Yeye aliyenituma yu pamoja nami; hajaniacha, kwa kuwa siku zote nafanya mapenzi yake.”
30 As he was saying these things, many believed in him. Wengi waliomsikia Isa akisema maneno haya wakamwamini.
31 Jesus then told the Jews who had believed him, "If you remain in my word, you are truly my disciples, Kisha Isa akawaambia wale Wayahudi waliomwamini, “Mkidumu katika maneno yangu, mtakuwa wanafunzi wangu kweli kweli.
32 and you will know the truth, and the truth will set you free." Ndipo mtaijua kweli, nayo kweli itawaweka huru.”
33 They answered him, "We are Abraham's descendants, never enslaved to anyone. How can you say, 'You will become free'?" Wao wakamjibu, “Sisi tu wazao wa Ibrahimu, nasi hatujakuwa watumwa wa mtu yeyote. Wawezaje kusema kwamba tutawekwa huru?”
34 Jesus answered them, "Truly, truly, I tell you: everyone who keeps sinning is sin's slave. Isa akajibu, “Amin, amin nawaambia, kila atendaye dhambi ni mtumwa wa dhambi.
35 The slave does not remain in the house forever; the son remains forever. Mtumwa hakai nyumbani anakotumika siku zote, lakini mwana hukaa nyumbani daima.
36 So if the Son sets you free, you will be free indeed. Hivyo Mwana akiwaweka huru mtakuwa huru kweli kweli.
37 I know you are Abraham's descendants; yet you seek to kill me because my word has no space in you. Ninajua ya kuwa ninyi ni wazao wa Ibrahimu, lakini mnatafuta wasaa wa kuniua kwa sababu ndani yenu hamna nafasi ya neno langu.
38 I speak what I've seen with my Father, and you do what you heard from your father." Ninasema yale niliyoyaona nikiwa mbele za Baba yangu, nanyi mnafanya yale mliyosikia kutoka kwa baba yenu.”
39 They answered, "Abraham is our father." Jesus said, "If you were Abraham's children, you'd do the works Abraham did, Wakajibu, “Baba yetu ni Ibrahimu.” Isa akawaambia, “Kama mngekuwa wazao wa Ibrahimu, mngefanya mambo yale aliyofanya Ibrahimu.
40 but now you want to kill me—a man who told you the truth I heard from my Father. Abraham didn't do this. Lakini sasa ninyi mnatafuta kuniua, mtu ambaye nimewaambia kweli ile niliyosikia kutoka kwa Mungu. Ibrahimu hakufanya jambo la namna hii.
41 You do your father's works." They said to him, "We weren't born of sexual sin. We have one Father—God himself." Ninyi mnafanya mambo afanyayo baba yenu.” Wakamjibu, “Sisi hatukuzaliwa kwa uzinzi. Tunaye Baba mmoja, Mungu pekee.”
42 Jesus said to them, "If God were your Father, you'd love me, for I came from God and am here. I didn't come on my own—he sent me. Isa akawaambia, “Kama Mungu angekuwa Baba yenu, mngenipenda, kwa maana nilitoka kwa Mungu na sasa niko hapa. Sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, ila yeye alinituma.
43 Why don't you understand my speech? Because you cannot bear to hear my word. Kwa nini hamwelewi ninayowaambia? Ni kwa sababu hamwezi kusikia nisemacho.
44 You belong to your father, the devil, and want to carry out his desires. He was a murderer from the beginning, not standing in truth, since no truth is in him. When he lies, he speaks from his own nature, since he's a liar and the lie's father. Ninyi ni watoto wa baba yenu, ibilisi, nanyi mnataka kutimiza matakwa ya baba yenu. Yeye alikuwa muuaji tangu mwanzo, wala hakushikana na kweli, maana hamna kweli ndani yake. Anaposema uongo, yeye husema lugha yake ya asili kwa maana yeye ni mwongo na baba wa huo uongo.
45 But because I tell the truth, you do not believe me. Lakini kwa sababu nimewaambia kweli, hamkuniamini!
46 Who among you convicts me of sin? If I speak truth, why don't you believe me? Je, kuna yeyote miongoni mwenu awezaye kunithibitisha kuwa mwenye dhambi? Kama nawaambia yaliyo kweli, mbona hamniamini?
47 Whoever is from our Father hears his words; you don't hear because you're not from our Father." Yeye atokaye kwa Mungu husikia kile Mungu asemacho. Sababu ya ninyi kutosikia ni kwa kuwa hamtokani na Mungu.”
48 The Jews replied, "Aren't we right in saying that you are a Samaritan and have a demon?" Wayahudi wakamjibu Isa, “Je, hatuko sahihi tunaposema kwamba wewe ni Msamaria, na kwamba una pepo mchafu?”
49 Jesus answered, "I do not have a demon, but I honor my Father, and you dishonor me. Isa akawajibu, “Mimi sina pepo mchafu, bali ninamheshimu Baba yangu, nanyi mnanidharau.
50 But I'm not seeking my own glory; our Father seeks it, and he judges. Lakini mimi sitafuti utukufu wangu mwenyewe, bali yuko anayetaka kunitukuza, naye ndiye mwamuzi.
51 Truly, truly, I say to you, if anyone keeps my word, he will never see death." Amin, amin nawaambia, mtu yeyote akilitii neno langu, hataona mauti milele.”
52 The Jews said to him, "Now we know you have a demon. Abraham died, as did the prophets, yet you say, 'Whoever keeps my word will never taste death.' Ndipo Wayahudi wakapaza sauti, wakamwambia, “Sasa tumejua kwamba una pepo mchafu! Ibrahimu alikufa, na manabii vilevile, nawe unasema kuwa mtu akitii neno lako hatakufa milele.
53 Are you greater than our father Abraham, who died? The prophets died too! Who do you claim to be?" Je, wewe ni mkuu kuliko baba yetu Ibrahimu ambaye alikufa, na manabii ambao pia walikufa? Unafikiri wewe ni nani?”
54 Jesus answered, "If I glorify myself, my glory is nothing. It is my Father who glorifies me, of whom you say, 'He is our God.' Isa akawajibu, “Nikijitukuza mwenyewe, utukufu wangu hauna maana. Baba yangu, huyo ambaye ninyi mnadai kuwa ni Mungu wenu, ndiye anitukuzaye mimi.
55 You don't know him, but I know him. If I said I didn't know him, I'd be a liar like you. But I know him and keep his word. Ingawa hamkumjua, mimi ninamjua. Kama ningesema simjui, ningekuwa mwongo kama ninyi, lakini mimi ninamjua na ninalitii neno lake.
56 Your father Abraham rejoiced that he would see my day. He saw it and was glad." Baba yenu Ibrahimu alishangilia kwamba angeiona siku yangu, naye akaiona na akafurahi.”
57 So the Jews said to him, "You're not yet fifty years old, and you've seen Abraham?" Wayahudi wakamwambia, “Wewe hujatimiza hata miaka hamsini, nawe wasema umemwona Ibrahimu?”
58 Jesus said to them, "Truly, truly, I say to you, before Abraham was, I AM." Isa akawaambia, “Amin, amin nawaambia, kabla Ibrahimu hajakuwa, Mimi niko.”
59 So they grabbed stones to throw at him, but Jesus hid himself and slipped out of the temple. Ndipo wakaokota mawe ili kumpiga, lakini Isa akajificha, naye akatoka Hekaluni.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]