Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

John 7 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 After this, Jesus traveled around Galilee, not wanting to go into Judea because Jewish leaders there were looking for a chance to kill him. Baada ya mambo haya, Isa alienda sehemu mbalimbali za Galilaya. Hakutaka kwenda Yudea kwa sababu viongozi wa Wayahudi huko walitaka kumuua.
2 But the Jewish Festival of Booths was near. Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.
3 His brothers told him, "Leave here and go to Judea, so your disciples can also see the works you do. Hivyo ndugu zake Isa wakamwambia, “Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi Wako wapate kuona miujiza unayofanya.
4 No one seeking public attention hides what he does. If you're doing these things, show yourself to the world." Mtu anayetaka kujulikana hafanyi mambo yake kwa siri. Kama unafanya mambo haya, jioneshe kwa ulimwengu.”
5 For not even his brothers believed in him. Hata ndugu zake mwenyewe hawakumwamini.
6 So Jesus told them, "My time has not yet come, but for you any time is right. Isa akawaambia, “Wakati wangu bado haujawadia, lakini wakati wenu upo siku zote.
7 "The world cannot hate you, but it hates me, because I testify that its works are evil. Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini unanichukia mimi kwa sababu ninawashuhudia kwamba matendo yao ni maovu.
8 You yourselves go up to the festival; I'm not going up to this festival, since my time hasn't yet fully come." Ninyi nendeni kwenye Sikukuu, lakini mimi sitahudhuria Sikukuu hii kwa sababu wakati wangu haujawadia.”
9 After saying this, he stayed in Galilee. Baada ya kusema hayo, akabaki Galilaya.
10 After his brothers went up to the festival, he too went up—not openly, but secretly. Lakini ndugu zake walipokwisha kuondoka kwenda kwenye Sikukuu, yeye pia alienda lakini kwa siri.
11 So the Jewish leaders were looking for him at the festival and asking, "Where is he?" Viongozi wa Wayahudi walikuwa wakimtafuta huko kwenye Sikukuu na kuulizana, “Yuko wapi huyu mtu?”
12 Much murmuring about him spread among the crowds: some said, "He's good," others, "No, he misleads the crowd." Kulikuwa na minong’ono iliyoenea kumhusu Isa katika umati wa watu, wakati wengine wakisema, “Ni mtu mwema.” Wengine walikuwa wakisema, “La, yeye anawadanganya watu.”
13 Yet no one spoke about him openly, for fear of the Jewish leaders. Lakini hakuna mtu yeyote aliyemsema waziwazi kwa sababu ya kuwaogopa viongozi wa Wayahudi.
14 About the middle of the festival, Jesus went up into the temple and began to teach. Ilipokaribia katikati ya Sikukuu, Isa alipanda kwenda Hekaluni na kuanza kufundisha.
15 The Jewish leaders were amazed and asked, "How does this man know so much without training?" Wayahudi wakastaajabia mafundisho yake wakasema, “Mtu huyu amepataje kujua mambo haya bila kufundishwa?”
16 Jesus answered them, "My teaching isn't mine—it's from the one who sent me. Ndipo Isa akawajibu, “Mafundisho yangu si yangu mwenyewe, bali yanatoka kwake yeye aliyenituma.
17 Whoever wants to do our Father's will knows if my teaching is from my Father or I speak on my own. Mtu yeyote akipenda kufanya mapenzi ya Mungu, atajua kama mafundisho yangu yanatoka kwa Mungu au ninasema kwa ajili yangu mwenyewe.
18 Whoever speaks on his own seeks his own glory, but whoever seeks the sender's glory is true, with no falsehood in him. Wale wanenao kwa ajili yao wenyewe hufanya hivyo kwa kutaka utukufu wao wenyewe. Lakini yeye atafutaye utukufu wa yule aliyemtuma ni wa kweli, wala hakuna uongo ndani yake.
19 Didn't Moses give you the law? Yet none of you obeys the law. Why are you trying to kill me?" Je, Musa hakuwapa ninyi sheria? Lakini hakuna hata mmoja wenu anayeishika hiyo sheria. Kwa nini mnataka kuniua?”
20 The crowd answered, "You have a demon! Who is trying to kill you?" Ule umati wa watu wakamjibu, “Wewe una pepo mchafu! Ni nani anayetaka kukuua?”
21 Jesus replied, "I did one work, and you are all amazed. Isa akawajibu, “Nimefanya muujiza mmoja na nyote mkastaajabu.
22 "Moses gave you circumcision—not from Moses, but the patriarchs—and you circumcise a man on the Sabbath. Lakini kwa kuwa Musa aliwaamuru tohara (ingawa kwa kweli haikutoka kwa Musa bali kwa baba zetu wa zamani), mnamtahiri mtoto hata siku ya Sabato.
23 If a man is circumcised on the Sabbath so the law of Moses isn't broken, why are you angry at me for making a whole man well on the Sabbath? Ikiwa mtoto aweza kutahiriwa siku ya Sabato kusudi Torati ya Musa isivunjwe, kwa nini mnanikasirikia kwa kumponya mtu mwili wake wote siku ya Sabato?
24 Stop judging by appearances, and judge with right judgment." Acheni kuhukumu mambo kwa jinsi mnavyoona tu, bali hukumuni kwa haki.”
25 Then some Jerusalemites said, "Isn't this the man they want to kill? Ndipo baadhi ya watu wa Yerusalemu wakawa wanasema, “Tazameni, huyu si yule mtu wanayetaka kumuua?
26 Yet he speaks openly, and they say nothing to him. Can the rulers truly know this is the Christ? Mbona yuko hapa anazungumza hadharani, na wala hawamwambii neno lolote? Je, inawezekana viongozi wanafahamu kuwa huyu ndiye Al-Masihi?
27 But we know this man's origin. When the Christ comes, no one will know his origin." Tunafahamu huyu mtu anakotoka, lakini Al-Masihi atakapokuja, hakuna yeyote atakayejua atokako.”
28 Then Jesus, teaching in the temple, cried out: "You know me, and know where I'm from. Yet I didn't come on my own—the one who sent me is true, and you don't know him. Ndipo Isa, akaendelea kufundisha Hekaluni, akisema, “Ninyi mnanifahamu na kujua nitokako. Mimi sikuja kwa ajili yangu mwenyewe, bali yeye aliyenituma ni wa kweli na ninyi hammjui.
29 I know him, because I am from him, and he sent me." Mimi namjua kwa kuwa nimetoka kwake, naye ndiye alinituma.”
30 So they tried to grab him, but no one touched him, because his hour had not yet come. Ndipo wakatafuta kumkamata, lakini hakuna mtu yeyote aliyethubutu kumshika kwa sababu saa yake ilikuwa bado haijawadia.
31 But many in the crowd believed in him, asking, "When the Christ comes, will he do more signs than this man did?" Nao watu wengi wakamwamini, wakasema, “Je, Al-Masihi atakapokuja, atafanya miujiza mikuu kuliko aliyoifanya mtu huyu?”
32 The Pharisees heard the crowd murmuring these things about him, so the chief priests and Pharisees sent temple guards to seize him. Mafarisayo wakasikia watu wakinong’ona mambo kama hayo kuhusu Isa, ndipo wao pamoja na viongozi wa makuhani wakatuma walinzi wa Hekalu waende kumkamata.
33 So Jesus said, "I'm with you a little while longer, and then I go to the one who sent me. Isa akasema, “Mimi bado niko pamoja nanyi kwa kitambo kidogo, kisha nitarudi kwake yeye aliyenituma.
34 You will search for me and not find me; you cannot come where I am." Mtanitafuta lakini hamtaniona, nami niliko ninyi hamwezi kuja.”
35 So the Jewish leaders asked each other, "Where does he intend to go that we won't find him? Does he intend to go to our people dispersed among the Greeks and teach the Greeks? Wayahudi wakaulizana wao kwa wao, “Huyu mtu anataka kwenda wapi ambako hatuwezi kumfuata? Je, anataka kwenda kwa Wayunani ambako baadhi ya watu wetu wametawanyikia, akawafundishe Wayunani?
36 What does he mean: 'You will look for me, but you will not find me,' and 'Where I am, you cannot come'?" Yeye ana maana gani anaposema, ‘Mtanitafuta lakini hamtaniona,’ na, ‘nami niliko ninyi hamwezi kuja’?”
37 On the last, great day of the festival, Jesus stood and called out, "Whoever is thirsty, let him come to me and drink. Siku ile ya mwisho ya Sikukuu, siku ile kuu, wakati Isa akiwa amesimama huko, akapaza sauti yake akasema, “Kama mtu yeyote anaona kiu na aje kwangu anywe.
38 Whoever believes in me, as Scripture said, rivers of living water will flow from his heart." Yeyote aniaminiye mimi, kama Maandiko yanavyosema, vijito vya maji ya uzima vitatiririka kutoka ndani yake.”
39 He said this about the Holy Spirit, whom believers in him were to receive; the Spirit had not yet been given, since Jesus had not yet been glorified. Isa aliposema haya, alimaanisha Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye wote waliomwamini wangempokea. Kwa maana hadi wakati huo Roho wa Mungu alikuwa hajatolewa, kwa kuwa Isa alikuwa bado hajatukuzwa.
40 When they heard these words, some of the crowd said, "This really is the Prophet." Waliposikia maneno hayo, baadhi ya watu miongoni mwa umati ule wakasema, “Hakika huyu ndiye yule Nabii.”
41 Others said, "This is the Christ." But others asked, "How can the Christ come from Galilee? Wengine wakasema, “Huyu ndiye Al-Masihi!” Lakini wengine wakauliza, “Je, Al-Masihi kwao ni Galilaya?
42 Doesn't Scripture say the Christ comes from David's line and from Bethlehem, David's village?" Je, Maandiko hayasemi kwamba Al-Masihi atakuja kutoka jamaa ya Daudi na kutoka Bethlehemu, mji alioishi Daudi?”
43 So the crowd was divided over him. Kwa hiyo watu wakagawanyika kwa ajili ya Isa.
44 Some of them wanted to seize him, but no one laid a hand on him. Baadhi yao walitaka kumkamata, lakini hakuna aliyethubutu kumgusa.
45 So the temple guards returned to the chief priests and Pharisees, who asked, "Why didn't you bring him?" Hatimaye wale walinzi wa Hekalu wakarudi kwa viongozi wa makuhani na Mafarisayo waliokuwa wamewatuma ili kumkamata Isa, wakaulizwa, “Mbona hamkumkamata?”
46 The guards answered, "No one ever spoke the way this man does." Wale walinzi wakajibu, “Kamwe hajanena mtu yeyote kama yeye anenavyo.”
47 "Have you also been deceived?" the Pharisees answered. Mafarisayo wakajibu, “Je, nanyi pia mmedanganyika?
48 "Has any of the rulers or of the Pharisees believed in him? Je, kuna kiongozi yeyote au mmoja wa Mafarisayo ambaye amemwamini?
49 But this crowd, who knows nothing of the law—they are under a curse." Lakini umati huu wa watu wasiojua Torati ya Musa, wamelaaniwa.”
50 Nicodemus, who had gone to Jesus earlier and was one of their own number, asked them, Ndipo Nikodemo, yule aliyekuwa amemwendea Isa siku moja usiku, na alikuwa mmoja wao, akauliza,
51 "Does our law condemn a man without first hearing him and finding out what he does?" “Je, sheria zetu zinaturuhusu kumhukumu mtu kabla ya kumsikiliza na kufahamu alilotenda?”
52 They replied, "Are you from Galilee too? Search, and see: no prophet arises from Galilee." Wakamjibu, “Je, wewe pia unatoka Galilaya? Chunguza nawe utaona kwamba hakuna nabii atokae Galilaya!” [
53 Then they all went home. Kisha wakaondoka, kila mtu akarudi nyumbani mwake.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]