Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

John 6 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 After this, Jesus crossed the Sea of Galilee, also called the Sea of Tiberias. Baada ya haya, Isa alienda ng’ambo ya Bahari ya Galilaya (ambayo pia huitwa Bahari ya Tiberia).
2 A large crowd followed him, because they saw the signs he performed on the sick. Umati mkubwa wa watu waliendelea kumfuata, kwa sababu waliona ishara nyingi za miujiza alizofanya kwa wagonjwa.
3 Jesus went up on the mountainside and sat down there with his disciples. Kisha Isa akapanda mlimani akaketi huko pamoja na wanafunzi wake.
4 Now the Passover, the feast of the Jews, was near. Pasaka ya Wayahudi ilikuwa imekaribia.
5 Looking up, Jesus saw a large crowd approaching and asked Philip, "Where can we buy bread for these people to eat?" Isa alipotazama na kuona umati ule mkubwa wa watu wakimjia, akamwambia Filipo, “Tutanunua wapi mikate ili watu hawa wale?”
6 He said this to test Philip, for he himself already knew what he was going to do. Aliuliza swali hili kumpima, kwa maana alishajua la kufanya.
7 Philip answered him, "200 days' wages of bread isn't enough for each of them to get a little." Filipo akamjibu, “Hata fedha kiasi cha dinari mia mbili hazitoshi kununua mikate ya kuwapa watu hawa ili kila mtu apate kidogo.”
8 One of his disciples, Andrew, Simon Peter's brother, said to him, Mmoja wa wanafunzi wake aitwaye Andrea, ndugu yake Simoni Petro, akamwambia,
9 "A boy here has five barley loaves and two fish—but what's that for so many?" “Hapa kuna mvulana mmoja mwenye mikate mitano ya shayiri na samaki wawili wadogo. Lakini hivi vitatosha nini kwa watu hawa wote?”
10 Jesus said, "Have the people sit down." Much grass grew there, so about 5,000 men sat down. Isa akasema, “Waketisheni watu chini.” Palikuwa na majani mengi katika eneo lile, nao watu wakaketi (palikuwa na wanaume wapatao elfu tano).
11 Jesus then took the loaves, gave thanks, and distributed them to those seated; likewise with the fish, as much as they wanted. Ndipo Isa akachukua ile mikate, akamshukuru Mungu na kuwagawia wale watu waliokuwa wameketi. Akafanya vivyo hivyo na wale samaki. Kila mtu akapata kadiri alivyotaka.
12 When they were full, he told his disciples, "Gather the leftover pieces, so nothing is lost." Watu wote walipokwisha kula na kushiba, akawaambia wanafunzi wake, “Kusanyeni vipande vilivyobaki vya ile mikate, kisipotee chochote.”
13 So they gathered the fragments left over from the five barley loaves after the people ate, filling twelve baskets. Hivyo wakavikusanya, wakajaza vikapu kumi na viwili kwa vipande vya ile mikate mitano ya shayiri na samaki wale wawili wadogo vilivyobakishwa na waliokula.
14 So when the people saw the sign he did, they said, "This really is the Prophet coming into the world!" Baada ya watu kuona muujiza ule Isa aliofanya, walianza kusema, “Hakika huyu ndiye Nabii ajaye ulimwenguni!”
15 Knowing they meant to come and seize him to make him king, Jesus withdrew again to the mountain alone. Isa akijua kwamba walitaka kuja kumfanya awe mfalme wao, kwa nguvu, akajitenga nao akaenda milimani peke yake.
16 When evening came, his disciples went down to the sea, Ilipofika jioni, wanafunzi wake waliteremka kwenda baharini.
17 got in a boat and headed across the sea to Capernaum. It was already dark, and Jesus had not yet reached them. Wakaingia kwenye mashua, wakaanza kuvuka bahari kwenda Kapernaumu. Wakati huu kulikuwa tayari giza na Isa alikuwa hajajumuika nao.
18 A strong wind was blowing, and the sea grew rough. Bahari ikachafuka kwa sababu upepo mkali ulikuwa unavuma.
19 After rowing three or four miles, they saw Jesus walking on the water, approaching the boat, and were afraid. Wanafunzi walipokuwa wameenda mwendo wa maili tatu au nne, walimwona Isa akitembea juu ya maji akikaribia mashua, nao wakaogopa sana.
20 But he said to them, "It is I; do not be afraid." Lakini Isa akawaambia, “Ni mimi. Msiogope.”
21 So they were glad to take him into the boat, and instantly it reached the shore they were heading toward. Ndipo wakamkaribisha kwa furaha ndani ya mashua, na mara wakafika ufuoni walikokuwa wakienda.
22 The next day, the crowd remaining on the far shore saw that only one boat had been there, that Jesus had not boarded it with his disciples, but that his disciples had gone off alone. Siku iliyofuata, wale watu waliokuwa wamebaki ng’ambo waliona kwamba palikuwa na mashua moja tu, na kwamba Isa hakuwa ameondoka pamoja na wanafunzi wake, ila walikuwa wameondoka peke yao.
23 Other boats came from Tiberias near the place where they ate bread after the Lord gave thanks. Lakini zikaja mashua nyingine kutoka Tiberia zikafika karibu na mahali pale walipokula mikate baada ya Bwana Isa kumshukuru Mungu.
24 So when the crowd saw Jesus and his disciples weren't there, they got in boats and went to Capernaum to look for Jesus. Mara wale watu wakatambua kwamba Isa hakuwa hapo, wala wanafunzi wake. Wakaingia kwenye mashua hizo, wakaenda Kapernaumu ili kumtafuta Isa.
25 Finding him across the sea, they asked, "Rabbi, when did you get here?" Walipomkuta Isa ng’ambo ya bahari wakamuuliza, “Mwalimu, umefika lini huku?”
26 Jesus answered them, "Truly, truly, I tell you: you seek me not because you saw signs, but because you ate the loaves and were filled. Isa akawajibu, “Amin, amin nawaambia, ninyi hamnitafuti kwa kuwa mliona ishara na miujiza, bali kwa sababu mlikula ile mikate mkashiba.
27 Don't work for food that spoils, but for food that lasts to eternal life, which the Son of Man will give you. For on him our Father has set his seal." Msishughulikie chakula kiharibikacho, bali chakula kidumucho hata uzima wa milele, ambacho Mwana wa Adamu atawapa. Yeye ndiye ambaye Mungu Baba Mwenyezi amemtia muhuri.”
28 Then they said to him, "What must we do to be doing the works of our Father?" Ndipo wakamuuliza, “Tufanye nini ili tupate kuitenda kazi ya Mungu?”
29 Jesus answered them, "This is our Father's work: that you believe in the one he sent." Isa akawajibu, “Kazi ya Mungu ndiyo hii: Mwaminini yeye aliyetumwa naye.”
30 So they asked him, "What sign will you give, so we may see and believe you? What work will you do? Hivyo wakamuuliza, “Utafanya ishara gani ya muujiza, ili tuione tukuamini? Utafanya jambo gani?
31 Our ancestors ate manna in the wilderness, as it is written: 'He gave them bread from heaven to eat.'" Baba zetu walikula mana jangwani, kama ilivyoandikwa, ‘Aliwapa mikate kutoka mbinguni ili wale.’ ”
32 Jesus told them, "Truly, truly, I tell you: Moses didn't give you the bread from heaven—my Father gives you the true bread from heaven. Isa akawaambia, “Amin, amin nawaambia, si Musa aliyewapa mikate kutoka mbinguni, bali Baba yangu ndiye anawapa mkate wa kweli kutoka mbinguni.
33 For the bread of our Father is he who comes down from heaven and gives the world life." Kwa maana mkate wa Mungu ni yule ashukaye kutoka mbinguni na kuupa ulimwengu uzima.”
34 So they said to him, "Lord, give us this bread always." Wakamwambia, “Bwana, kuanzia sasa tupatie huo mkate siku zote.”
35 Jesus told them, "I am the bread of life. Whoever comes to me will never hunger; whoever believes in me will never thirst. Isa akawaambia, “Mimi ndimi mkate wa uzima. Yeye ajaye kwangu, hataona njaa kamwe na yeye aniaminiye, hataona kiu kamwe.
36 But as I told you, you have seen me and still do not believe. Lakini kama nilivyowaambia, mmeniona lakini bado hamwamini.
37 All the Father gives me will come to me, and the one who comes to me I will never drive away. Wale wote anipao Baba watakuja kwangu na yeyote ajaye kwangu, sitamfukuza nje kamwe.
38 For I came down from heaven not to do my own will, but the will of him who sent me. Kwa kuwa nimeshuka kutoka mbinguni si ili kufanya mapenzi yangu, bali mapenzi yake yeye aliyenituma.
39 This is the will of him who sent me: that I lose none of all he has given me, but raise them up on the last day. Haya ndio mapenzi yake yeye aliyenituma, kwamba, nisimpoteze hata mmoja wa wale alionipa, bali niwafufue siku ya mwisho.
40 For this is the will of my Father: that everyone who looks to the Son and believes in him should have eternal life, and I will raise them up on the last day." Kwa maana mapenzi ya Baba yangu ni kwamba kila mmoja amtazamaye, Mwana na kumwamini awe na uzima wa milele, nami nitawafufua siku ya mwisho.”
41 So the Jews grumbled about him because he said, "I am the bread that came down from heaven." Wayahudi wakaanza kunung’unika kwa kuwa alisema, “Mimi ndimi mkate ulioshuka kutoka mbinguni.”
42 They said, "Isn't this Jesus, Joseph's son, whose father and mother we know? How can he now say, 'I have come down from heaven'?" Wakasema, “Huyu si Isa, mwana wa Yusufu, ambaye baba yake na mama yake tunawajua? Anawezaje basi sasa kusema, ‘Nimeshuka kutoka mbinguni’?”
43 Jesus answered them, "Stop grumbling among yourselves. Hivyo Isa akawaambia, “Acheni kunung’unikiana ninyi kwa ninyi.
44 "No one can come to me unless the Father who sent me draws him, and I will raise him on the last day. Hakuna mtu awezaye kuja kwangu kama asipovutwa na Baba aliyenituma, nami nitamfufua siku ya mwisho.
45 It is written in the Prophets: 'And they will all be taught by our Father.' Everyone who has heard and learned from the Father comes to me. Imeandikwa katika Manabii, ‘Wote watafundishwa na Mungu.’ Yeyote amsikilizaye Baba na kujifunza kutoka kwake, huyo huja kwangu.
46 Not that anyone has seen the Father except the one from him; he has seen the Father. Hakuna mtu yeyote aliyemwona Baba isipokuwa yeye atokaye kwa Mungu, yeye ndiye peke yake aliyemwona Baba.
47 Truly, truly, I tell you, whoever believes has eternal life. Amin, amin nawaambia, yeye anayeamini anao uzima wa milele.
48 I am the bread of life. Mimi ni mkate wa uzima.
49 Your ancestors ate the manna in the wilderness, yet they died. Baba zenu walikula mana jangwani, lakini wakafa.
50 This is the bread that comes down from heaven, so anyone may eat it and not die. Lakini hapa kuna mkate kutoka mbinguni, ambao mtu yeyote akiula, hatakufa.
51 I am the living bread come down from heaven. Whoever eats this bread will live forever. The bread I will give is my flesh, for the life of the world." Mimi ni mkate wa uzima ule uliotoka mbinguni. Mtu yeyote akiula mkate huu, ataishi milele. Mkate huu ni mwili wangu, ambao nitautoa kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.”
52 Then the Jews argued sharply among themselves, "How can this man give us his flesh to eat?" Ndipo Wayahudi wakaanza kuhojiana vikali wao kwa wao wakisema, “Mtu huyu awezaje kutupatia mwili wake tuule?”
53 Jesus told them, "Truly, truly, I tell you, unless you eat the flesh of the Son of Man and drink his blood, you have no life in yourselves. Hivyo Isa akawaambia, “Amin, amin nawaambia, msipoula mwili wa Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu.
54 Whoever feeds on my flesh and drinks my blood has eternal life, and I will raise him on the last day. Mtu yeyote aulaye mwili wangu na kunywa damu yangu, anao uzima wa milele. Nami nitamfufua siku ya mwisho.
55 For my flesh is true food, and my blood is true drink. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli na damu yangu ni kinywaji cha kweli.
56 Whoever feeds on my flesh and drinks my blood remains in me, and I in him. Yeyote alaye mwili wangu na kunywa damu yangu, atakaa ndani yangu nami nitakaa ndani yake.
57 As the living Father sent me and I live because of the Father, so whoever feeds on me will live because of me. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, na kama nami ninavyoishi kwa sababu ya Baba, hivyo anilaye mimi ataishi kwa sababu yangu.
58 This is the bread that came down from heaven. It is not like the bread your ancestors ate and still died. Whoever feeds on this bread will live forever." Huu ndio mkate ushukao kutoka mbinguni, si kama ule mkate baba zenu waliokula nao wakafa. Lakini yeye aulaye mkate huu ataishi milele.”
59 He said these things while teaching in the synagogue at Capernaum. Isa alisema maneno haya alipokuwa akifundisha katika sinagogi huko Kapernaumu.
60 On hearing it, many of his disciples said, "This is a hard teaching. Who can accept it?" Wengi wa wafuasi wake waliposikia jambo hili wakasema, “Mafundisho haya ni magumu. Ni nani awezaye kuyapokea?”
61 Aware that his disciples were grumbling about this, Jesus said to them, "Does this offend you? Isa alipojua kwamba wafuasi wake wananung’unika kuhusu mafundisho yake, akawaambia, “Je, jambo hili limewaudhi?
62 "Then what if you see the Son of Man ascending to where he was before? Ingekuwaje basi kama mngemwona Mwana wa Adamu akipaa kwenda zake huko alipokuwa kwanza?
63 The Spirit gives life; the flesh helps nothing. The words I have spoken to you are spirit and life. Roho ndiye atiaye uzima, mwili haufai kitu. Maneno haya niliyowaambia ni Roho tena ni uzima.
64 But some of you don't believe." For Jesus knew from the start who didn't believe, and who would betray him. Lakini baadhi yenu hamwamini.” Kwa maana Isa alifahamu tangu mwanzo wale ambao hawangemwamini miongoni mwao na yule ambaye angemsaliti.
65 And he said, "This is why I told you: no one can come to me unless the Father enables him." Akaendelea kusema, “Hii ndiyo sababu niliwaambia kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu.”
66 From this time many of his disciples turned back and no longer walked with him. Tangu wakati huo wafuasi wake wengi wakarejea nyuma wakaacha kumfuata.
67 So Jesus asked the Twelve, "Do you want to leave too?" Hivyo Isa akawauliza wale wanafunzi wake kumi na wawili, “Je, ninyi pia mnataka kuondoka?”
68 Simon Peter answered him, "Lord, to whom should we go? You have the words of eternal life. Simoni Petro akamjibu, “Bwana, tuondoke twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele.
69 We have believed and known you are the Holy One of our Father." Tunaamini na kujua kuwa wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu.”
70 Jesus answered them, "Have I not chosen you, the Twelve? Yet one of you is a devil." Ndipo Isa akajibu, “Je, sikuwachagua ninyi kumi na wawili? Lakini mmoja wenu ni ibilisi.”
71 He meant Judas, son of Simon Iscariot, one of the Twelve, who was about to betray him. (Hapa alikuwa anasema kuhusu Yuda, mwana wa Simoni Iskariote. Ingawa alikuwa mmoja wa wale kumi na wawili, ndiye ambaye baadaye angemsaliti Isa.)
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]