Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

John 10 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 "Truly, truly, I tell you: whoever doesn't enter the sheepfold through the gate, but climbs in another way, is a thief and a robber. “Amin, amin nawaambia, yeye asiyeingia katika zizi la kondoo kupitia kwenye lango, lakini akwea kuingia ndani kwa njia nyingine, huyo ni mwizi na mnyang’anyi.
2 But the one who enters by the gate is the shepherd of the sheep. Yeye anayeingia kupitia kwenye lango ndiye mchungaji wa kondoo.
3 The gatekeeper opens for him, and the sheep hear his voice. He calls his own sheep by name and leads them out. Mlinzi humfungulia lango, na kondoo huisikia sauti yake. Yeye huwaita kondoo wake kwa majina yao na kuwatoa nje ya zizi.
4 After bringing all his own out, he goes ahead of them, and the sheep follow him because they know his voice. Baada ya kuwatoa wote nje, yeye hutangulia mbele yao na kondoo humfuata, kwa kuwa wanaijua sauti yake.
5 They will never follow a stranger—they'll run from him, since they don't know the voice of strangers." Lakini kondoo hawatamfuata mgeni, bali watamkimbia kwa sababu hawaijui sauti ya mgeni.”
6 Jesus told them this figure of speech, but they didn't grasp what he meant. Isa alitumia mfano huu, lakini wao hawakuelewa hayo aliyokuwa akiwaambia.
7 So Jesus said again, "Truly, truly, I tell you, I am the gate for the sheep. Kwa hiyo Isa akasema nao tena, akawaambia, “Amin, amin nawaambia, mimi ndimi lango la kondoo.
8 "All who came before me are thieves and robbers, but the sheep did not listen to them. Wote walionitangulia ni wezi na wanyang’anyi, nao kondoo hawakuwasikia.
9 I am the gate; whoever enters through me will be saved, going in and out, finding pasture. Mimi ndimi lango. Yeyote anayeingia zizini kupitia kwangu ataokoka. Ataingia na kutoka, naye atapata malisho.
10 The thief comes only to steal, kill, and destroy. I came so they may have life, and have it in abundance. Mwizi huja ili aibe, aue na aangamize. Mimi nimekuja ili wapate uzima, kisha wawe nao tele.
11 "I am the good shepherd. The good shepherd lays down his life for the sheep. “Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
12 The hired hand, not a shepherd, doesn't own the sheep. Seeing the wolf coming, he leaves the sheep and flees—the wolf snatches and scatters them. Mtu wa kuajiriwa sio mchungaji mwenye kondoo. Anapomwona mbwa-mwitu akija, yeye hukimbia na kuwaacha kondoo. Naye mbwa-mwitu hulishambulia kundi na kulitawanya.
13 The man runs away because he is a hired hand and cares nothing for the sheep. Yeye hukimbia kwa sababu ameajiriwa wala hawajali kondoo.
14 "I am the good shepherd. I know my own and my own know me, “Mimi ndimi mchungaji mwema. Ninawajua kondoo wangu, nao kondoo wangu wananijua.
15 as the Father knows me and I know the Father, and I lay down my life for the sheep. Kama vile Baba anavyonijua mimi, nami ninavyomjua Baba, ndivyo nami ninautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.
16 I have other sheep not of this fold; I must lead them too, and they will hear my voice. They will become one flock, one shepherd. Ninao kondoo wengine ambao si wa zizi hili. Inanipasa kuwaleta, nao wataisikia sauti yangu; hivyo patakuwa na kundi moja na mchungaji mmoja.
17 This is why the Father loves me: I lay down my life only to take it up again. Baba yangu ananipenda kwa kuwa ninautoa uhai wangu ili niupate tena.
18 No one takes it from me, but I lay it down on my own. I have authority to lay it down, and authority to take it up again. This charge I received from my Father." Hakuna mtu aniondoleaye uhai wangu, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai wangu, na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena. Amri hii nimepewa na Baba yangu.”
19 These words brought division among the Jews once again. Waliposikia maneno haya, Wayahudi wakagawanyika.
20 Many of them said, "He is demon-possessed and out of his mind. Why listen to him?" Wengi wao wakasema, “Huyu amepagawa na pepo mchafu, naye amechanganyikiwa.”
21 But others said, "These aren't a demon-possessed man's words. Can a demon open blind eyes?" Wengine wakasema, “Haya si maneno ya mtu aliyepagawa na pepo mchafu. Je, pepo mchafu aweza kufungua macho ya kipofu?”
22 Then came the Feast of Dedication at Jerusalem. It was winter, Ikafika Sikukuu ya Kuwekwa wakfu kwa Hekalu huko Yerusalemu. Ilikuwa majira ya baridi.
23 and Jesus was walking in the temple, in Solomon's Colonnade. Naye Isa alikuwa akitembea ndani ya Hekalu katika Ukumbi wa Sulemani.
24 The Jews surrounded him and said, "How long will you hold us in suspense? If you are the Christ, tell us plainly." Wayahudi wakamkusanyikia, wakamuuliza, “Utatuweka katika hali ya mashaka hadi lini? Kama wewe ndiwe Al-Masihi, tuambie waziwazi.”
25 Jesus answered, "I told you, and you don't believe. The works I do in my Father's name testify about me, Isa akawajibu, “Nimewaambia, lakini hamwamini. Mambo ninayoyatenda kwa jina la Baba yangu yananishuhudia.
26 but you do not believe, because you are not my sheep. Lakini hamwamini, kwa sababu ninyi si wa kundi la kondoo wangu.
27 My sheep listen to my voice; I know them, and they follow me. Kondoo wangu huisikia sauti yangu nami nawajua, nao hunifuata.
28 I give them eternal life, and they will never perish, and no one will snatch them from my hand. Nami ninawapa uzima wa milele; hawataangamia kamwe, wala hakuna mtu atakayewapokonya kutoka mikono yangu.
29 My Father, who gave them to me, is greater than all; no one can snatch them out of the Father's hand. Baba yangu aliyenipa hawa ni mkuu kuliko wote, na hakuna awezaye kuwapokonya kutoka mikononi mwake.
30 I and the Father are one." Mimi na Baba yangu tu umoja.”
31 Again the Jews picked up stones to stone him. Kwa mara nyingine Wayahudi wakainua mawe ili wampige nayo,
32 Jesus replied, "I have shown you many good works from the Father. For which of these are you going to stone me?" lakini Isa akawaambia, “Nimewaonesha miujiza mingi mikubwa kutoka kwa Baba yangu. Ni kwa ipi kati ya hiyo miujiza mnataka kunipiga mawe?”
33 "We're stoning you not for good work," they said, "but for blasphemy, because you, a mere man, claim to be God." Wayahudi wakamjibu, “Hatukupigi mawe kwa sababu ya mambo mema uliyotenda, bali ni kwa kuwa umekufuru. Ingawa wewe ni mwanadamu, unajifanya kuwa Mungu.”
34 Jesus answered them, "Is it not written in your Law: 'I have said you are gods'? Isa akawajibu, “Je, haikuandikwa katika Torati yenu kwamba, ‘Nimesema kuwa ninyi ni “miungu” ’?
35 If he called them 'gods,' to whom the word of my Father came—and Scripture cannot be broken, Kama aliwaita ‘miungu’ wale ambao neno la Mungu liliwafikia, nayo Maandiko hayawezi kutanguka,
36 what about the one the Father set apart and sent into the world? Why accuse me of blasphemy for saying, 'I am the Son of our Father'? je, mwawezaje kusema kwamba yule ambaye Baba amemweka wakfu na kumtuma ulimwenguni anakufuru, kwa sababu nilisema, ‘Mimi ni Mwana wa Mungu’?
37 "If I am not doing the works of my Father, then do not believe me. Ikiwa sifanyi kazi za Baba yangu, basi msiniamini.
38 But if I do them, even if you won't believe me, believe the works, so you'll know and keep knowing the Father is in me, and I in the Father." Lakini ikiwa nazifanya kazi za Mungu, hata kama hamniamini mimi ziaminini hizo kazi, ili mpate kujua na kuelewa kwamba Baba yu ndani yangu, nami ni ndani yake.”
39 Again they tried to seize him, but he escaped their grasp. Ndipo wakajaribu kumkamata kwa mara nyingine, lakini akaponyoka kutoka mikononi mwao.
40 Jesus then went back across the Jordan, to the place where John had first been baptizing, and stayed there. Isa akaenda tena ng’ambo ya Yordani hadi mahali Yahya alikuwa akibatiza hapo awali, naye akakaa huko.
41 Many came to him, saying, "John performed no sign, but all John said about this man was true." Watu wengi wakamjia, nao wakawa wakisema, “Yahya hakufanya muujiza wowote, lakini kila jambo alilosema kumhusu huyu mtu ni kweli.”
42 And in that place many believed in him. Nao watu wengi wakamwamini Isa huko.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]