Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Leviticus 3 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 "If someone's offering is a peace offering from the herd, male or female, he must present it without defect before me. “ ‘Ikiwa mtu anatoa sadaka ya amani, naye akatoa ng’ombe, akiwa dume au jike, atamleta mnyama asiye na dosari mbele za Mwenyezi Mungu.
2 He lays his hand on his offering's head and slaughters it at the tent of meeting's entrance, and Aaron's sons the priests splash the blood against all sides of the altar. Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake na kumchinja penye ingilio la Hema la Kukutania. Ndipo makuhani, wana wa Haruni, watanyunyiza damu ya huyo mnyama pande zote za madhabahu.
3 From the peace offering he must present to me a food offering made by fire: the fat covering the inner parts and all the fat on them, Katika hiyo sadaka ya amani ataleta sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto: sehemu za ndani na mafuta yote yanayoungana nazo,
4 both kidneys with the fat on them near the flanks, and the long lobe of the liver, which he removes with the kidneys. figo zote pamoja na mafuta yaliyozifunika karibu na kiuno, na kipande kirefu cha ini; utayaondoa pamoja na figo.
5 Aaron's sons will burn it on the altar atop the burnt offering on the wood over the fire—a food offering, a pleasing aroma to me. Kisha wana wa Haruni wataiteketeza juu ya madhabahu, juu ya ile sadaka ya kuteketezwa iliyo juu ya kuni zinazowaka; ni sadaka ya kuteketezwa kwa moto, harufu nzuri ya kumpendeza Mwenyezi Mungu.
6 "If his peace offering to me is from the flock, male or female, he must present it without defect. “ ‘Akitoa kondoo au mbuzi kutoka kundi kuwa sadaka ya amani kwa Mwenyezi Mungu, atamtoa dume au jike asiye na dosari.
7 If he brings a lamb as his offering, he is to present it before me, Akimtoa mwana-kondoo, atamleta mbele za Mwenyezi Mungu.
8 lay his hand on the head of his offering and slaughter it before the tent of meeting; Aaron's sons will splash its blood on all sides of the altar. Ataweka mkono wake juu ya kichwa cha sadaka yake, naye atamchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Haruni watanyunyiza damu ya huyo mnyama pande zote za madhabahu.
9 From the peace offering he must present a food offering to me by fire: its fat, the whole fat tail cut off close to the backbone, the fat covering the inner parts, and all the fat on them, Katika hiyo sadaka ya amani ataleta dhabihu iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto: mafuta yake, mafuta yote ya mkia uliokatwa karibu na uti wa mgongo, mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani au yale yanayounganika nazo,
10 both kidneys with the fat near the loins, and the liver's long lobe, which he removes with the kidneys. figo mbili pamoja na mafuta yanayozifunika yaliyo karibu na kiuno, na kipande kirefu cha ini, ambayo utayaondoa pamoja na figo.
11 The priest will burn it on the altar as food, an offering made to me by fire. Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu viwe chakula, sadaka iliyotolewa kwa Mwenyezi Mungu kwa moto.
12 "If his offering is a goat, he is to present it before me, “ ‘Ikiwa sadaka yake ni mbuzi, ataileta mbele za Mwenyezi Mungu.
13 lay his hand on its head and slaughter it in front of the tent of meeting; Aaron's sons will splash its blood on all sides of the altar. Ataweka mkono wake juu ya kichwa chake na kumchinja mbele ya Hema la Kukutania. Kisha wana wa Haruni watanyunyiza damu ya huyo mnyama pande zote za madhabahu.
14 From it he must present a food offering to me by fire: the fat covering the inner parts and all the fat on them, Katika ile sadaka anayotoa, atatoa hii sadaka ya kuteketezwa kwa Mwenyezi Mungu: mafuta yote yanayofunika sehemu za ndani na yale yanayoungana nazo,
15 both kidneys with their fat near the loins, and the liver's long lobe, which he removes with the kidneys. figo zote mbili pamoja na mafuta yaliyo juu yake karibu na kiuno, na kipande kirefu cha ini, ambayo atayaondoa pamoja na figo.
16 The priest will burn them on the altar as food, an offering by fire, a pleasing aroma. All fat is mine. Kuhani ataviteketeza juu ya madhabahu viwe chakula, sadaka iliyotolewa kwa moto, harufu nzuri. Mafuta yote ya mnyama ni ya Mwenyezi Mungu.
17 "This is a lasting rule for all generations, wherever you live: never eat any fat or any blood." “ ‘Hili ni agizo la kudumu kwa vizazi vijavyo, popote mnapoishi: Msile mafuta yoyote ya mnyama wala damu.’ ”
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]