Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

John 12 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 Six days before Passover, Jesus came to Bethany, where Lazarus, whom Jesus raised from death, lived. Siku sita kabla ya Pasaka, Isa alienda Bethania, makao ya Lazaro, aliyekuwa amemfufua kutoka kwa wafu.
2 There they gave him a dinner; Martha served, and Lazarus was one of those at the table with him. Wakaandaa karamu kwa heshima ya Isa. Martha akawahudumia, wakati Lazaro alikuwa miongoni mwa waliokaa mezani pamoja na Isa.
3 Mary took about a pint of pure nard perfume, expensive, and anointed Jesus' feet, then wiped his feet with her hair. The house filled with the fragrance of the perfume. Kisha Mariamu akachukua chupa ya painti moja yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa, akayamimina miguuni mwa Isa na kuifuta kwa nywele zake. Nyumba nzima ikajaa harufu nzuri ya manukato.
4 But Judas Iscariot, one of his disciples, the one who was about to betray him, said, Ndipo Yuda Iskariote mwana wa Simoni, mmoja wa wanafunzi wa Isa, ambaye baadaye angemsaliti Isa, akasema,
5 "Why was this perfume not sold for about a year's wages and given to the poor?" “Kwa nini manukato haya hayakuuzwa kwa dinari mia tatu, na fedha hizo wakapewa maskini?”
6 He said this not because he cared about the poor, but because he was a thief who kept the money box, taking what was put in it. Yuda hakusema hivi kwa kuwa aliwajali maskini, bali kwa kuwa alikuwa mwizi; ndiye alikuwa akitunza mfuko wa fedha, na akawa akiiba zile fedha.
7 So Jesus said, "Leave her alone. She has kept this for the day of my burial. Isa akasema, “Mwacheni. Aliyanunua manukato hayo ili ayaweke kwa ajili ya siku ya maziko yangu.
8 You will always have the poor among you, but you will not always have me." Maskini mtakuwa nao siku zote, lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.”
9 A large crowd of Jews learned Jesus was there and came, not only for him but to see Lazarus, whom he had raised from the dead. Umati mkubwa wa Wayahudi walipojua kwamba Isa alikuwa huko Bethania, walikuja si tu kwa ajili ya Isa, lakini pia kumwona Lazaro ambaye Isa alikuwa amemfufua.
10 So the chief priests planned to kill Lazarus as well, Kwa hiyo viongozi wa makuhani wakapanga njama ya kumuua Lazaro pia,
11 because on account of him many of the Jews were going over and believing in Jesus. kwa kuwa kutokana na habari za kufufuliwa kwake, Wayahudi wengi walikuwa wanamfuata Isa na kumwamini.
12 The next day, the large crowd that came for the feast heard Jesus was coming to Jerusalem. Siku iliyofuata umati mkubwa wa watu waliokuwa wamekuja kwenye Sikukuu walisikia kwamba Isa angekuja Yerusalemu.
13 They took palm branches and went out to meet him, shouting, "Hosanna! Blessed is he who comes in the name of our Father—the King of Israel!" Basi wakachukua matawi ya mitende, wakatoka kwenda kumlaki, huku wakipaza sauti wakisema, “Hosana!” “Amebarikiwa yeye ajaye kwa Jina la Mwenyezi Mungu!” “Amebarikiwa mfalme wa Israeli!”
14 Jesus found a young donkey and rode on it, just as it is written: Isa akamkuta mwana-punda, akampanda, kama ilivyoandikwa,
15 "Do not be afraid, daughter of Zion; look, your king is coming, seated on a donkey's colt." “Usiogope, ewe Binti Sayuni; tazama, mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda!”
16 His disciples didn't understand these things at first; but when Jesus was glorified, they remembered these things were written about him, and that they had done these things to him. Wanafunzi wake Isa mwanzoni hawakuelewa mambo haya. Lakini Isa alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka kuwa mambo haya yalikuwa yameandikwa kwa ajili yake na alitendewa yeye.
17 The crowd that was with him when he called Lazarus from the tomb and raised him from the dead kept testifying. Wale waliokuwepo Isa alipomwita Lazaro kutoka kaburini na kumfufua kutoka kwa wafu waliendelea kushuhudia.
18 The crowd went to meet him because they heard he had done this sign. Na kwa sababu walikuwa wamesikia kwamba alikuwa ametenda muujiza huu, umati wa watu wakaenda kumlaki.
19 So the Pharisees said to each other, "See, you're accomplishing nothing—the whole world has gone after him." Hivyo Mafarisayo walipoona hayo, wakaambiana, “Mnaona, hamwezi kufanya lolote. Angalieni, ulimwengu wote unamfuata yeye!”
20 Now there were some Greeks among those who went up to worship at the feast. Basi palikuwa Wayunani fulani miongoni mwa wale waliokuwa wameenda kuabudu wakati wa Sikukuu.
21 These came to Philip, from Bethsaida in Galilee, and asked him, "Sir, we want to see Jesus." Hawa wakaenda kwa Filipo, aliyekuwa raia wa Bethsaida huko Galilaya, wakiwa na ombi. Wakamwambia, “Tungependa kumwona Isa.”
22 Philip went and told Andrew; then Andrew and Philip went and told Jesus. Filipo akaenda akamweleza Andrea, nao wote wawili wakamwambia Isa.
23 Jesus replied to them, "The hour has come for the Son of Man to be glorified. Isa akawajibu, “Saa imewadia ya Mwana wa Adamu kutukuzwa.
24 Truly, truly, I tell you, unless a wheat grain falls to the ground and dies, it stays alone; but if it dies, it bears much fruit. Amin, amin nawaambia, mbegu ya ngano isipoanguka ardhini na kufa, hubakia kama mbegu peke yake. Lakini ikifa, huzaa mbegu nyingi.
25 Whoever loves his life loses it; whoever hates his life in this world keeps it for eternal life. Mtu yeyote anayependa maisha yake atayapoteza, naye ayachukiaye maisha yake katika ulimwengu huu atayaokoa hata kwa uzima wa milele.
26 Whoever serves me must follow me, so my servant will be where I am. Whoever serves me, my Father will honor him." Mtu yeyote akinitumikia lazima anifuate, nami mahali nilipo ndipo mtumishi wangu atakapokuwa. Mtu akinitumikia, Baba yangu atamheshimu.
27 "Now my soul is troubled. What should I say—'Father, save me from this hour'? But this is why I came to this hour. Father, glorify your name." “Sasa roho yangu imefadhaika sana. Niseme nini? ‘Baba, niokoe katika saa hii’? Lakini ni kwa kusudi hili nimeufikia wakati huu.
28 Then a voice came from heaven: "I have glorified it, and I will glorify it again." Baba, litukuze jina lako.” Ndipo ikaja sauti kutoka mbinguni, ikasema, “Nimelitukuza, nami nitalitukuza tena.”
29 The crowd standing there heard it and said it thundered; others said an angel spoke to him. Umati ule wa watu waliokuwa mahali pale waliisikia ile sauti, nao wakasema hiyo ilikuwa sauti ya radi; wengine wakasema malaika ameongea naye.
30 Jesus said, "This voice came for your sake, not mine. Isa akawaambia, “Sauti hii imesikika kwa faida yenu, wala si kwa faida yangu.
31 Now is the judgment of this world; now the ruler of this world will be cast out. Sasa ni saa ya hukumu kwa ajili ya ulimwengu huu, sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje.
32 And I, when I am lifted up from the earth, will draw all people to myself." Lakini mimi, nikiinuliwa kutoka nchi, nitawavuta watu wote waje kwangu.”
33 He said this to show by what kind of death he was going to die. Isa aliyasema haya akionesha ni kifo gani atakachokufa.
34 The crowd replied, "We've heard from the Law that the Christ stays forever. How can you say the Son of Man must be lifted up? Who is this Son of Man?" Umati ule wa watu wakapaza sauti, wakasema, “Tumesikia kutoka Torati kwamba Al-Masihi adumu milele; hivyo wewe wawezaje kusema, ‘Mwana wa Adamu hana budi kuinuliwa juu’? Huyu ‘Mwana wa Adamu’ ni nani?”
35 So Jesus said, "The light is with you a little while longer. Walk while you have light, so darkness doesn't overtake you. Whoever walks in darkness doesn't know where he's going. Ndipo Isa akawaambia, “Bado kitambo kidogo nuru ingali pamoja nanyi. Nendeni maadamu mna nuru, msije mkakumbwa na giza. Mtu anayetembea gizani hajui anakoenda.
36 While you have light, believe in the light, so you become children of light." Having said this, Jesus left and hid from them. Wekeni tumaini lenu katika nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru.” Baada ya kusema haya, Isa aliondoka, akajificha wasimwone.
37 Though he had performed so many signs in their presence, they still would not believe in him, Hata baada ya Isa kufanya miujiza hii yote mbele yao, bado hawakumwamini.
38 so that the word of Isaiah the prophet would be fulfilled, which he spoke: "Father, who has believed our message? And to whom has the arm of our Father been revealed?" Hili lilikuwa ili kutimiza lile neno la nabii Isaya lililosema: “Mwenyezi Mungu, ni nani aliyeamini ujumbe wetu, na mkono wa Mwenyezi Mungu umefunuliwa kwa nani?”
39 This is why they could not believe, for Isaiah said again: Kwa hivyo hawakuamini, kwa sababu Isaya anasema mahali pengine:
40 "He has blinded their eyes and hardened their heart, so that they would not see with their eyes, nor understand with their heart, nor turn—and I would heal them." “Amewafanya vipofu, na kuifanya mioyo yao kuwa migumu, ili wasiweze kuona kwa macho yao, wala kuelewa kwa mioyo yao, wasije wakageuka nami nikawaponya.”
41 Isaiah said these things because he saw Jesus' glory and spoke about him. Isaya alisema haya alipoona utukufu wa Isa na kunena habari zake.
42 Still, many even of the rulers believed in him, but they didn't admit it because of the Pharisees, so they wouldn't be expelled from the synagogue, Lakini wengi miongoni mwa viongozi wa Wayahudi walimwamini, lakini kwa sababu ya Mafarisayo hawakukiri waziwazi kwa maana waliogopa kufukuzwa katika masinagogi.
43 for they loved the glory that comes from people more than the glory that comes from our Father. Wao walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zinazotoka kwa Mungu.
44 Jesus cried out, "Whoever believes in me does not believe in me only, but in the one who sent me. Isa akapaza sauti akasema, “Yeyote aniaminiye, haniamini mimi peke yangu, bali pia yeye aliyenituma.
45 And whoever sees me sees the one who sent me. Yeyote anionaye mimi amemwona yeye aliyenituma.
46 I came into the world as light, so no one who believes in me stays in the darkness. Mimi nimekuja kama nuru ulimwenguni, ili kila mtu aniaminiye asibaki gizani.
47 If anyone hears my words and doesn't keep them, I don't judge him—I didn't come to judge the world, but to save the world. “Mimi simhukumu mtu yeyote anayesikia maneno yangu na asiyatii, kwa maana sikuja kuuhukumu ulimwengu, bali kuuokoa.
48 Whoever rejects me and doesn't accept my words already has a judge: my spoken word will judge him on the last day. Yuko anayehukumu yule anayenikataa mimi na kuyakataa maneno yangu; yale maneno niliyoyasema yenyewe yatamhukumu siku ya mwisho.
49 I have not spoken on my own; but the Father who sent me himself commanded me what to say and how to speak. Kwa maana sisemi kwa ajili yangu mwenyewe, bali Baba aliyenituma aliniamuru ni nini cha kusema na jinsi ya kukisema.
50 I know his commandment is eternal life, so I say only what the Father told me to say." Nami ninajua amri zake huongoza hadi kwenye uzima wa milele. Hivyo lolote nisemalo, ndilo lile Baba aliloniambia niseme.”
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]