Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Numbers 3 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 This is the family line of Aaron and Moses, when our Father spoke with Moses on Mount Sinai. Hivi ndivyo vizazi vya Haruni na Musa kwa wakati ambao Mwenyezi Mungu alizungumza na Musa katika Mlima Sinai.
2 These are the names of the sons of Aaron: Nadab the firstborn, then Abihu, Eleazar, and Ithamar. Majina ya wana wa Haruni yalikuwa: Nadabu mzaliwa wa kwanza na Abihu, Eleazari na Ithamari.
3 These are the names of Aaron's sons, the anointed priests whom Moses ordained to serve as priests. Hayo yalikuwa majina ya wana wa Haruni, makuhani wapakwa mafuta, waliokuwa wamesimikwa kuhudumu kama makuhani.
4 Nadab and Abihu died before our Father in the wilderness of Sinai when they offered unauthorized fire before him; they had no children. So Eleazar and Ithamar served as priests before Aaron their father. Hata hivyo Nadabu na Abihu walikufa mbele za Mwenyezi Mungu walipotoa sadaka kwa moto usioruhusiwa mbele zake katika Jangwa la Sinai. Hawakuwa na wana; kwa hiyo Eleazari na Ithamari walihudumu peke yao kama makuhani wakati wote wa maisha ya Haruni baba yao.
5 Then our Father said to Moses: Mwenyezi Mungu akamwambia Musa,
6 "Bring the tribe of Levi near and set them before Aaron the priest, to serve him. “Walete kabila la Lawi mbele ya Haruni kuhani ili wamsaidie.
7 They are to keep his duties and those of the whole community before the tent of meeting, performing the tabernacle's service. Watafanya huduma kwa ajili yake na kwa jumuiya yote katika Hema la Kukutania kwa kufanya kazi za Maskani.
8 They are to guard all the tent of meeting's equipment and the Israelites' duty, doing the tabernacle's service. Watatunza samani zote za Hema la Kukutania, wakitimiza wajibu wa kuhudumia Waisraeli kwa kufanya kazi ya Maskani.
9 Give the Levites to Aaron and his sons; they are given entirely to him from among Israel's people. Wakabidhi Walawi kwa Haruni na wanawe; hao ndio Waisraeli ambao wanakabidhiwa kwake kabisa.
10 Appoint Aaron and his sons to guard their priesthood; any outsider who comes near must die." Waweke Haruni na wanawe kuhudumu kama makuhani; mtu mwingine yeyote atakayesogea mahali patakatifu atauawa.”
11 Then our Father said to Moses: Mwenyezi Mungu akamwambia Musa,
12 "Look, I have taken the Levites from among the Israelites in place of every firstborn that opens the womb among the Israelites. The Levites are mine. “Nimewatwaa Walawi kutoka miongoni mwa Waisraeli badala ya mzaliwa wa kwanza wa kiume wa kila mwanamke wa Mwisraeli. Walawi ni wangu,
13 Every firstborn is mine. The day I struck down every firstborn in Egypt, I set apart for myself every firstborn in Israel—both man and animal. They will be mine. I am your Father." kwa kuwa wazaliwa wote wa kwanza ni wangu. Nilipowaua wazaliwa wa kwanza huko Misri, nilimtenga kila mzaliwa wa kwanza katika Israeli awe wangu, akiwa mwanadamu au mnyama. Watakuwa wangu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.”
14 Then our Father spoke to Moses in the wilderness of Sinai: Mwenyezi Mungu akamwambia Musa katika Jangwa la Sinai,
15 "Count Levi's sons by fathers' houses and clans; count every male a month old and up." “Wahesabu Walawi kwa jamaa zao na koo zao. Mhesabu kila mwanaume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi.”
16 So Moses counted them at the word of our Father, just as he had been commanded. Kwa hiyo Musa akawahesabu, kama alivyoamriwa na neno la Mwenyezi Mungu.
17 These were the sons of Levi by their names: Gershon, Kohath, and Merari. Haya yalikuwa majina ya wana wa Lawi: Gershoni, Kohathi na Merari.
18 These are the names of the sons of Gershon by their clans: Libni and Shimei. Haya ndio yaliyokuwa majina ya koo za Wagershoni: Libni na Shimei.
19 The sons of Kohath by their clans: Amram, Izhar, Hebron, and Uzziel. Koo za Wakohathi zilikuwa ni: Amramu, Ishari, Hebroni na Uzieli.
20 Merari's sons by clan: Mahli and Mushi. These are the Levite clans by fathers' houses. Koo za Wamerari zilikuwa ni: Mahli na Mushi. Hizo zilikuwa koo za Walawi, kufuatana na jamaa zao.
21 From Gershon: the Libnite clan and the Shimeite clan—these are the Gershonite clans. Kulikuwa na koo za Walibni na Washimei kwa Gershoni; hizo zilikuwa koo za Wagershoni.
22 The number of males counted, a month old or older, was 7,500. Idadi ya wanaume wote wa umri wa mwezi mmoja au zaidi waliohesabiwa walikuwa elfu saba na mia tano.
23 The clans of the Gershonites camped behind the tabernacle on the west. Ukoo wa Wagershoni walitakiwa kuweka kambi zao upande wa magharibi, nyuma ya Maskani.
24 The leader of the fathers' house of the Gershonites was Eliasaph son of Lael. Kiongozi wa jamaa za Wagershoni alikuwa Eliasafu mwana wa Laeli.
25 Gershon's sons at the tent of meeting cared for the tabernacle, the tent, its covering, and the entrance screen of the tent of meeting. Katika Hema la Kukutania, Wagershoni walikuwa na wajibu wa kutunza Maskani na hema, vifuniko vyake, pazia katika mlango wa kuingilia ndani ya Hema la Kukutania,
26 The courtyard's curtains and its entrance screen, surrounding the tabernacle and altar, and its cords for all its service. mapazia ya ua, pazia katika ingilio la ua unaozunguka Maskani na madhabahu, pamoja na kamba, na kila kinachohusika kwa matumizi yake.
27 From Kohath came the Amramite clan, the Izharite clan, the Hebronite clan, and the Uzzielite clan; these are the clans of the Kohathites. Kwa Kohathi kulikuwa koo za Waamrami, Waishari, Wahebroni na Wauzieli; hizo zilikuwa koo za Wakohathi.
28 Males a month old and up numbered 8,600, in charge of the sanctuary. Hesabu ya wanaume wote wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi, walikuwa elfu nane na mia sita. Wakohathi waliwajibika kutunza mahali patakatifu.
29 The clans of the sons of Kohath camped on the south side of the tabernacle. Koo za Wakohathi zilitakiwa kuweka kambi zao upande wa kusini wa Maskani.
30 The leader of the fathers' house of the Kohathite clans was Elizaphan son of Uzziel. Kiongozi wa jamaa za koo za Wakohathi alikuwa Elisafani mwana wa Uzieli.
31 They cared for the ark, the table, the lampstand, the altars, the sanctuary vessels used in service, the screen, and all its work. Waliwajibika kutunza Sanduku la Agano, meza, kinara cha taa, madhabahu, na vile vyombo vya mahali patakatifu vinavyotumika kuhudumu, pazia, na kila kitu kinachohusika na matumizi yake.
32 Eleazar son of Aaron the priest was chief leader of the Levites, in charge of those guarding the sanctuary. Kiongozi mkuu wa Walawi alikuwa Eleazari mwana wa kuhani, Haruni. Aliwekwa juu ya wale waliowajibika kutunza mahali patakatifu.
33 From Merari: the Mahlite clan and the Mushite clan—these are Merari's clans. Kwa Merari kulikuwa na koo za Wamahli na Wamushi; hizi zilikuwa koo za Merari.
34 The number of males counted, a month old or older, was 6,200. Hesabu ya wanaume wote wenye umri wa mwaka mmoja au zaidi waliohesabiwa, walikuwa elfu sita na mia mbili.
35 Leader of Merarite clans' ancestral house: Zuriel son of Abihail; they camped on the tabernacle's north side. Kiongozi wa jamaa za koo za Wamerari alikuwa Surieli mwana wa Abihaili. Hawa walitakiwa kuweka kambi zao upande wa kaskazini mwa Maskani.
36 Merari's sons were charged with the tabernacle's frames, crossbars, posts, bases, all its equipment, and all its service, Wamerari waliwekwa kutunza miimo ya Maskani, mataruma yake, nguzo, vitako na vifaa vyake vyote na kila kitu kilichohusika na matumizi yake,
37 as well as the posts of the surrounding courtyard with their bases, pegs, and cords. na pia nguzo za ua unaozunguka pamoja na vitako vyake, vigingi vya hema na kamba zake.
38 Camped east of the tabernacle, in front of the tent of meeting toward sunrise, were Moses, Aaron, and his sons, who kept charge of the sanctuary for the Israelites; any outsider who approached was to be put to death. Musa, na Haruni na wanawe walitakiwa kuweka kambi zao mashariki mwa Maskani, kuelekea mawio ya jua, mbele ya Hema la Kukutania. Wao walihusika na utunzaji wa mahali patakatifu kwa niaba ya Waisraeli. Mtu mwingine yeyote aliyepasogelea mahali patakatifu angeuawa.
39 All the Levites whom Moses and Aaron counted at our Father's command, by their clans, every male a month old and up: 22,000. Jumla ya hesabu ya Walawi waliohesabiwa na Musa na Haruni kwa amri ya Mwenyezi Mungu, kufuatana na koo zao, pamoja na kila mwanaume mwenye umri wa mwezi mmoja au zaidi, walikuwa elfu ishirini na mbili.
40 Then our Father said to Moses, "Count every firstborn male of Israel a month old or older, and record the number of their names. Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, “Wahesabu wazaliwa wa kwanza wa kiume wote wa Waisraeli wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi na uorodheshe majina yao.
41 Take the Levites for me—I am your Father—in place of every firstborn among the people of Israel, and the Levites' livestock in place of every firstborn among Israel's livestock." Nitwalie Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya wazaliwa wa mifugo ya Waisraeli. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.”
42 So Moses counted every firstborn among the people of Israel, just as our Father had commanded him. Hivyo Musa akawahesabu wazaliwa wa kwanza wote wa Waisraeli, kama Mwenyezi Mungu alivyomwamuru.
43 All firstborn males, a month or older, listed by name: 22,273. Jumla ya hesabu ya wazaliwa wa kwanza wanaume wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi, walioorodheshwa kwa majina, walikuwa elfu ishirini na mbili na mia mbili na sabini na watatu (22,273).
44 Then our Father spoke to Moses: Mwenyezi Mungu akamwambia Musa,
45 "Take the Levites instead of every firstborn among Israel's people, and the Levites' livestock instead of theirs. The Levites will be mine. I am your Father. “Watwae Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli, nayo mifugo ya Walawi badala ya mifugo yao. Walawi watakuwa wangu. Mimi ndimi Mwenyezi Mungu.
46 To redeem the 273 firstborn Israelites exceeding the Levites' count. Ili kukomboa wazaliwa wa kwanza mia mbili na sabini na watatu (273) wa Waisraeli ambao wamezidi hesabu ya Walawi,
47 Collect about 2 ounces per person, by sanctuary standard (each measure about half an ounce of silver). kusanya shekeli tano kwa kila mmoja, kufuatana na shekeli ya mahali patakatifu, ambayo ina uzito wa gera ishirini.
48 Give the money to Aaron and his sons as the redemption price for the extra firstborn sons." Mpe Haruni na wanawe hizo fedha kwa ajili ya ukombozi wa idadi ya Waisraeli waliozidi.”
49 So Moses collected the redemption money from the firstborn sons who exceeded the number of the Levites; Kwa hiyo Musa akakusanya fedha za ukombozi kutoka kwa wale ambao hesabu yao ilizidi wale waliokombolewa na Walawi.
50 from Israel's firstborn sons he took 1,365—about 2 ounces, by the sanctuary standard. Kutokana na wazaliwa wa kwanza wa Waisraeli alikusanya fedha yenye uzito wa shekeli elfu moja na mia tatu sitini na tano (1,365) kufuatana na shekeli ya mahali patakatifu.
51 Moses gave the redemption money to Aaron and his sons, by our Father's word, just as our Father commanded Moses. Musa akampa Haruni na wanawe ile fedha ya ukombozi, kama alivyoamriwa na neno la Mwenyezi Mungu.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]