Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Mark 1 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 The beginning of the gospel of Jesus Christ, the Son of our Father. Mwanzo wa Injili ya Isa Al-Masihi, Mwana wa Mungu,
2 As written in Isaiah the prophet: "Look, I send my messenger ahead of you, who will prepare your way. kama ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: “Tazama, nitamtuma mjumbe wangu mbele yako, atakayetengeneza njia mbele yako”:
3 A voice calling out in the wilderness: 'Prepare the way of the Lord, make his paths straight.'" “sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Itengenezeni njia ya Mwenyezi Mungu, yanyoosheni mapito yake.’ ”
4 John appeared, baptizing in the wilderness and proclaiming a baptism of repentance for the forgiveness of sins. Yahya alikuja akibatiza huko nyikani, akihubiri ubatizo wa toba kwa ajili ya msamaha wa dhambi.
5 All Judea and everyone in Jerusalem went out to him, and he baptized them in the Jordan River as they confessed their sins. Watu kutoka Yudea yote na sehemu zote za Yerusalemu walikuwa wakimwendea. Nao wakaziungama dhambi zao, akawabatiza katika Mto Yordani.
6 John was dressed in camel's hair, with a leather belt around his waist, eating locusts and wild honey. Yahya alivaa mavazi yaliyotengenezwa kwa singa za ngamia na mkanda wa ngozi kiunoni mwake. Alikula nzige na asali ya mwitu.
7 He announced: "After me comes one stronger than I; I'm not worthy to stoop and untie his sandal strap. Naye alihubiri akisema, “Baada yangu atakuja yeye aliye na uwezo kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuinama na kulegeza kamba za viatu vyake.
8 I have baptized you with water, but he will baptize you with the Holy Spirit." Mimi nawabatiza kwa maji, lakini yeye atawabatiza kwa Roho wa Mungu.”
9 In those days Jesus came from Nazareth of Galilee and was baptized by John in the Jordan. Wakati huo Isa akaja kutoka Nasiri ya Galilaya, naye akabatizwa na Yahya katika Mto Yordani.
10 Immediately, as he came up out of the water, he saw the heavens split open and the Holy Spirit come down on him like a dove. Isa alipokuwa akitoka ndani ya maji, aliona mbingu zikifunguka na Roho wa Mungu akishuka juu yake kama hua.
11 And a voice came from heaven: "You are my beloved Son; in you I delight." Nayo sauti kutoka mbinguni ikasema, “Wewe ni Mwanangu mpendwa; nami nimependezwa nawe sana.”
12 And immediately the Holy Spirit drove him out into the wilderness. Wakati huo huo, Roho wa Mungu akamwongoza Isa hadi nyikani,
13 He was in the wilderness forty days, tempted by Satan, with the wild animals, and the angels served him. naye Isa akawa huko nyikani kwa muda wa siku arobaini, akijaribiwa na Shetani. Alikaa na wanyama pori, nao malaika wakamhudumia.
14 Now after John was arrested, Jesus came into Galilee, proclaiming the gospel of our Father, Baada ya Yahya kutiwa gerezani, Isa alienda Galilaya, akaanza kuhubiri Injili ya Mungu,
15 and saying, "The time is fulfilled, and our Father's kingdom is near; repent and believe the good news." akisema, “Wakati umetimia, ufalme wa Mungu umekaribia. Tubuni na kuiamini Injili.”
16 Passing the Sea of Galilee, he saw Simon and his brother Andrew casting a net in the sea, for they were fishermen. Isa alipokuwa akitembea kando ya Bahari ya Galilaya, aliwaona Simoni na Andrea nduguye wakizitupa nyavu zao baharini, kwa kuwa walikuwa wavuvi.
17 And Jesus said to them, "Follow me, and I will make you become fishers of people." Isa akawaambia, “Njooni, nifuateni nami nitawafanya mwe wavuvi wa watu.”
18 And immediately they left their nets and followed him. Mara wakaacha nyavu zao, wakamfuata.
19 Going a little farther, he saw James son of Zebedee and John his brother in their boat, mending the nets. Alipoenda mbele kidogo, akamwona Yakobo mwana wa Zebedayo na Yohana nduguye, wakiwa kwenye mashua yao wakizitengeneza nyavu zao.
20 At once he called them; leaving their father Zebedee in the boat with the hired hands, they followed him. Papo hapo akawaita, nao wakamwacha Zebedayo baba yao kwenye mashua pamoja na watumishi wa kuajiriwa, nao wakamfuata Isa.
21 They went to Capernaum. At once, on the Sabbath, he entered the synagogue and began teaching. Wakaenda hadi Kapernaumu. Mara ilipofika siku ya Sabato, Isa akaingia sinagogi, akaanza kufundisha.
22 They were amazed at his teaching, for he taught them with authority, not like the scribes. Watu wakashangaa sana kwa mafundisho yake, kwa maana alikuwa akiwafundisha kama mtu mwenye mamlaka, wala si kama walimu wa Torati.
23 And immediately there was in their synagogue a man with an unclean spirit, and he cried out. Wakati huo huo katika sinagogi lao palikuwa na mtu aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu, naye akapaza sauti akisema,
24 Why meddle with us, Jesus of Nazareth? Have you come to destroy us? I know who you are—God's Holy One! “Tuna nini nawe, Isa Al-Nasiri? Je, umekuja kutuangamiza? Ninakujua wewe ni nani. Wewe ndiwe Aliye Mtakatifu wa Mungu!”
25 But Jesus rebuked him, saying, "Be silent, and come out of him!" Lakini Isa akamkemea, akamwamuru, “Nyamaza! Mtoke mtu huyu!”
26 And the unclean spirit, convulsing him and crying out with a loud voice, came out of him. Yule pepo mchafu akamgaragaza huyo mtu kwa nguvu, kisha akamtoka akipiga kelele kwa sauti kubwa.
27 All were amazed, and they questioned each other: "What is this? A new teaching with authority - he commands even the unclean spirits, and they obey him!" Watu wote wakashangaa, hata wakaulizana wao kwa wao, “Haya ni mambo gani? Ni mafundisho mapya, tena yenye mamlaka! Anaamuru hata pepo wachafu, nao wanamtii!”
28 And at once his fame spread everywhere throughout all the surrounding region of Galilee. Sifa zake zikaanza kuenea haraka katika eneo lote la karibu na Galilaya.
29 Immediately he left the synagogue and went to Simon and Andrew's house, with James and John. Mara walipotoka katika sinagogi, walienda pamoja na Yakobo na Yohana hadi nyumbani mwa Simoni na Andrea.
30 Now Simon's mother-in-law lay sick with a fever, and immediately they told him about her. Mama mkwe wa Simoni alikuwa kitandani, ana homa, nao wakamweleza Isa habari zake.
31 He came, took her hand, raised her up. The fever left her, and she served them. Hivyo Isa akamwendea, akamshika mkono na kumwinua. Kisha homa ikamwacha, naye akaanza kuwahudumia.
32 That evening, when the sun set, they brought him all who were sick and those oppressed by demons. Jioni ile baada ya jua kutua, watu wakamletea Isa wagonjwa wote na waliopagawa na pepo wachafu.
33 And the whole city was gathered together at the door. Mji wote ukakusanyika mbele ya nyumba hiyo.
34 He healed many sick with various diseases and drove out many demons, not letting the demons speak, since they knew him. Isa akawaponya watu wengi waliokuwa na magonjwa ya aina mbalimbali. Akawatoa pepo wachafu wengi, lakini hakuwaacha hao pepo wachafu waseme, kwa sababu walimjua yeye ni nani.
35 Long before dawn, while still dark, he got up, went out to a deserted place, and prayed there. Alfajiri na mapema sana kulipokuwa bado kuna giza, Isa akaamka, akaondoka, akaenda mahali pa faragha ili kuomba.
36 And Simon and those who were with him searched for him, Simoni na wenzake wakaenda kumtafuta,
37 and they found him and said to him, "Everyone is looking for you." nao walipomwona, wakapaza sauti, wakasema, “Kila mtu anakutafuta!”
38 He said, "Let us go elsewhere, to the neighboring towns, so I can preach there too, for that is why I came." Isa akawajibu, “Twendeni mahali pengine, kwenye vijiji jirani, ili niweze kuhubiri huko pia. Maana nilikuja kwa kusudi hili.”
39 And he went throughout all Galilee, preaching in their synagogues and casting out demons. Kwa hiyo akazunguka Galilaya yote, akihubiri katika masinagogi yao na kutoa pepo wachafu.
40 A man with leprosy came, knelt, and begged him, "If you're willing, you can make me clean." Mtu mmoja mwenye ukoma alimjia Isa, akapiga magoti, akimwomba, “Ukitaka, unaweza kunitakasa.”
41 Moved with deep compassion, he stretched out his hand, touched him, and said to him, "I am willing; be clean." Isa, akiwa amejawa na huruma, akaunyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Nataka. Takasika!”
42 And immediately the leprosy left him, and he was made clean. Mara ukoma ukamtoka, naye akatakasika.
43 Sternly warning him, he sent him away at once, Baada ya Isa kumwonya vikali, akamruhusu aende zake mara moja;
44 and told him, "Make sure you tell no one—but go, show yourself to the priest, and offer what Moses commanded for your cleansing, as proof to the people." akamwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote habari hizi, bali nenda ukajioneshe kwa kuhani, na ukatoe sadaka alizoagiza Musa kwa utakaso wako, ili kuwa ushuhuda kwao.”
45 But he went out, proclaiming it freely and spreading the news, so Jesus could no longer enter a town openly, but stayed in lonely places. Yet people came to him from everywhere. Lakini yule mtu akaenda akaanza kutangaza habari za kuponywa kwake waziwazi. Kwa hiyo, Isa hakuweza tena kuingia katika miji waziwazi bali alikaa sehemu zisizo na watu. Hata hivyo watu wakamfuata huko kutoka kila upande.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]