Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

John 1 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 In the beginning was the Word, and the Word was with our Father, and the Word was God. Hapo mwanzo alikuwako Neno, naye huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 He was in the beginning with our Father. Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na Mungu.
3 All things were made through him, and without him not one thing was made that was made. Vitu vyote viliumbwa kupitia kwake, na hakuna chochote kilichoumbwa ambacho kimeumbwa pasipo yeye.
4 In him was life, and the life was the light of all people. Ndani yake kulikuwa na uzima, nao huo uzima ulikuwa nuru ya watu.
5 The light shines in the darkness, and the darkness has not overcome it. Nuru hung’aa gizani nalo giza halikuishinda.
6 There came a man sent from our Father, whose name was John. Alikuja mtu mmoja aliyetumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yahya.
7 He came as a witness, to bear witness about the light, so that all might believe through John's witness. Alikuja kama shahidi apate kuishuhudia hiyo nuru, ili kupitia kwake watu wote waweze kuamini.
8 He was not the light, but came to bear witness about the light. Yeye mwenyewe hakuwa ile nuru, bali alikuja kuishuhudia hiyo nuru.
9 The true light, which gives light to everyone, was coming into the world. Nuru halisi inayomwangazia kila mtu ilikuwa inakuja ulimwenguni.
10 He was in the world. The world came into being through him, yet did not know him. Huyo Neno alikuwako ulimwenguni, na ingawa ulimwengu uliumbwa kupitia kwake, haukumtambua.
11 He came to his own, and his own people did not receive him. Alikuja kwa walio wake, lakini wao hawakumpokea.
12 But to all who received him, believing in his name, he gave the right to become children of our Father, Bali wote waliompokea, yaani wale walioliamini jina lake, aliwapa uwezo wa kufanyika wana wa Mungu.
13 children born not of blood nor of the will of flesh nor of the will of man, but of our Father. Hawa hawakuzaliwa kwa damu, wala kwa mapenzi ya mwili au kwa mapenzi ya mtu, bali wamezaliwa kwa mapenzi ya Mungu.
14 The Word became flesh and lived among us. We saw his glory, the glory of the one and only Son from the Father, full of grace and truth. Neno alifanyika mwili, akakaa miongoni mwetu, nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba, amejaa neema na kweli.
15 John testified about him, crying out, "This is the one I meant: he who comes after me outranks me, since he existed before me." Yahya alishuhudia habari zake, akapaza sauti, akisema, “Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Yeye ajaye baada yangu ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa alikuwa kabla yangu.’ ”
16 For from his fullness we have all received, grace upon grace. Kutokana na ukamilifu wake, sisi sote tumepokea neema juu ya neema.
17 For the law was given through Moses; grace and truth came through Jesus Christ. Kwa kuwa sheria ilitolewa kwa mkono wa Musa, lakini neema na kweli zimekuja kupitia Isa Al-Masihi.
18 No one has ever seen our Father; the one and only God, close beside the Father, has made him known. Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote, ila ni Mungu Mwana pekee, aliye kifuani mwa Baba, ndiye ambaye amemdhihirisha.
19 This is John's testimony, when the Jews sent priests and Levites from Jerusalem to ask him, "Who are you?" Huu ndio ushuhuda wa Yahya wakati viongozi wa Wayahudi waliwatuma makuhani na Walawi kutoka Yerusalemu kumuuliza, “Wewe ni nani?”
20 He confessed, and did not deny, but confessed, "I am not the Christ." Yahya alikiri waziwazi pasipo kuficha, akasema, “Mimi si Al-Masihi.”
21 So they asked him, "What then? Are you Elijah?" "I am not," he said. "Are you the Prophet?" "No," he answered. Wakamuuliza, “Wewe ni nani, basi? Je, wewe ni Ilya?” Yeye akajibu, “Hapana, mimi siye.” “Je, wewe ni yule Nabii?” Akajibu, “Hapana.”
22 So they asked, "Who are you? We need to give an answer to those who sent us. What do you say about yourself?" Ndipo wakasema, “Basi tuambie wewe ni nani ili tupate jibu la kuwapelekea wale waliotutuma. Wewe wasemaje juu yako mwenyewe?”
23 He said, "I'm the voice of one crying out in the wilderness, 'Make straight the way of the Lord,' as the prophet Isaiah said." Akawajibu kwa maneno ya nabii Isaya, akisema, “Mimi ni sauti ya mtu aliaye nyikani, ‘Yanyoosheni mapito ya Mwenyezi Mungu.’ ”
24 Now they had been sent from the Pharisees. Basi walikuwa wametumwa watu kutoka kwa Mafarisayo,
25 They asked him, "Why baptize, then, if you're not the Christ, nor Elijah, nor the Prophet?" wakamuuliza, “Kama wewe si Al-Masihi, wala si Ilya na wala si yule Nabii, kwa nini basi unabatiza?”
26 John answered them, "I baptize with water, but among you stands one you do not know, Yahya akawajibu, “Mimi ninabatiza kwa maji, lakini kati yenu yupo mtu msiyemjua.
27 even he who comes after me, whose sandal strap I am not worthy to untie." Yeye anakuja baada yangu, nami sistahili hata kufungua kamba za viatu vyake.”
28 These things took place in Bethany across the Jordan, where John was baptizing. Mambo haya yote yalitukia huko Bethania, ng’ambo ya Yordani, mahali Yahya alipokuwa akibatiza.
29 The next day, seeing Jesus coming toward him, he said, "Look! The Lamb of our Father—Jesus—who takes away the sin of the world! Siku iliyofuata, Yahya alimwona Isa akimjia, akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!
30 This is the one I meant: 'After me comes a man who ranks before me, because he was before me.' Huyu ndiye yule niliyewaambia kwamba, ‘Mtu anakuja baada yangu ambaye ni mkuu kuliko mimi, kwa kuwa alikuwa kabla yangu.’
31 I didn't know him, but I came baptizing with water so he would be revealed to Israel." Mimi mwenyewe sikumfahamu, lakini sababu ya kuja nikibatiza kwa maji ni ili yeye apate kufunuliwa kwa Israeli.”
32 John testified: "I saw the Holy Spirit descend from heaven like a dove and remain on him. Kisha Yahya akatoa ushuhuda huu: “Nilimwona Roho Mtakatifu wa Mungu akishuka kutoka mbinguni kama hua, akakaa juu yake.
33 I didn't know him, but the one who sent me to baptize with water told me, 'The one you see the Holy Spirit come down and stay on—he is the one who baptizes with the Holy Spirit.' Mimi nisingemtambua, lakini yeye aliyenituma nibatize kwa maji alikuwa ameniambia, ‘Yule mtu utakayemwona Roho Mtakatifu wa Mungu akimshukia na kukaa juu yake, huyo ndiye atakayebatiza kwa Roho wa Mungu.’
34 And I have seen and have borne witness that this is the Son of our Father." Mimi mwenyewe nimeona jambo hili na ninashuhudia kuwa huyu ndiye Mwana wa Mungu.”
35 The next day John was standing again with two of his disciples, Siku iliyofuata, Yahya alikuwa huko tena pamoja na wanafunzi wake wawili.
36 and looking at Jesus as he walked by, he said, "Look! The Lamb of our Father!" Alipomwona Isa akipita, akasema, “Tazama, Mwana-Kondoo wa Mungu!”
37 The two disciples heard him say this, and they followed Jesus. Wale wanafunzi wawili walipomsikia Yahya akisema haya, wakamfuata Isa.
38 Jesus turned, saw them following, and asked, "What do you seek?" They said, "Rabbi" (meaning Teacher), "where do you stay?" Isa akageuka, akawaona wakimfuata, akawauliza, “Mnataka nini?” Wakamwambia, “Mwalimu, unaishi wapi?”
39 He told them, "Come and you will see." So they went and saw where he was staying, and remained with him that day—about four in the afternoon. Isa akawajibu, “Njooni, nanyi mtapaona!” Hivyo wakaenda na kupaona mahali alipokuwa anaishi, wakakaa naye siku ile, kwa kuwa ilikuwa yapata saa kumi.
40 One of the two who heard John speak and followed Jesus was Andrew, Simon Peter's brother. Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliosikia yale Yahya alisema na kumfuata Isa.
41 He first found his own brother Simon and told him, "We've found the Messiah" (meaning Christ). Kitu cha kwanza Andrea alichofanya ni kumtafuta Simoni nduguye na kumwambia, “Tumemwona Masihi” (yaani Al-Masihi).
42 He brought him to Jesus. Jesus looked at him and said, "You are Simon the son of John. You will be called Cephas" (meaning Peter). Naye akamleta kwa Isa. Isa akamwangalia na kusema, “Wewe ni Simoni mwana wa Yohana. Utaitwa Kefa” (ambalo limetafsiriwa Petro).
43 The next day, Jesus decided to leave for Galilee. He found Philip and said, "Follow me." Siku iliyofuata Isa aliamua kwenda Galilaya. Akamkuta Filipo, akamwambia, “Nifuate.”
44 Now Philip was from Bethsaida, the city of Andrew and Peter. Filipo alikuwa raia wa Bethsaida, mji walikotoka Andrea na Petro.
45 Philip found Nathanael and told him, "We've found the one Moses wrote of in the Law and the prophets—Jesus, son of Joseph, from Nazareth." Filipo naye akamkuta Nathanaeli na kumwambia, “Tumemwona yeye ambaye Musa aliandika habari zake katika Torati, na ambaye pia manabii waliandika kumhusu, yaani Isa Al-Nasiri, mwana wa Yusufu.”
46 Nathanael said, "Can anything good come from Nazareth?" Philip said, "Come and see." Nathanaeli akauliza, “Nasiri! Je, kitu chochote chema chaweza kutoka Nasiri?” Filipo akamwambia, “Njoo uone.”
47 Jesus saw Nathanael approaching and said of him, "Look—a true Israelite, with no deceit in him!" Isa alipomwona Nathanaeli anakaribia, akanena habari zake, akasema, “Tazama huyu ni Mwisraeli kweli kweli; hana hila ndani yake.”
48 Nathanael asked him, "How do you know me?" Jesus answered, "Before Philip called you, while you were under the fig tree, I saw you." Nathanaeli akamuuliza, “Umenifahamuje?” Isa akamjibu, “Nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini, kabla hata Filipo hajakuita.”
49 Nathanael answered him, "Rabbi, you are the Son of our Father! You are the King of Israel!" Nathanaeli akamwambia, “Mwalimu, wewe ni Mwana wa Mungu! Wewe ni Mfalme wa Israeli!”
50 Jesus answered him, "You believe because I told you I saw you under the fig tree? You'll see greater things than these." Isa akamwambia, “Unaamini kwa kuwa nilikuambia nilikuona ulipokuwa bado uko chini ya mtini? Basi utaona mambo makuu kuliko hilo.”
51 He told him, "Truly, truly, I say to you, you will see heaven opened, and our Father's angels ascending and descending on the Son of Man." Ndipo akawaambia, “Amin, amin nawaambia, ninyi mtaona mbingu ikifunguka na malaika wa Mungu wakipanda na kushuka juu ya Mwana wa Adamu.”
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]