Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

James 3 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 My brothers and sisters, not many of you should become teachers, since we teachers face stricter judgment. Ndugu zangu, msiwe walimu wengi, kwa maana mnafahamu kwamba sisi tufundishao tutahukumiwa vikali zaidi.
2 For we all stumble in many ways. Anyone who never stumbles in speech is a mature man, able to control his whole body too. Sisi sote tunajikwaa katika mambo mengi. Ikiwa mtu yeyote hakosei kamwe katika yale anayosema, yeye ni mkamilifu, naye anaweza kuuzuia pia na mwili wake wote.
3 If we put bits in horses' mouths to make them obey us, we guide their whole bodies too. Tunapotia lijamu kwenye vinywa vya farasi ili kuwafanya watutii, tunaweza kuigeuza miili yao yote.
4 Consider ships too: though large and driven by strong winds, a tiny rudder steers them wherever the pilot wants. Au chukua mfano wa meli: ingawa ni kubwa sana, nazo hupelekwa na upepo mkali, zinaelekezwa kwa usukani mdogo sana kokote wanakotaka nahodha.
5 So too the tongue is a small body part, yet boasts great things. See how small a fire sets ablaze a great forest! Vivyo hivyo ulimi ni kiungo kidogo sana katika mwili, lakini hujivuna majivuno makuu. Fikirini jinsi moto mdogo unavyoweza kuteketeza msitu mkubwa!
6 The tongue is a fire, a world of wickedness placed among our body's parts. It stains the whole body, sets the whole course of life ablaze, and is itself set ablaze by hell. Ulimi pia ni moto, ndio ulimwengu wa uovu kati ya viungo vya mwili. Ulimi huutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa Jehanamu.
7 Every kind of beast, bird, reptile, and sea creature is tamed, and has been tamed, by humankind, Kwa maana kila aina ya wanyama, ndege, wanyama watambaao na viumbe vya baharini hufugika na hufugwa na binadamu,
8 but no human being can tame the tongue. It is a restless evil, full of deadly poison. lakini hakuna mtu awezaye kuufuga ulimi. Ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
9 With it we bless our Father; with it we curse people made in the likeness of our Father. Kwa ulimi tunamhimidi Mwenyezi Mungu na Baba yetu, na kwa huo twawalaani watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu.
10 From the same mouth come blessing and cursing. My brothers and sisters, this should not be. Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haistahili kuwa hivyo.
11 Does a spring pour out both fresh and bitter water from the same opening? Je, chemchemi moja inaweza kutoa katika tundu moja maji matamu na maji ya chumvi?
12 Brothers and sisters, can a fig tree bear olives, or a vine figs? Neither can a salt spring yield fresh water. Je, ndugu zangu, mtini unaweza kuzaa zeituni, au mzabibu kuzaa tini? Wala chemchemi ya maji ya chumvi haiwezi kutoa maji matamu.
13 Who is wise and understanding among you? Let him show his deeds through good conduct, in wisdom's humility. Ni nani aliye na hekima na ufahamu miongoni mwenu? Basi na aioneshe hiyo kwa maisha yake mema na kwa matendo yake yaliyotendwa kwa unyenyekevu utokanao na hekima.
14 But if bitter envy and selfish ambition fill your heart, don't boast or lie against the truth. Lakini ikiwa mna wivu na ni wenye chuki na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu kwa ajili ya hayo wala msiikatae kweli.
15 This is not the wisdom that comes down from above, but is earthly, unspiritual, demonic. Hekima kama hiyo haishuki kutoka mbinguni, bali ni ya kidunia, isiyo ya kiroho, na ya kishetani.
16 For where there is jealousy and selfish ambition, there will be disorder and every vile practice. Kwa maana panapokuwa na wivu na ubinafsi, ndipo penye machafuko na uovu wa kila namna.
17 Wisdom from above: pure first, then peace-loving, gentle, reasonable, full of mercy and good fruit, unbiased, sincere. Lakini hekima inayotoka mbinguni kwanza ni safi, kisha inapenda amani, tena ni ya upole, iliyo tayari kusikiliza wengine kwa unyenyekevu, iliyojaa huruma na matunda mema, isiyopendelea mtu, tena isiyokuwa na unafiki.
18 And the harvest of righteousness is sown in peace by those who make peace. Mavuno ya haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]