Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

2 Chronicles 4 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 He made a bronze altar thirty feet long, thirty feet wide, and fifteen feet high. Mfalme Sulemani akatengeneza madhabahu ya shaba yenye urefu wa dhiraa ishirini, upana wa dhiraa ishirini na kimo chake dhiraa kumi.
2 He made the cast-metal Sea, round: fifteen feet across, seven and a half high, forty-five around. Akatengeneza Bahari ya kusubu, yenye umbo la mviringo, ya dhiraa kumi kutoka ukingo hadi ukingo na kimo cha dhiraa tano. Kamba ya urefu wa dhiraa thelathini ingeweza kuizunguka.
3 Below the rim, figures of oxen encircled it, about seven to every foot around the Sea, cast in two rows as one piece with it. Chini ya huo ukingo, kulikuwa na mafahali kuizunguka, yaani mafahali kumi katika kila dhiraa moja. Hayo mafahali waliyasubu katika safu mbili yakiwa ya kitu kimoja na hiyo Bahari.
4 The Sea stood on twelve oxen, three facing north, three west, three south, three east, resting on them, their hindquarters all inward. Bahari hiyo ilikaa juu ya mafahali kumi na wawili, mafahali watatu walielekeza nyuso zao kaskazini, watatu magharibi, watatu kusini, na watatu mashariki. Bahari hiyo ilikaa juu ya hao mafahali, nazo sehemu zao za nyuma zilielekeana.
5 About three inches thick, its rim like a cup's, like a lily's flower, holding about 17,000 gallons. Unene wake ulikuwa nyanda moja, na ukingo wake ulifanana na ukingo wa kikombe, kama ua la yungiyungi iliyochanua. Ingejazwa na bathi elfu tatu.
6 He made ten washing basins, five south, five north, to rinse what was used for the burnt offerings; the Sea was for the priests to wash in. Kisha akatengeneza masinia kumi kwa ajili ya kuoshea vifaa, naye akayaweka matano upande wa kusini na matano upande wa kaskazini. Ndani yake ndimo walioshea vifaa vya kutumika katika sadaka za kuteketezwa, lakini ile Bahari ilikuwa ya makuhani kunawia.
7 He made ten gold lampstands as specified, five for the temple's south side, five for the north. Akatengeneza vinara kumi vya taa vya dhahabu kama ilivyoainishwa na kuviweka hekaluni, vinara vitano upande wa kusini, na vitano upande wa kaskazini.
8 He made ten tables, placed them in the temple—five south, five north—and one hundred gold basins. Akatengeneza meza kumi na kuziweka hekaluni, tano upande wa kusini na tano upande wa kaskazini. Pia akatengeneza mabakuli mia moja ya dhahabu ya kunyunyizia.
9 He made the priests' court, the great court, its doors, and plated their doors with bronze. Akatengeneza ukumbi wa makuhani, na ukumbi mwingine mkubwa na milango yake, naye akaifunika hiyo milango kwa shaba.
10 He placed the Sea on the south side, at the southeast corner. Akaiweka ile Bahari upande wa kusini, kwenye pembe ya kusini-mashariki mwa nyumba.
11 Huram made the pots, shovels, and basins. So Huram finished the work he did for King Solomon in the house of our Father: Huramu pia akatengeneza masufuria, masepetu na mabakuli ya kunyunyizia. Kwa hiyo Huramu akakamilisha kazi katika Hekalu la Mungu kama vile Mfalme Sulemani alikuwa amemwagiza:
12 the two pillars; the two bowl-shaped capitals atop the pillars; the two networks covering those capitals; zile nguzo mbili; yale mataji mawili yaliyokuwa juu ya hizo nguzo, zile nyavu mbili za kupamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli yaliyowekwa juu ya zile nguzo;
13 400 pomegranates for the two networks, two rows each, covering the two capital bowls on the pillars; yale makomamanga mia nne kwa ajili ya hizo nyavu mbili (safu mbili za makomamanga kwa kila wavu yakipamba hayo mataji mawili yenye umbo la bakuli juu ya hizo nguzo);
14 the stands and the basins on the stands; vishikio pamoja na masinia yake;
15 the one Sea and the twelve oxen beneath it. hiyo Bahari na hao mafahali kumi na wawili chini yake;
16 Pots, shovels, meat forks, and all their utensils—Huram-abi made these for King Solomon, for our Father's house, of polished bronze. pia hayo masufuria, masepetu, uma za nyama na vyombo vingine vyote vilivyohusiana. Vitu vyote ambavyo Huram-Abi alimtengenezea Mfalme Sulemani kwa ajili ya Hekalu la Mwenyezi Mungu vilikuwa vya shaba iliyosuguliwa.
17 The king had them cast in clay molds in the Jordan plain between Succoth and Zeredah. Mfalme aliagiza wavisubu vitu hivi kwenye kalibu za udongo wa mfinyanzi katika uwanda wa Yordani kati ya Sukothi na Sereda.
18 Solomon made all these items in such quantity that the bronze weight could not be determined. Vitu hivi vyote Mfalme Sulemani alivyotengeneza vilikuwa vingi sana hivi kwamba uzani wa shaba haungekadirika.
19 Solomon made all the furnishings for our Father's house: the golden altar and tables with the bread of the Presence. Sulemani pia akatengeneza samani zote zilizokuwa ndani ya Hekalu la Mungu: madhabahu ya dhahabu; meza za kuweka mikate ya Wonesho;
20 The pure gold lampstands with their lamps, to burn before the inner sanctuary as prescribed; vinara vya taa vya dhahabu safi pamoja na taa zake ili ziwake mbele ya mahali patakatifu kama ilivyoelekezwa;
21 the gold flowers, lamps, and tongs (these were of the purest gold). maua ya dhahabu yaliyofanyizwa, taa na makoleo (vilikuwa vya dhahabu bora kabisa);
22 Pure gold: the wick trimmers, sprinkling bowls, dishes, censers, and the temple's doorways—inner doors to the Most Holy Place, and the main hall's doors. mikasi ya dhahabu safi, mabakuli ya kunyunyizia, masinia na vyetezo; milango ya dhahabu ya Hekalu: yaani milango ya ndani ya Patakatifu pa Patakatifu, na milango ya ukumbi mkuu.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]