Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Numbers 1 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 Our Father spoke to Moses in the Sinai wilderness, in the tent of meeting, on the first day of the second month of the second year after they left the land of Egypt. He said: Mwenyezi Mungu alisema na Musa katika Jangwa la Sinai, katika Hema la Kukutania, siku ya kwanza ya mwezi wa pili, katika mwaka wa pili baada ya Waisraeli kutoka nchi ya Misri. Akamwambia,
2 "Count the whole community of Israel's people, by clans and fathers' houses—every male, by name, head by head. “Hesabu watu wa jumuiya yote ya Waisraeli kwa kufuata koo zao na jamaa zao, ukiorodhesha kila mwanaume kwa jina lake, mmoja mmoja.
3 Register everyone in Israel twenty and older who can serve in the army—you and Aaron—by their divisions. Wewe na Haruni mtawahesabu kwa migawanyo yao wanaume wote katika Israeli wenye miaka ishirini na kuendelea wanaoweza kutumika katika jeshi.
4 A man from each tribe is to be with you, each one the head of his family. Mwanaume mmoja kutoka kila kabila, kila aliye kiongozi wa jamaa yake, atawasaidia.
5 "Names of the men who will stand with you: from Reuben, Elizur son of Shedeur. “Haya ndiyo majina ya wanaume watakaowasaidia: “kutoka Reubeni, ni Elisuri mwana wa Shedeuri;
6 "From Simeon, Shelumiel son of Zurishaddai; kutoka Simeoni, ni Shelumieli mwana wa Surishadai;
7 "From Judah, Nahshon son of Amminadab; kutoka Yuda, ni Nashoni mwana wa Aminadabu;
8 "From Issachar, Nethanel son of Zuar; kutoka Isakari, ni Nethaneli mwana wa Suari;
9 "From Zebulun, Eliab son of Helon; kutoka Zabuloni, ni Eliabu mwana wa Heloni;
10 "From the sons of Joseph: from Ephraim, Elishama son of Ammihud; from Manasseh, Gamaliel son of Pedahzur; kutoka wana wa Yusufu: kutoka Efraimu, ni Elishama mwana wa Amihudi; kutoka Manase, ni Gamalieli mwana wa Pedasuri;
11 "From Benjamin, Abidan son of Gideoni; kutoka Benyamini, ni Abidani mwana wa Gideoni;
12 "From Dan, Ahiezer son of Ammishaddai; kutoka Dani, ni Ahiezeri mwana wa Amishadai;
13 "From Asher, Pagiel son of Ochran; kutoka Asheri, ni Pagieli mwana wa Okrani;
14 "From Gad, Eliasaph son of Deuel; kutoka Gadi, ni Eliasafu mwana wa Deueli;
15 "From Naphtali, Ahira son of Enan. kutoka Naftali, ni Ahira mwana wa Enani.”
16 "These were the community's called ones, leaders of their ancestral tribes, heads of Israel's clans." Hawa walikuwa wanaume walioteuliwa kutoka jumuiya, viongozi wa makabila ya baba zao. Walikuwa wakuu wa koo za Israeli.
17 So Moses and Aaron took these men who had been designated by name, Musa na Haruni wakawachukua wanaume hao waliokuwa wamepewa majina yao,
18 on the first day of the second month they gathered the whole community. The people registered their ancestry by clan and family—every male twenty years old and older, listed by name, one by one, wakaita jumuiya yote pamoja katika siku ya kwanza ya mwezi wa pili. Watu wakaonesha nasaba zao kwa koo zao na jamaa zao, nao wanaume waliokuwa na miaka ishirini au zaidi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja,
19 as our Father had commanded Moses. So Moses counted them in the wilderness of Sinai. kama Mwenyezi Mungu alivyomwagiza Musa. Hivyo aliwahesabu katika Jangwa la Sinai:
20 From Reuben's descendants, Israel's firstborn: recorded by clan and family, name by name, every male twenty years old and up, able to serve in war. Kutoka wazao wa Reubeni, mzaliwa wa kwanza wa kiume wa Israeli: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
21 Those counted from the tribe of Reuben were 46,500. Idadi kutoka kabila la Reubeni ilikuwa watu elfu arobaini na sita na mia tano.
22 Simeon's descendants, by clans and families, counted by name, head by head: every male twenty years old and up, fit for the army. Kutoka wazao wa Simeoni: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi walihesabiwa na kuorodheshwa kwa majina, mmoja mmoja, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
23 Those counted from the tribe of Simeon were 59,300. Idadi kutoka kabila la Simeoni walikuwa watu elfu hamsini na tisa na mia tatu.
24 From Gad's descendants: by clans, families, and names, every man twenty and older fit for military service. Kutoka wazao wa Gadi: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
25 Those counted from the tribe of Gad were 45,650. Idadi kutoka kabila la Gadi walikuwa watu elfu arobaini na tano, mia sita na hamsini.
26 Judah's descendants, listed by clans and families, by name, every man twenty and older able to serve in the army: Kutoka wazao wa Yuda: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
27 those counted from the tribe of Judah were 74,600. Idadi kutoka kabila la Yuda walikuwa watu elfu sabini na nne na mia sita.
28 Issachar's descendants, listed by clan and family, by name, every man twenty years and older fit for war: Kutoka wazao wa Isakari: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
29 those counted from the tribe of Issachar were 54,400. Idadi kutoka kabila la Isakari walikuwa watu elfu hamsini na nne na mia nne.
30 Zebulun's descendants: registered by clan and family, by name, every man twenty years old or older fit for military service. Kutoka wazao wa Zabuloni: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
31 Those counted from the tribe of Zebulun were 57,400. Idadi kutoka kabila la Zabuloni walikuwa watu elfu hamsini na saba na mia nne.
32 Sons of Joseph, Ephraim's line: recorded by clan and family, by name, every man twenty and older fit for military service. Kutoka wana wa Yusufu: Kutoka wazao wa Efraimu: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
33 Those counted from the tribe of Ephraim were 40,500. Idadi kutoka kabila la Efraimu walikuwa watu elfu arobaini na mia tano.
34 Manasseh's descendants, listed by clans and families, by name, each man twenty years or older able to serve in the army: Kutoka wazao wa Manase: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
35 those counted from the tribe of Manasseh were 32,200. Idadi kutoka kabila la Manase walikuwa watu elfu thelathini na mbili na mia mbili.
36 From Benjamin's descendants, recorded by clan and family, by name, every man twenty years old and older, fit for military service: Kutoka wazao wa Benyamini: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
37 those counted from the tribe of Benjamin were 35,400. Idadi kutoka kabila la Benyamini walikuwa watu elfu thelathini na tano na mia nne.
38 From Dan's descendants, listed by clan and family, by name, every man twenty years old and older fit for war: Kutoka wazao wa Dani: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
39 those counted from the tribe of Dan were 62,700. Idadi kutoka kabila la Dani walikuwa watu elfu sitini na mbili na mia saba.
40 Asher's descendants, listed by clan and family, by name: every man twenty years old and up, fit for military service. Kutoka wazao wa Asheri: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
41 Those counted from the tribe of Asher were 41,500. Idadi kutoka kabila la Asheri walikuwa watu elfu arobaini na moja na mia tano.
42 Naphtali's descendants: by clan and family, counted by name, every man twenty and older fit for war. Kutoka wazao wa Naftali: Wanaume wote waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi waliorodheshwa kwa majina, kufuatana na kumbukumbu za koo zao na jamaa zao.
43 Those counted from the tribe of Naphtali were 53,400. Idadi kutoka kabila la Naftali walikuwa watu elfu hamsini na tatu na mia nne.
44 Moses, Aaron, and Israel's twelve leaders counted these men, each for his family. Hawa walikuwa wanaume waliohesabiwa na Musa, Haruni na viongozi kumi na wawili wa Israeli, kila mmoja akiwakilisha jamaa yake.
45 All Israel's people were counted by families, every man twenty years old and older, fit to serve in Israel's army. Wanaume wote Waisraeli waliokuwa na miaka ishirini au zaidi ambao waliweza kutumika katika jeshi la Israeli walihesabiwa kufuatana na jamaa zao.
46 All those counted came to 603,550. Jumla ya hesabu yao ilikuwa watu elfu mia sita na tatu mia tano na hamsini (603,550).
47 But the Levites were not counted among them by their ancestral tribe. Hata hivyo, jamaa ya kabila la Lawi hawakuhesabiwa pamoja na wengine.
48 For our Father had said to Moses: Mwenyezi Mungu alikuwa amemwambia Musa:
49 "Do not count the tribe of Levi or list them among the Israelites. “Kamwe usihesabu kabila la Lawi wala kuwaweka pamoja katika hesabu ya Waisraeli wengine.
50 Instead, put the Levites in charge of the tabernacle of the testimony, all its furnishings, and everything belonging to it. They must carry the tabernacle and its furnishings, care for it, and camp around it. Badala yake, waweke Walawi kuwa viongozi wa Maskani ya Ushuhuda, juu ya samani zake na kila kitu kilicho ndani yake. Wao watabeba Maskani na samani zake zote; wataitunza na kupiga kambi kuizunguka.
51 When the tabernacle sets out, Levites take it down; when it is pitched, Levites set it up. Any outsider who comes near is to be put to death. Wakati wowote Maskani inapohamishwa, Walawi wataifungua, na wakati wowote Maskani inapotakiwa kusimamishwa, Walawi watafanya kazi hiyo. Mtu yeyote mwingine ambaye atasogea karibu nayo atauawa.
52 Israel's people are to camp, each by his own camp, each under his own banner, by their companies. Waisraeli watapiga mahema yao kwa makundi makundi, kila mwanaume katika kambi yake mwenyewe chini ya bendera yake.
53 The Levites must camp around the tabernacle of the testimony, so no wrath falls on the Israelite community; the Levites are to guard the tabernacle of the testimony." Hata hivyo, Walawi watapiga mahema yao kuzunguka Maskani ya Ushuhuda ili ghadhabu isiipate jumuiya ya Waisraeli. Walawi watawajibika kwa utunzaji wa Maskani ya Ushuhuda.”
54 The people of Israel did everything our Father had commanded Moses; that is exactly what they did. Waisraeli walifanya haya yote kama Mwenyezi Mungu alivyomwamuru Musa.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]