Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

Mark 14 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 Two days before Passover and Unleavened Bread, the chief priests and scribes were looking for a way to seize Jesus by trickery and kill him. Zilikuwa zimebaki siku mbili tu kabla ya Sikukuu ya Pasaka, na Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu. Viongozi wa makuhani na walimu wa Torati walikuwa wakitafuta njia ya kumkamata Isa kwa hila na kumuua.
2 For they said, "Not during the feast, or the people might riot." Lakini walisema, “Tusilifanye jambo hili wakati wa Sikukuu, maana watu wanaweza wakafanya ghasia.”
3 While he was in Bethany, in Simon the leper's house, reclining at the table, a woman came with an alabaster flask of pure nard perfume, very costly. She broke the flask and poured it on his head. Isa alikuwa Bethania nyumbani mwa Simoni aliyekuwa na ukoma. Alipokuwa ameketi mezani akila chakula cha jioni, mwanamke mmoja aliingia akiwa na chupa ya marhamu yenye manukato ya nardo safi ya thamani kubwa. Akaivunja hiyo chupa, akamiminia hayo manukato kichwani mwa Isa.
4 There were some who said to themselves indignantly, "Why was this perfume wasted like that? Baadhi ya watu waliokuwa pale walikasirika na wakasemezana, “Upotevu huu wote wa manukato ni wa nini?
5 For this perfume could have sold for over 300 denarii and given to the poor." And they scolded her. Manukato haya yangeuzwa kwa zaidi ya dinari mia tatu, na fedha hizo wakapewa maskini.” Wakamkemea vikali huyo mwanamke.
6 But Jesus said, "Leave her alone. Why trouble her? She has done a beautiful thing for me. Lakini Isa akawaambia, “Mbona mnamsumbua huyu mwanamke? Mwacheni! Yeye amenitendea jambo zuri sana.
7 For the poor are always with you, and you can do good for them whenever you want; but you won't always have me. Maskini mtakuwa nao siku zote na mnaweza kuwasaidia wakati wowote mnaotaka. Lakini mimi hamtakuwa nami siku zote.
8 She has done what she could; she has anointed my body beforehand for burial. Huyu mwanamke amenitendea lile aliloweza. Ameumiminia mwili wangu manukato ili kuniandaa kwa maziko yangu.
9 Truly, I tell you, wherever the gospel is preached worldwide, what she did will be told in memory of her." Amin, nawaambia, mahali popote ulimwenguni ambapo Injili itahubiriwa, jambo hili alilolitenda huyu mwanamke litatajwa pia kwa ukumbusho wake.”
10 Then Judas Iscariot, one of the twelve, went to the chief priests to betray Jesus to them. Kisha Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi kumi na wawili, akaenda kwa viongozi wa makuhani ili kumsaliti Isa kwao.
11 Hearing this, they were glad and promised him money. So he looked for a chance to betray Jesus. Walifurahi sana kusikia jambo hili na wakaahidi kumpa fedha. Hivyo yeye akawa anatafuta wakati uliofaa wa kumsaliti.
12 On the first day of Unleavened Bread, when they sacrificed the Passover lamb, his disciples asked him, "Where do you want us to go and prepare for you to eat the Passover?" Siku ya kwanza ya Sikukuu ya Mikate Isiyotiwa Chachu, siku ambayo kwa desturi mwana-kondoo wa Pasaka huchinjwa, wanafunzi wa Isa wakamuuliza, “Unataka twende wapi ili tukuandalie mahali pa kula Pasaka?”
13 He sent two of his disciples, "Go into the city; a man carrying a jar of water will meet you. Follow him, Basi akawatuma wawili miongoni mwa wanafunzi wake, akawaambia, “Nendeni mjini. Huko mtakutana na mwanaume amebeba mtungi wa maji. Mfuateni.
14 and wherever he enters, tell the house's owner, 'The Teacher says: Where is my guest room, where I may eat the Passover with my disciples?' Mwambieni mwenye nyumba ile atakayoingia, ‘Mwalimu anauliza: Kiko wapi chumba changu cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka?’
15 And he will show you a large upper room furnished and ready; there prepare for us." Atawaonesha chumba kikubwa ghorofani, kilichopambwa tena kilicho tayari. Tuandalieni humo.”
16 The disciples left, went to the city, found things as he had told them, and prepared the Passover. Wale wanafunzi wakaondoka na kwenda mjini, nao wakakuta kila kitu kama Isa alivyowaambia. Hivyo wakaiandaa Pasaka.
17 And when it was evening, Jesus came with the twelve. Ilipofika jioni, Isa akaja pamoja na wale wanafunzi wake kumi na wawili.
18 While they reclined and ate, Jesus said, "Truly, I tell you, one of you will betray me, one eating with me." Walipoketi mezani wakila, Isa akawaambia, “Amin, nawaambia, mmoja wenu atanisaliti, mmoja anayekula pamoja nami.”
19 They began to grieve and ask him, one by one, "Is it I?" Wakaanza kuhuzunika na kumuuliza mmoja baada ya mwingine, “Je, ni mimi, Bwana?”
20 He said to them, "One of the twelve, dipping bread with me into the dish. Akawajibu, “Ni mmoja miongoni mwenu ninyi kumi na wawili, yule anayechovya mkate kwenye bakuli pamoja nami.
21 The Son of Man goes as the Scriptures said about him, but how terrible for that man who betrays him—better if he had never been born." Mwana wa Adamu anaenda zake kama vile alivyoandikiwa. Lakini ole wake mtu yule amsalitiye Mwana wa Adamu! Ingekuwa heri kwake mtu huyo kama hangezaliwa.”
22 As they ate, he took bread, blessed it, broke it, gave it to them, and said, "Take; this is my body." Walipokuwa wanakula, Isa akachukua mkate, akashukuru, akaumega na kuwapa wanafunzi wake, akisema, “Twaeni mle; huu ndio mwili wangu.”
23 He took a cup, gave thanks, gave it to them, and they all drank from it. Kisha akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, nao wote wakanywa kutoka humo.
24 He said to them, "This is my blood of the covenant, poured out for many. Akawaambia, “Hii ndiyo damu yangu ya agano, imwagikayo kwa ajili ya wengi.
25 Truly I tell you, I will not drink wine again until that day when I drink it new in the kingdom of our Father." Amin, nawaambia, sitakunywa tena katika uzao wa mzabibu, hadi siku ile nitakapounywa mpya katika ufalme wa Mungu.”
26 And when they had sung a hymn, they went out to the Mount of Olives. Walipokwisha kuimba wimbo, wakatoka wakaenda Mlima wa Mizeituni.
27 Jesus said to them, "You will all stumble, for it's written: 'I will strike the shepherd, and the sheep will be scattered.' Isa akawaambia, “Ninyi nyote mtaniacha, kwa maana imeandikwa: “ ‘Nitampiga mchungaji, nao kondoo watatawanyika.’
28 But after I am raised up, I will go ahead of you to Galilee." Lakini baada ya kufufuka kwangu, nitawatangulia kwenda Galilaya.”
29 Peter said to him, "Even though they all fall away, I will not." Petro akasema, “Hata kama wengine wote watakuacha, mimi sitakuacha.”
30 Jesus said to him, "Truly I tell you, today, this night, before the rooster crows twice, you will deny me three times." Isa akamwambia, “Amin, nakuambia; leo, usiku huu, kabla jogoo hajawika mara mbili, wewe mwenyewe utanikana mara tatu.”
31 But he insisted, "Even if I must die with you, I will never deny you." They all said the same. Lakini Petro akasisitiza zaidi, “Hata kama itabidi kufa pamoja nawe, sitakukana kamwe.” Nao wale wengine wote wakasema vivyo hivyo.
32 They arrived at a place called Gethsemane, and he told his disciples, "Sit here while I pray." Wakaenda mahali paitwapo Gethsemane. Isa akawaambia wanafunzi wake, “Kaeni hapa, nami niende nikaombe.”
33 He took Peter, James, and John, and began to feel deep distress and anguish. Kisha akawachukua pamoja naye Petro, Yakobo na Yohana. Akaanza kuhuzunika sana na kutaabika.
34 He said to them, "My soul is crushed with grief, to death. Stay here and stay alert." Akawaambia, “Moyo wangu umejawa na huzuni kiasi cha kufa. Kaeni hapa na mkeshe.”
35 Going a little farther, he fell to the ground and prayed that, if possible, the hour would pass from him. Akaenda mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba kwamba kama ingewezekana saa hiyo ya mateso imwondokee.
36 He said, "Abba, Father, all things are possible for you. Take this cup from me—but let it be your will, not mine." Akasema, “Abba, Baba, mambo yote yawezekana kwako. Niondolee kikombe hiki. Lakini si kama nipendavyo mimi, bali vile upendavyo wewe.”
37 He returned, found them asleep, and said to Peter, "Simon, are you asleep? Couldn't you stay awake one hour? Akarudi kwa wanafunzi wake, akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, “Simoni, umelala? Je, hukuweza kukesha hata kwa saa moja?
38 Watch and pray, so you don't fall into temptation. The spirit is willing, but the flesh is weak." Kesheni na mwombe, msije mkaingia majaribuni. Roho iko radhi, lakini mwili ni mdhaifu.”
39 And again he went away and prayed, saying the same words. Akaenda tena kuomba, akisema maneno yale yale.
40 Again he found them sleeping, eyes heavy, not knowing how to answer him. Aliporudi, akawakuta tena wamelala kwa sababu macho yao yalikuwa mazito. Nao hawakujua la kumwambia.
41 He came a third time and said, "Still sleeping and resting? Enough—the hour has come. Look, the Son of Man is handed over into the hands of sinners. Akaja mara ya tatu, akawaambia, “Bado mmelala na kupumzika? Imetosha! Saa imewadia. Tazameni, Mwana wa Adamu anasalitiwa na kutiwa mikononi mwa wenye dhambi.
42 Rise, let us be going; see, my betrayer is here." Inukeni, twende zetu! Tazameni, msaliti wangu yuaja!”
43 While he was still speaking, Judas—one of the twelve—arrived, and with him a crowd with swords and clubs from the chief priests, scribes, and elders. Isa alipokuwa bado anazungumza, Yuda, mmoja wa wale kumi na wawili, akatokea. Alikuwa amefuatana na umati wa watu wenye panga na marungu, waliokuwa wametumwa na viongozi wa makuhani, walimu wa Torati, na wazee.
44 His betrayer had given them a signal: "The one I kiss is him—seize him and take him away securely." Basi msaliti alikuwa amewapa hao watu ishara, kwamba: “Yule nitakayembusu ndiye. Mkamateni, mkamchukue chini ya ulinzi.”
45 He came up to Jesus at once, said, "Rabbi!" and kissed him. Mara Yuda akamjia Isa na kusema, “Mwalimu.” Akambusu.
46 And they laid hands on him and seized him. Wale watu wakamkamata Isa, wakamweka chini ya ulinzi.
47 One of the bystanders drew his sword, struck the high priest's servant, and cut off his ear. Ndipo mmoja wa wale waliokuwa wamesimama karibu aliuchomoa upanga wake na kumpiga mtumishi wa kuhani mkuu, akamkata sikio.
48 Jesus said to them, "Have you come out with swords and clubs to seize me, like a robber? Kisha Isa akawaambia, “Mmekuja na panga na marungu kunikamata kana kwamba mimi ni mnyang’anyi?
49 Every day I was with you in the temple teaching, and you didn't arrest me. But let the Scriptures be fulfilled." Siku kwa siku nilikuwa pamoja nanyi nikifundisha Hekaluni, wala hamkunikamata. Lakini Maandiko sharti yatimie.”
50 And they all left him and fled. Ndipo wanafunzi wake wote wakamwacha, wakakimbia.
51 And a young man followed him, wearing nothing but a linen cloth. And they seized the young man, Kijana mmoja, aliyekuwa amevaa nguo ya kitani pekee, alikuwa akimfuata Isa. Walipomkamata,
52 but he left the linen cloth and ran away naked. alikimbia uchi, akaliacha vazi lake.
53 They led Jesus to the high priest, and all the chief priests and elders and scribes gathered. Wakampeleka Isa kwa kuhani mkuu, nao viongozi wa makuhani wote, na wazee na walimu wa Torati wote wakakusanyika pamoja.
54 Peter had followed at a distance, all the way into the high priest's courtyard, and sat with the guards, warming himself by the fire. Petro akamfuata kwa mbali, hadi uani kwa kuhani mkuu. Huko akaketi pamoja na walinzi, akiota moto.
55 The chief priests and the whole council sought testimony against Jesus to put him to death, but found none. Viongozi wa makuhani na Baraza la Wayahudi lote wakatafuta ushahidi dhidi ya Isa ili wapate kumuua. Lakini hawakupata jambo lolote.
56 For many gave false testimony against him, but their testimony did not agree. Wengi walitoa ushahidi wa uongo dhidi yake, lakini maelezo yao hayakukubaliana.
57 And some stood up and gave false testimony against him, saying, Ndipo wengine wakasimama wakatoa ushahidi wa uongo dhidi yake, wakisema:
58 "We heard him say, 'I will destroy this temple made by hands, and in three days build another not made by hands.'" “Sisi tulimsikia akisema, ‘Mimi nitalibomoa Hekalu hili lililojengwa na wanadamu, na katika siku tatu nitajenga jingine ambalo halikujengwa na wanadamu.’ ”
59 Yet even about this their testimony did not agree. Lakini hata hivyo, ushahidi wao haukukubaliana.
60 The high priest stood up in the midst and asked Jesus, "You have no answer? What are these men testifying against you?" Basi kuhani mkuu akasimama mbele yao, akamuuliza Isa, “Je, wewe hutajibu? Ni ushahidi gani hawa watu wanauleta dhidi yako?”
61 He stayed silent, answered nothing. Again the high priest asked him, "Are you the Christ, the Son of the Blessed?" Lakini Isa akakaa kimya, hakusema neno lolote. Kuhani mkuu akamuuliza tena, “Je, wewe ndiwe Al-Masihi, Mwana wa Mungu Aliyebarikiwa?”
62 Jesus said, "I AM, and you will see the Son of Man seated at the right hand of the Mighty One and coming with heaven's clouds." Isa akajibu, “Mimi ndimi. Nanyi mtamwona Mwana wa Adamu akiwa ameketi mkono wa kuume wa Mwenye Nguvu, na akija juu ya mawingu ya mbinguni.”
63 And the high priest tore his clothes and said, "What further witnesses do we need? Kuhani mkuu akayararua mavazi yake, akasema, “Tuna haja gani tena ya mashahidi zaidi?
64 You have heard his blasphemy. What is your decision?" And they all condemned him as deserving death. Ninyi mmesikia alivyokufuru. Uamuzi wenu ni gani?” Wote wakamhukumu kwamba anastahili kifo.
65 Some began spitting on him, covering his face, and punching him, saying to him, "Prophesy!" Then the guards slapped him. Kisha baadhi ya watu wakaanza kumtemea mate; wakamfunga kitambaa machoni, wakampiga kwa ngumi na kumwambia, “Tabiri!” Walinzi wakamchukua na kumpiga makofi.
66 While Peter was below in the courtyard, one of the high priest's servant girls came, Petro alipokuwa bado yuko chini uani, tazama akaja mmoja wa wajakazi wa kuhani mkuu.
67 seeing Peter warming himself, she looked at him and said, "You too were with the Nazarene, Jesus." Alipomwona Petro akiota moto, akamtazama sana, akamwambia, “Wewe pia ulikuwa pamoja na Isa, Mnasiri.”
68 But he denied it: "I don't know or understand what you mean." Then he went out to the entrance, and a rooster crowed. Lakini Petro akakana, akasema, “Sijui wala sielewi unalosema.” Naye akaondoka kuelekea kwenye njia ya kuingilia.
69 The servant girl saw him and again told the bystanders, "This man is one of them." Yule mjakazi alipomwona mahali pale, akawaambia tena wale waliokuwa wamesimama hapo, “Huyu mtu ni mmoja wao.”
70 But he denied it again. A little later the bystanders again told Peter, "You truly are one of them, for you're a Galilean." Lakini Petro akakana tena. Baada ya muda kidogo wale waliokuwa wamesimama hapo karibu na Petro wakamwambia, “Hakika wewe ni mmoja wao, kwa maana wewe pia ni Mgalilaya!”
71 He began to call down curses on himself and swear, "I don't know this man you're talking about." Petro akaanza kujilaani na kuwaapia, “Mimi simjui huyu mtu mnayesema habari zake!”
72 At once a rooster crowed a second time. Peter remembered Jesus' words: "Before the rooster crows twice, you will deny me three times." He broke down and wept. Papo hapo jogoo akawika mara ya pili. Ndipo Petro akakumbuka lile neno Isa alikuwa amemwambia: “Kabla jogoo hajawika mara mbili, utanikana mara tatu.” Akavunjika moyo, akalia sana.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]