Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

John 4 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 So when Jesus knew the Pharisees heard he was making and baptizing more disciples than John. Isa alipata habari kuwa Mafarisayo walisikia kwamba yeye alikuwa akipata wanafunzi kuliko Yahya na kuwabatiza,
2 (though Jesus himself was not baptizing, but his disciples were), ingawa kwa kweli si Isa mwenyewe aliyekuwa akibatiza, ila ni wanafunzi wake.
3 he left Judea and went back to Galilee. Bwana Isa alipojua mambo haya, aliondoka Yudea akarudi tena Galilaya.
4 And he had to pass through Samaria. Wakati huo ilimlazimu apitie Samaria.
5 So he came to a town of Samaria called Sychar, near the field Jacob gave his son Joseph. Akafika kwenye mji mmoja wa Samaria uitwao Sikari, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa mwanawe Yusufu.
6 Jacob's well was there. Jesus, tired from the trip, sat down at the well—about noon. Kisima cha Yakobo kilikuwa huko. Naye Isa alikuwa amechoka kwa kuwa alikuwa ametoka safarini. Akaketi karibu na hicho kisima. Ilikuwa yapata saa sita mchana.
7 A woman of Samaria came to draw water. Jesus said to her, "Give me a drink." Mwanamke mmoja Msamaria alipokuja kuteka maji, Isa akamwambia, “Naomba maji ninywe.”
8 (For his disciples had gone into the town to buy food.). (Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wameenda mjini kununua chakula.)
9 The Samaritan woman said, "You're a Jew; why ask me, a Samaritan woman, for a drink?" (Jews don't associate with Samaritans.). Yule mwanamke Msamaria akamjibu, “Wewe ni Myahudi na mimi ni Msamaria. Yawezekanaje uniombe maji ya kunywa?” (Wayahudi walikuwa hawashirikiani kabisa na Wasamaria.)
10 Jesus answered her, "If you knew our Father's gift, and who asks you, 'Give me a drink,' you'd have asked him, and he'd have given you living water." Isa akamjibu, “Kama ungeijua karama ya Mungu, na ni nani anakuomba maji ya kunywa, ungemwomba yeye, naye angekupa maji ya uzima.”
11 The woman said to him, "Sir, you have nothing to draw with, and the well is deep. Where then do you get this living water? Yule mwanamke akamjibu, “Bwana, wewe huna chombo cha kutekea maji na kisima hiki ni kirefu. Hayo maji ya uzima utayapata wapi?
12 Are you greater than our father Jacob, who gave us the well, drank from it himself, with his sons and livestock?" Kwani wewe ni mkuu kuliko baba yetu Yakobo ambaye alitupatia kisima hiki, ambacho yeye pamoja na watoto wake na mifugo yake walikitumia?”
13 Jesus said to her, "Everyone who drinks of this water will be thirsty again, Isa akamjibu, “Kila mtu anayekunywa maji ya kisima hiki ataona kiu tena.
14 but whoever drinks the water I give him will never thirst again; that water will become in him a spring of water welling up to eternal life." Lakini yeyote anywaye maji nitakayompa hataona kiu kamwe. Maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika uzima wa milele.”
15 The woman said to him, "Sir, give me this water, so I won't get thirsty or come here to draw water." Yule mwanamke akamwambia, “Bwana, tafadhali nipe maji hayo ili nisipate kiu tena, wala nisije tena hapa kuteka maji!”
16 Jesus said to her, "Go, call your husband, and come back here." Isa akamjibu, “Nenda ukamwite mumeo, uje naye hapa.”
17 The woman answered, "I have no husband." Jesus told her, "You're right to say you have no husband. Yule mwanamke akajibu, “Sina mume.” Isa akamwambia, “Umesema kweli kuwa huna mume.
18 For you've had five husbands, and the man you have now isn't your husband. You've spoken the truth." Kwa maana umeshakuwa na wanaume watano, na mwanaume unayeishi naye sasa si mume wako! Umesema ukweli.”
19 The woman said to him, "Sir, I see that you are a prophet. Yule mwanamke akasema, “Bwana, naona bila shaka wewe ni nabii.
20 Our fathers worshiped on this mountain, but you say Jerusalem is where people must worship." Baba zetu waliabudu kwenye mlima huu, lakini ninyi Wayahudi mnasema ni lazima tukaabudu huko Yerusalemu.”
21 Jesus told her, "Woman, believe me: an hour is coming when you'll worship the Father neither on this mountain nor in Jerusalem. Isa akamjibu, “Mwanamke, niamini: wakati unakuja ambapo hamtamwabudu Baba katika mlima huu, wala huko Yerusalemu.
22 You worship what you don't know; we worship what we know—salvation comes from the Jews. Ninyi Wasamaria mnaabudu msichokijua. Sisi Wayahudi tunamwabudu Mungu tunayemjua kwa sababu wokovu unatoka kwa Wayahudi.
23 But a time is coming, and now is, when true worshipers worship the Father in spirit and truth—for the Father seeks such worshipers. Lakini saa yaja, tena ipo, ambapo wale waabuduo halisi watamwabudu Baba katika roho na kweli. Kwa maana Baba anawatafuta watu wanaomwabudu kwa namna hii.
24 The Father is spirit, and those who worship him must worship in spirit and truth." Mungu ni Roho, na wote wanaomwabudu imewapasa kumwabudu katika roho na kweli.”
25 The woman said to him, "I know Messiah—the one called Christ—is coming. When he comes, he will tell us everything." Yule mwanamke akamwambia, “Ninafahamu kwamba Al-Masihi” (yaani Aliyetiwa mafuta) “anakuja. Yeye akija, atatueleza mambo yote.”
26 Jesus said to her, "I am he—the one speaking to you." Isa akamwambia, “Mimi ninayezungumza nawe, ndiye.”
27 Just then his disciples returned, amazed he was talking with a woman. Yet no one said, "What do you want?" or, "Why talk with her?" Wakati huo wanafunzi wake wakarudi, wakashangaa sana kumwona akizungumza na mwanamke. Lakini hakuna aliyemuuliza, “Unataka nini kwake?” Au, “Kwa nini unazungumza naye?”
28 So the woman left her water jar and went back to town and said to the people, Yule mwanamke akaacha mtungi wake, akarudi mjini, akawaambia watu,
29 "Come, see a man who told me everything I ever did. Could this be the Christ?" “Njooni mkamwone mtu aliyeniambia kila kitu nilichotenda! Je, yawezekana huyu ndiye Al-Masihi?”
30 They left the town and were coming to him. Basi wakamiminika watu kutoka mjini, wakamwendea Isa.
31 Meanwhile the disciples were urging him, "Rabbi, eat." Wakati huo wanafunzi wake walikuwa wakimsihi, “Mwalimu, kula.”
32 But he said to them, "I have food to eat that you know nothing about." Lakini yeye akawajibu, “Mimi ninacho chakula ambacho ninyi hamkifahamu.”
33 So the disciples said to one another, "Has anyone brought him something to eat?" Basi wanafunzi wakaanza kuulizana, “Kuna mtu ambaye amemletea chakula?”
34 Jesus said to them, "My food is doing the will of the one who sent me and finishing his work. Lakini Isa akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma na kuikamilisha kazi yake.
35 Don't you say, 'Four months more, then harvest comes'? Look, I tell you: raise your eyes, see the fields—white for harvest. Je, ninyi hamsemi, ‘Bado miezi minne tuvune’? Inueni macho yenu myaangalie mashamba jinsi mazao yalivyo tayari kuvunwa!
36 Already the harvester earns wages, gathering fruit for eternal life, so that planter and harvester may rejoice together. Mvunaji tayari anapokea mshahara wake, naye anakusanya mazao kwa ajili ya uzima wa milele, ili yeye apandaye na yeye avunaye wafurahi pamoja.
37 For here the saying holds true: 'One plants and another harvests.' Hivyo ule msemo, ‘Mmoja hupanda na mwingine huvuna,’ ni kweli kabisa.
38 I sent you to reap what you didn't work for. Others worked, and you have entered into their labor." Niliwatuma mkavune mazao ambayo hamkupanda. Wengine walifanya kazi ngumu, nanyi mmevuna faida ya taabu yao.”
39 Many Samaritans from that town believed in him because of the woman's testimony: "He told me everything I ever did." Wasamaria wengi katika mji ule wakamwamini Isa kwa sababu ya ushuhuda wa yule mwanamke alipowaambia kwamba, “Ameniambia kila kitu nilichotenda.”
40 When the Samaritans came to him, they asked him to stay with them; he stayed two days. Hivyo wale Wasamaria walipomjia, wakamsihi akae kwao. Naye akakaa huko siku mbili.
41 And many more believed because of his word. Kwa sababu ya neno lake, watu wengi wakaamini.
42 They told the woman, "It is no longer because of what you said that we believe—we've heard for ourselves, and we know this man truly is the Savior of the world." Wakamwambia yule mwanamke, “Sasa tunaamini, wala si kwa sababu ya maneno yako tu, bali kwa kuwa tumemsikia sisi wenyewe. Tumejua hakika kwamba huyu ndiye Al-Masihi, Mwokozi wa ulimwengu.”
43 After the two days he departed from there for Galilee. Baada ya zile siku mbili, Isa aliondoka kwenda Galilaya.
44 (For Jesus himself had testified that a prophet has no honor in his own hometown.). (Basi Isa mwenyewe alikuwa amesema kwamba nabii hapati heshima katika nchi yake mwenyewe.)
45 When he arrived in Galilee, the Galileans welcomed him, having seen all he did in Jerusalem at the feast—they too had gone to the feast. Alipofika Galilaya, Wagalilaya walimkaribisha, kwani walikuwa wameona yale aliyoyatenda huko Yerusalemu wakati wa Sikukuu ya Pasaka. Kwa maana wao pia walikuwa wamehudhuria hiyo Sikukuu.
46 He went again to Cana in Galilee, where he had turned water to wine. A royal official's son was sick at Capernaum. Hivyo Isa akafika tena Kana ya Galilaya, kule alikuwa amebadili maji kuwa divai. Kulikuwa na afisa mmoja wa mfalme, ambaye mwanawe alikuwa mgonjwa huko Kapernaumu.
47 Hearing that Jesus had come from Judea to Galilee, he went to him and begged him to come down and heal his son, who was about to die. Huyo mtu aliposikia kwamba Isa alikuwa amewasili Galilaya kutoka Yudea, alimwendea na kumsihi aende akamponye mwanawe, aliyekuwa mgonjwa karibu ya kufa.
48 So Jesus said to him, "Unless you people see signs and wonders, you will never believe." Isa akamwambia, “Ninyi watu msipoona ishara na miujiza kamwe hamtaamini.”
49 The royal official said to him, "Sir, come down before my child dies." Yule afisa wa mfalme akamwambia, “Bwana, tafadhali shuka kabla mwanangu hajafa.”
50 Jesus said to him, "Go; your son will live." The man believed what Jesus told him and left. Isa akamjibu, “Nenda zako, mwanao yu hai.” Yule afisa akaamini yale maneno Isa aliyomwambia, akaenda zake.
51 As he was going down, his servants met him and told him that his boy was living. Alipokuwa bado yuko njiani, akakutana na watumishi wake, wakamwambia kwamba mwanawe yu mzima.
52 So he asked them the hour he improved, and they said, "Yesterday at the seventh hour, the fever left him." Akawauliza saa ambayo alianza kupata nafuu. Wakamwambia, “Jana saa saba, ndipo homa iliisha.”
53 So the father knew this was the hour when Jesus told him, "Your son will live." He and his whole household believed. Ndipo baba wa huyo mtoto akakumbuka kuwa huo ndio wakati Isa alikuwa amemwambia, “Mwanao yu hai.” Kwa hiyo yeye na wote wa nyumbani mwake wakamwamini Isa.
54 This was now the second sign that Jesus did when he had come from Judea to Galilee. Hii ilikuwa ishara ya pili ambayo Isa alifanya aliporudi Galilaya kutoka Yudea.
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]