Skip to content
The Believer's Library

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024

John 17 ONMM

Show ONMM only
Verse × ×
1 After saying this, Jesus looked up to heaven and said: "Father, the hour has come. Glorify your Son, so the Son may glorify you, Baada ya Isa kusema haya, alitazama kuelekea mbinguni akawaombea na kusema: “Baba, saa imewadia. Mtukuze Mwanao, ili Mwanao apate kukutukuza wewe.
2 since you gave him authority over all people, to give eternal life to all you gave him. Kwa kuwa umempa mamlaka juu ya wote wenye mwili ili awape uzima wa milele wale uliompa.
3 This is eternal life: that they know you, the only true Father, and Jesus Christ whom you sent. Nao uzima wa milele ndio huu: wakujue wewe uliye Mungu wa pekee wa kweli, na Isa Al-Masihi uliyemtuma.
4 I glorified you on the earth, having finished the work you gave me to do. Nimekutukuza wewe duniani kwa kuitimiza ile kazi uliyonipa niifanye.
5 Father, glorify me now with yourself, with the glory I had with you before the world existed. Hivyo sasa, Baba, unitukuze mbele zako kwa ule utukufu niliokuwa nao pamoja na wewe kabla ulimwengu haujaumbwa.
6 I revealed your name to those you gave me from the world. They were yours; you gave them to me, and they have kept your word. “Nimelidhihirisha jina lako kwa wale ulionipa kutoka ulimwengu. Walikuwa wako, nawe ukanipa mimi, nao wamelitii neno lako.
7 Now they know that everything you have given me is from you, Sasa wamejua ya kuwa vyote ulivyonipa vimetoka kwako,
8 for I gave them the words you gave me; they received them, truly knew I came from you, and believed you sent me. kwa kuwa maneno yale uliyonipa nimewapa wao, nao wameyapokea na kujua kwamba kweli nimetoka kwako, nao wameamini kuwa wewe ulinituma.
9 I pray for them, not for the world, but for those you gave me, since they are yours. Ninawaombea wao. Siuombei ulimwengu, bali nawaombea wale ulionipa kwa sababu wao ni wako.
10 Everything mine is yours, and yours is mine, and I am glorified in them. Wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu, nami nimetukuzwa ndani yao.
11 I'm no longer in the world, but they are in the world, and I'm coming to you. Holy Father, keep them in your name, the name you gave me, so they may be one as we are. Mimi sasa simo tena ulimwenguni, lakini wao bado wamo ulimwenguni, nami naja kwako. Baba Mtakatifu, uwalinde kwa uweza wa jina lako ulilonipa, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja.
12 While with them, I kept them in your name you gave me. I guarded them—none was lost except the son of destruction, so Scripture would be fulfilled. Nilipokuwa pamoja nao, niliwalinda, wakawa salama kwa lile jina ulilonipa. Hakuna hata mmoja aliyepotea, isipokuwa yule aliyekusudiwa upotevu, ili Maandiko yapate kutimia.
13 Now I come to you, and I say these things in the world so they may have my joy completed in themselves. “Lakini sasa naja kwako, nami ninasema mambo haya wakati bado nikiwa ulimwenguni, ili wawe na furaha yangu kamili ndani yao.
14 I've given them your word; the world hated them, since they're not of the world, just as I'm not of the world. Nimewapa neno lako, nao ulimwengu umewachukia, kwa kuwa wao si wa ulimwengu kama mimi nisivyo wa ulimwengu huu.
15 I don't ask you to remove them from the world, but to guard them from the evil one. Siombi kwamba uwaondoe ulimwenguni, bali uwalinde dhidi ya yule mwovu.
16 They are not of the world, just as I am not of the world. Wao si wa ulimwengu huu, kama vile mimi nisivyo wa ulimwengu.
17 Make them holy by truth; your word is truth. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndilo kweli.
18 As you sent me into the world, so I have sent them into the world. Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami nawatuma vivyo hivyo.
19 For them I make myself holy, so they too may be made holy in truth. Kwa ajili yao najiweka wakfu ili wao nao wapate kutakaswa katika ile kweli.
20 I pray not only for these, but also for those who will believe in me through their word. “Siwaombei hawa peke yao, bali nawaombea na wale wote watakaoniamini kupitia neno lao,
21 Father, let them all be one, as you're in me and I in you, so they're in us too, and the world believes you sent me. ili wawe na umoja kama vile wewe Baba ulivyo ndani yangu na mimi nilivyo ndani yako. Wao nao wawe ndani yetu, ili ulimwengu upate kuamini ya kuwa wewe ndiwe uliyenituma mimi.
22 The glory you have given me, I have given them, so they may be one as we are one. Utukufu ule ulionipa nimewapa wao, ili wawe na umoja kama sisi tulivyo wamoja.
23 I in them and you in me, so they may be made completely one, so the world may know you sent me and loved them as you loved me. Mimi ndani yao na wewe ndani yangu: ili wawe wamekamilika katika umoja, na ulimwengu upate kujua ya kuwa umenituma, nami nimewapenda wao kama unavyonipenda mimi.
24 Father, I want those you gave me to be with me where I am, to see my glory, which you gave me because you loved me before the world was made. “Baba, shauku yangu ni kwamba wale ulionipa wawe pamoja nami pale nilipo, ili waweze kuuona utukufu wangu, yaani utukufu ule ulionipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.
25 Righteous Father—the world doesn't know you, but I know you, and these know you sent me. “Baba Mwenye Haki, ingawa ulimwengu haukujui, mimi ninakujua, nao wanajua ya kuwa umenituma.
26 I have made your name known to them, and will keep making it known, so the love you loved me with may be in them, and I in them." Nimefanya jina lako lijulikane kwao, nami nitaendelea kufanya lijulikane, ili upendo ule unaonipenda mimi uwe ndani yao, na mimi mwenyewe nipate kuwa ndani yao.”
FHB

Scripture from Father’s Heart Bible™. © 2026 Spirit Media Publishing, the imprint of Spirit Media Inc. All rights reserved. In Divine Voice™ Color, the words spoken by our Father show in blue, the words of the Son in red, and the words of the Spirit in purple.

ONMM

Biblica® Toleo Wazi Neno: Maandiko Matakatifu™ ONMM™ Hakimiliki © 2018, 2024 na Biblica, Inc. Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ Copyright © 2018, 2024 by Biblica, Inc.
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Scriptures™ 2024 · Creative Commons - Attribution-ShareAlike [CC BY-SA]